Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Kwa taarifa yako utarudi huku huku unapokudharau tukuzike.
Akili yako unaijua mwenyewe tu. Aliyekuambia naikana Tanzania ni nani? Tanzania ni nchi yangu, ulitaka nizikwe wapi sasa? Hivyo wewe ulitaka nitathmini maendeleo ya nchi yangu kutumia akili zako ama? HII ni tathmini yangu mimi wala si ya mtu mwingine yeyote yule, na lengo lake ni kuamsha mjadala na kuwastua wenye mamlaka ili wafanyie kazi .....ULITAKA NIDANGANYE KWA KUSEMA 1. DARAJA LA MFUGALE NI ZURI NA IMARA KULIKO YOTE YALIYOKO DUNIANI 2. AIRPORT YA DSM NI NZURI NA KUBWA KULIKO SCHIPHOL? PIA ULITAKA NISEME DSM NI MJI SAFI NA UNA NYUMA ZILIZOPANGWA VIZURI KULIKO LONDON? N.K NINGESEMA HAYA NDIYO UNGEFURAHI? NA JE NINGEKUWA SAHIHI? ACHA UPUUZI, ULITAKA NISEME WATANZANIA NI MATAJIRI NA WANAISHI MAISHA BORA?
 
Huyu jamaa ni fala, zuzu, limbukeni wa maisha na juha kwa pamoja.
Angefahamu hata kiduchu kuhusu historia ya jinsi nchi za ulaya zilivyojitajirisha kwa kuzinyonya nchi za dunia ya tatu, ikiwemo Tanzania, labda mshipa wa aibu ungemshikisha breki.

Na ukimwuliza umemsaidiaje baba yako kwa kumjengea angalau ka ghorofa tu kama kaulaya, ili naye ajisikie ana mtoto anayeishi Ulaya, domo litambaki wazi!
Amemaliza zizi la kuku la mama yake fukara na kumwachia manyoya tu, huku akiendelea kujitoa ufahamu. Boya sana huyu jamaa.
AKILI ZAKO ZINAONESHA HUJAWAHI KUTOKA NJE YA NCHI, HUNA UNALOLIFAHAMU, WE NI WAKUPUUZA TU, HUJUI ULITENDALO
 
Ipende nchi yako ndugu yangu.... mwanzo mgumu .
 
Shalom,

Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.

Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya ujerumani. Pia ili kukidhi haja ya moyo wangu nimetembelea karibu miji yote mikubwa na midogo ya nchi ninayoishi. Pia nilibahatika kutembelea tel aviv na jerusalem nchini israel. Kwa ujumla matembezi yangu yameniwezesha kujionea landmarks muhimu karibu yote kwenye nchi nilizotembelea. Pia kwa kuwa, mbali na safari ya London, Oslo na nchini Israel ambapo nilipanda ndege miji yote iliyobaki nilisafiri kwa bus ambapo nilipata furasa ya kuiona ulaya kwa undani zaidi hasa highways. Kwa ufupi ulaya imeunganishwa na barabara nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu kabisa. Kuna raha yake kusafiri nchi za Ulaya kwa kutumia barabara.

Baada ya utangulizi sasa naeleza nilivyoiona tanzania baada ya kutua Dar es Salaam.

1. Kwa kuwa tulitua usiku, haikuwa ajabu sana kuiona Dar es Salaam.mfano wa nyota za angani ambazo huwa hazina mpangilio maalum maana naijua vema na hata kabla sijaondoka kwenda ng'ambo nilitua na kupaa mara kadhaa kwa safari za ndani, nilijua Dar es Salaam. ina mipango miji mibovu inayofanya nyumba kujengwa bila mpangilio na hivyo usiku kuonesha taa zilizozagaa kama nyota angani. Tofauti kabisa na unavyoshuka usiku kwenye miji mingine duniani ambapo utaona namna barabara za mitaa na highways zilivyopangwa, na hata taa za mji kuwa kwenye mpangilio maalum. Tofauti na nilivyouacha uwanja wa ndege. Walau mara hii terminal 3 kwa mbali sana nilikiri inaondoa aibu tuliyokuwa nayo, lakini hata hivyo niliona kama bado ni ndogo sana.

2. Baada ya kutua na kuvuka security control nilitoka nje na kukutana na dereva wa "hotel' niliyofanya booking kwa njia ya simu baada ya kuiona kwenye booking.Com, haiko mbali sana na airport, nikili wazi njia nzima kuelekea hotelini, nikiwa na picha ya miji ya ulaya kichwani, niliona mji kuwa ni masikini na mchafu kupindukia. Hotel yenyewe niliyolipia laki moja ambayo kiukweli ni hela ndogo sana kwa euro niliikuta ni ya hovyo, chumbani nilikuta kuna neti ya mbu hiki nacho kilinistua maana Ulaya sikuwahi kulala na neti, pia nilikuta chumba kimepuliziwa dawa ya mbu. Palinishinda ilibidi nitafute sehemu nyingine ya kulala.

3. Kesho yake asubuhi nilisafiri kuelekea Mwanza. Baada ya kutua nilendelea kuona umasikini kama niliouona Dar es Salaam, nyumba za kimasikini zisizopangiliwa vema. Airport mtu anakubebea mzigo kwa vile vigari mpaka kwenye taxi, lakini baadaye anakuomba hela wakati haukukubaliana naye. Sintoongelea sana Mwanza.

4. Siku zangu zilivyokaribia za kurejea Ulaya, nilirudi Dar es Salaam. siku 2 kabla, lengo likiwa ni kuona mechi ya timu ya taifa. Nakumbuka kulipokucha na baada ya breakfast nilimwambia dereva taxi anizungushe dsm niione kwa ukaribu, hasa miundombinu inayoongelewa sana kwamba imeifanya Dar es Salaam kuwa kama Ulaya. Lengo lilikuwa baada ya kuzunguka mimi na dereva taxi tukaone mechi. Nilikubali kumlipa kwa ujumla. Nilimtaka anipeleke tff maana kulikuwa na dada mmoja nilitaka kukutana naye ili aniuzie jezi za timu ya taifa, Daraja la Mfugale, daraja Ubungo, kisha twende Mlimani City kwa ajili ya chakula, kisha daraja la Selandar, baadaye twende Kigamboni kupitia Daraja la Nyerere.

  • Daraja la Mfugale - sina mengi ila niliona ni kama kituta fulani tu kilichojaa umasikini - hakuna la maana la kupiga kelele nyingi
  • TFF - licha ya hela zote wazipatazo nilisikitika kuikuta kama nilivyoiacha, inatia aibu
  • Daraja la kijazi - hakuna kitu, kampala tu mbali na kuihusisha nairobi tunatia aibu kwa kelele tuzipigazo, maana wenzetu wa east africa wako mbali sana kwenye mambo ya flyovers
  • Mlimani City-licha ya kuwa napafahamu sana, niliona kuna ulazima wa kujenga malls kubwa zaidi kama ilivyo kwa nairobi na miji ya south africa
  • Daraja la baharini Selandar
  • Niliona kama tunajipiga wenyewe, kiukweli sikuona umuhimu wa lile daraja, maana kijiographia niliona kama limelazimishwa, nadhani linalenda kuwarahisishia mabalozi na watu wakubwa wakaao maeneo ya Mbezi Beach, Oysetrbay na kwingineko kufikia ofisi zao kiurahisi.
  • Maeneo yote ya Upanga na hata ikulu niliona ni pa hovyo sana, uchafu ni mwingi mno, pengine nimeathiriwa na kuishi miji ambayo eneo lote la mji limewekewa tiles.
  • Barabara ya Ali Hassan Mwinyi niliona kuna majengo yamechomoka kidogo yaliupendezesha mji, maana kiukweli Watanzania tuko obsessed obssessed sana na maghorofa pengine kuliko miundombinu muhimu ikiwamo maji taka na maji safi na umeme, hivyo kiurefu wa majengo tu, dsm inayazidi majiji yote niliyotembelea, labda kwa uimara yanaweza kuwa chini ya kiwango ila si haba.
  • Hatukubahatika kuliona daraja la nyerere maana muda wa mechi ulikuwa umefika.

Mwisho - siyo kwamba napachukia nyumbani lengo la uzi huu ni kutaka tubadilike na ikiwa tunataka maendeleo ya kweli ya miji yetu ni lazima tukubali kujifunza na kuona wenzetu wanafanyaje. Ili dsm yetu iwe na hadhi ya kidunia ni lazima (ukweli mchungu) kubomolewa upya, labda kuacha maeneo machache sana, na kujengwa upya (ni hasara lakini baada ya kujengwa upya faida yake ni kubwa sana)

Nawaomba viongozi wetu watembee, wajifunze jinsi miji inavyojengwa kuna faida kubwa sana kwa kufanya hivyo

Hamia huko Ulaya kama wajinga wenzio. Malabuku zako
 
Limbukeni akioneshwa mwezi hujidai yeye ndiye mwanzilishi wa kuona mwanga; ulichokielezea kinasadifu na laiti kama mzazi wako anakaa kijijini akisoma hiki alichokiandika hawezi kukuruhusu kurudi hata kuona kaburi lake ABADI.

Ni bora upotelee huko huko ulikolowea kuliko kubagaza taifa lako. Usiache mbachao kwa msala upitao. Huna mfano boara wa kuigwa na yeyote anayetafuta kutoka katika maisha yaliyojaa changamoto.

Wanaokutumia kwa kukulipa pesa ambazo hujui zimetokana na nini ndio waliokujaza kiburi ambacho kabla hujarejea ukimbizini utarejea kwenye jukwaa hili kuomba msamaha.
Tzn inanuka umaskini kwani uongo?
 
Aiseee juzi nilipita maeneo ya Mbagala pale karibu na kituo cha daladala cha Rangi tatu.. Daaah huku barabarani hii mitaro ina maji yametuama mpaka yamekuwa meusiiii na yanatoa harufu mbaya kwelikweli, alafu jirani tu kuna mama ntilie, kuna watu wanauza matunda na wengine sijui mitumba na chipsi yanii nilishangaa mno..

Dar ni chafu chafu chafu inanukaaa
Binafsi Dar siwezi kuishi mimi nina kinyaa Sana,hata ukijidai kuishi kwenye maeneo ya nafuu lakini lazima utapita sehemu zinazonuka

Kana kwamba haitoshi ikinyesha tuu ni vurumai Mji mzima,joto na kunuka
 
Usitetee ujinga mkuu, Dar ni chafu na inatia kinyaa.. Mara nyingine bora hata tunaoishi mikoani.

Dar ni takataka na washamba tu mmejazana huko..
Huwa nasema mara nyingi huo mji siwezi kuishi mimi ,unakuta unanunua matunda fresh afu sehemu inanuka

Pia kila sehemu ni machinga no order,mvua ikinyesha sasa ni balaa,usafiri wa umma ni majanga yaani kila kitu tabu
 
Labda kwa sababu ya ugeni tu ungekuwa unajua ungesafiri moja kwa moja mpaka Chato International Airport hakuna tofauti na ule wa Dubai baada ya hapo ungeingia mji kama Ulaya ungejikuta uko nyumbani kabisa tofauti wenyeji ni Wasukuma. Siku nyingine ukija toka utokako nenda moja kwa moja mpaka Chato International Airport baada ya hapo ukatalii Burigi National Park, utapata mengi ya kusimulia ukirudi kwenu.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Ndugu unasifia miji ya Ulaya iliyojengwa na wanaume wenzako? Rudi bongo ushiriki kujenga nchi yako.

Ni kweli miji ya Tanzania haikupangwa vizuri, nyumba zake si za kisasa, na kadhalika na kadhalika. Lakini ndio hivyo tulikotoka ni mbali na bado tunasonga mbele kivyetu vyetu. Siku hizi tunae kiongozi anaetufundisha kwa mfano wake mwenyewe kupitia kutosafiri nchi yoyote ya Ulaya: kwamba penda vya kwenu, sifia vya kwenu, acha kusifia vya wanaume wenzako.
Bora tulikotoka tunakoenda ni hovyo kabisa ukichanganya na kasi ya kuzaana na siasa uchwara za Jiwe ndio kabisaa tunaenda gizani
 
Una miaka 4 tu Ulaya unasahau neti? Niko miaka 20 na nathamini kwetu Bongo. Kila sehemu inao uzuri na ubaya wake hata hiyo Colon yako.
Jamaa limbukeni flan,angeona wamarekani weusi wanavyokuja kwa bongo angejiona mjinga sana
 
Havi kweli unafananisha majiji kama london, Berlin, tel Aviv, dotmund etc na mwanza na DSM!!!??
Majiji baadhi ya hayo yana miaka 50-200yrs, pia uchumi wa hayo majiji na yetu kweli lakini unafikia kufananisha london na dsm.
Nimelia sana niseme tu tz ndo kwenu na utarudi mfu au uzikwe huko kama mbwa. Kenge wewe
 
Shalom,

Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.

Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya ujerumani. Pia ili kukidhi haja ya moyo wangu nimetembelea karibu miji yote mikubwa na midogo ya nchi ninayoishi. Pia nilibahatika kutembelea tel aviv na jerusalem nchini israel. Kwa ujumla matembezi yangu yameniwezesha kujionea landmarks muhimu karibu yote kwenye nchi nilizotembelea. Pia kwa kuwa, mbali na safari ya London, Oslo na nchini Israel ambapo nilipanda ndege miji yote iliyobaki nilisafiri kwa bus ambapo nilipata furasa ya kuiona ulaya kwa undani zaidi hasa highways. Kwa ufupi ulaya imeunganishwa na barabara nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu kabisa. Kuna raha yake kusafiri nchi za Ulaya kwa kutumia barabara.

Baada ya utangulizi sasa naeleza nilivyoiona tanzania baada ya kutua Dar es Salaam.

1. Kwa kuwa tulitua usiku, haikuwa ajabu sana kuiona Dar es Salaam.mfano wa nyota za angani ambazo huwa hazina mpangilio maalum maana naijua vema na hata kabla sijaondoka kwenda ng'ambo nilitua na kupaa mara kadhaa kwa safari za ndani, nilijua Dar es Salaam. ina mipango miji mibovu inayofanya nyumba kujengwa bila mpangilio na hivyo usiku kuonesha taa zilizozagaa kama nyota angani. Tofauti kabisa na unavyoshuka usiku kwenye miji mingine duniani ambapo utaona namna barabara za mitaa na highways zilivyopangwa, na hata taa za mji kuwa kwenye mpangilio maalum. Tofauti na nilivyouacha uwanja wa ndege. Walau mara hii terminal 3 kwa mbali sana nilikiri inaondoa aibu tuliyokuwa nayo, lakini hata hivyo niliona kama bado ni ndogo sana.

2. Baada ya kutua na kuvuka security control nilitoka nje na kukutana na dereva wa "hotel' niliyofanya booking kwa njia ya simu baada ya kuiona kwenye booking.Com, haiko mbali sana na airport, nikili wazi njia nzima kuelekea hotelini, nikiwa na picha ya miji ya ulaya kichwani, niliona mji kuwa ni masikini na mchafu kupindukia. Hotel yenyewe niliyolipia laki moja ambayo kiukweli ni hela ndogo sana kwa euro niliikuta ni ya hovyo, chumbani nilikuta kuna neti ya mbu hiki nacho kilinistua maana Ulaya sikuwahi kulala na neti, pia nilikuta chumba kimepuliziwa dawa ya mbu. Palinishinda ilibidi nitafute sehemu nyingine ya kulala.

3. Kesho yake asubuhi nilisafiri kuelekea Mwanza. Baada ya kutua nilendelea kuona umasikini kama niliouona Dar es Salaam, nyumba za kimasikini zisizopangiliwa vema. Airport mtu anakubebea mzigo kwa vile vigari mpaka kwenye taxi, lakini baadaye anakuomba hela wakati haukukubaliana naye. Sintoongelea sana Mwanza.

4. Siku zangu zilivyokaribia za kurejea Ulaya, nilirudi Dar es Salaam. siku 2 kabla, lengo likiwa ni kuona mechi ya timu ya taifa. Nakumbuka kulipokucha na baada ya breakfast nilimwambia dereva taxi anizungushe dsm niione kwa ukaribu, hasa miundombinu inayoongelewa sana kwamba imeifanya Dar es Salaam kuwa kama Ulaya. Lengo lilikuwa baada ya kuzunguka mimi na dereva taxi tukaone mechi. Nilikubali kumlipa kwa ujumla. Nilimtaka anipeleke tff maana kulikuwa na dada mmoja nilitaka kukutana naye ili aniuzie jezi za timu ya taifa, Daraja la Mfugale, daraja Ubungo, kisha twende Mlimani City kwa ajili ya chakula, kisha daraja la Selandar, baadaye twende Kigamboni kupitia Daraja la Nyerere.

  • Daraja la Mfugale - sina mengi ila niliona ni kama kituta fulani tu kilichojaa umasikini - hakuna la maana la kupiga kelele nyingi
  • TFF - licha ya hela zote wazipatazo nilisikitika kuikuta kama nilivyoiacha, inatia aibu
  • Daraja la kijazi - hakuna kitu, kampala tu mbali na kuihusisha nairobi tunatia aibu kwa kelele tuzipigazo, maana wenzetu wa east africa wako mbali sana kwenye mambo ya flyovers
  • Mlimani City-licha ya kuwa napafahamu sana, niliona kuna ulazima wa kujenga malls kubwa zaidi kama ilivyo kwa nairobi na miji ya south africa
  • Daraja la baharini Selandar
  • Niliona kama tunajipiga wenyewe, kiukweli sikuona umuhimu wa lile daraja, maana kijiographia niliona kama limelazimishwa, nadhani linalenda kuwarahisishia mabalozi na watu wakubwa wakaao maeneo ya Mbezi Beach, Oysetrbay na kwingineko kufikia ofisi zao kiurahisi.
  • Maeneo yote ya Upanga na hata ikulu niliona ni pa hovyo sana, uchafu ni mwingi mno, pengine nimeathiriwa na kuishi miji ambayo eneo lote la mji limewekewa tiles.
  • Barabara ya Ali Hassan Mwinyi niliona kuna majengo yamechomoka kidogo yaliupendezesha mji, maana kiukweli Watanzania tuko obsessed obssessed sana na maghorofa pengine kuliko miundombinu muhimu ikiwamo maji taka na maji safi na umeme, hivyo kiurefu wa majengo tu, dsm inayazidi majiji yote niliyotembelea, labda kwa uimara yanaweza kuwa chini ya kiwango ila si haba.
  • Hatukubahatika kuliona daraja la nyerere maana muda wa mechi ulikuwa umefika.

Mwisho - siyo kwamba napachukia nyumbani lengo la uzi huu ni kutaka tubadilike na ikiwa tunataka maendeleo ya kweli ya miji yetu ni lazima tukubali kujifunza na kuona wenzetu wanafanyaje. Ili dsm yetu iwe na hadhi ya kidunia ni lazima (ukweli mchungu) kubomolewa upya, labda kuacha maeneo machache sana, na kujengwa upya (ni hasara lakini baada ya kujengwa upya faida yake ni kubwa sana)

Nawaomba viongozi wetu watembee, wajifunze jinsi miji inavyojengwa kuna faida kubwa sana kwa kufanya hivyo
Mkubavu mkubwa wewe.......ulizaliwa kwenye ward kama ya kulishia ng'ombe unajifanya unaijua ulaya kuliko kijijini kwenu........wewe Acha ushamba uko ulaya watu walianza kwenda toka MTU anatumia passport moja yeye na familia nzima na bado wakarudi kufia bongo bila kutoa kashfa kuenda kidogo Tu kuuza ngada unajifanya kunanuka muulize aliye kuzaa kama kuna nuka hapa bongo............si alipanua mpaka ukapaona hapa duniani Acha kudharau kwenu mkubavu umenikera ............😬😬😬😬😬😬 Nisamehee lakini kama nimekukwaza
 
Back
Top Bottom