Niliwahi kuelezea nguvu ya Kanisa Katoliki katika Siasa za Tanzania nikadhihakiwa, sasa taratibu nadhani tutaelewana tu!

Niliwahi kuelezea nguvu ya Kanisa Katoliki katika Siasa za Tanzania nikadhihakiwa, sasa taratibu nadhani tutaelewana tu!

Kwa hiyo mama ni mkatoliki...hivi shule hazijafunguliwa bado?
 
Nayaheshimu sana na mno Madhehebu mengine yote ukiachilia langu la Katoliki, ila kwa Tanzania hii na Nguvu ya Kanisa Katoliki tokea Uhuru na lilivyojikita indirectly katika Siasa za Tanzania huwezi kuwa Rais wa Tanzania au Makamu kama siyo Mkatoliki. Ukilibishia hili unataka tu Ligi isiyokuwa na maana kwani ndiyo Ukweli wenyewe.
Nimesoma mistari hii michache tu, ikatosha kunipa ukweli kwamba wewe na kanisa katoliki ni vitu mbalimbali kabisa, na wala husogelei kamwe kuwa mmoja miongoni mwao.

Pili, wewe ni mwongo na huoni hata aibu kusema uongo ulio wazi, kana kwamba unaowaandikia wakusome ni vilaza kama ulivyo wewe!

Napata shida kuendelea kusoma mengine uliyoandika huko chini, baada ya kusoma upuuzi ulioweka hapa.
 
Je, kanisa katoliki lina nguvu na kuwa na influence kwenye tawala mbalimbali, jibu ni ndio...

Je, kanisa katoliki ndilo linalotoa hatma ya uongozi wa juu kwa nchi yetu, hapa mleta mada yakupasa uweke nyama zaidi
 
Catholic hawana nguvu yoyote ndio maana Ulaya imetapakaa kwenye vinchi masikini vya Eastern Europe,Africa na Latinos....nchi zote zenye nguvu Ulaya sio Catholics
Wacha uongo..
Hebu google hizi nchi Kesha rudi hapa... Italy,Spain,Poland,Portugal,Germany,..hizi ni kwa uchache.....Unechanganyikiwa ehhh...au umeamua kujitoa Ufahamu..
 
Mkuu unafahamu, Katoliki kwa utaratibu wao Askofu ni mkuu wa eneo husika

Pengo alikuwa anashambulia mamlaka ya Dar es Salaam ambalo ndio eneo Lake la utawala

Kumbuka Mamlaka ya Dar es Salaam
ndio kuna Ikulu
Askofu wa Songea anatawala Songea hivyo anashambulia mamlaka zake za jimbo Songea


Usiwachukulie Poa hao watu, Ukisikia alienda Vatican kusomea the sheria za kanisa usifikirie sheria za Africa

Kuna siri nzito sana
Kutishana tishana ni uhuni wa kishamba
 
Ni kweli nimelisikia kitambo hili lakini ..hata Congo DRC Kanisa Katoliki lina nguvu sana kupanga safu za viongozi wake
Thubutu, huko kongo kanisa kila siku linabishana na serikali
 
Nilivyoifungua uzi wako nilisoma hadi mwisho nikifikiri labda kuna jambo umelilenga. Kumbe ni upupu wanzo mwisho.
 
Wacha uongo..
Hebu google hizi nchi Kesha rudi hapa... Italy,Spain,Poland,Portugal,Germany,..hizi ni kwa uchache.....Unechanganyikiwa ehhh...au umeamua kujitoa Ufahamu..

Ukweli ni kwamba ukatoliki huko dunia ya kwanza hauna ushawishi tena na asilimia kubwa ya ulaya ya magharibi na marekani ukatoliki ulishafifia Ndio maana Leo ulaya ushoga, kutoa mimba na mambo mengi ambayo ni kinyume cha ukatoliki ndivyo vimetamalaki ulaya.

Hata upande wa fedha kwa sasa kanisa limeyumba mno kiasi cha waamini kuanza changishana michango isiyokwisha.
 
Papa Pius alijaribu kushindana na Napoleon Bonaparte, lakini jamaa likaenda hadi Vatican na kumteka Papa kisha kutangaza kwamba Kanisa Katoliki halitamiliki ardhi tena wala kuingilia siasa za nchi. Ardhi walikuja rudishiwa mwaka 1929 na Benito Mussolini kwenye Mkataba wa Lateran. Huyu Papa Pius baada ya yale mateso alifia uhamishoni na wala Kanisa Katoliki halikufanya chochote wala Lolote.

Kuna siku Napoleon Bonaparte alimuambia Kadinali Ercole Consalvi hivi "Your eminence do you know I have the Power to destroy the Church ???" kwa kiburi na madaha Kadinali Ercole Consalvi akamjibu Napoleon Bonaparte hivi " You will not succeed your majesty. Not even we priests, bishops and cardinals have been able to do that". Kanisa lilikosea sana, Napoleon aliwavuruga na kama siyo Mungu kutaka, basi baada ya 1814 Kanisa lisingekuwepo kabisa.

Hilihilo Kanisa la Katoliki lenye nguvu, lilishindwa kupambana na wakina Robespierre na The Jacobins Club hadi kupelekea mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789. Kwenye yale mapinduzi ya Ufaransa The Jacobins waliua mapadri 30,000 ndani ya siku moja aidha kwa kukata vichwa (Guillotine) au kupigwa risasi kichwani.

Mwaka 1861-1864 Papa na Vatican walimwambia Jeff Davis (Mkatoliki) kwamba akianzisha vita dhidi ya Marekani Kaskazini basi Papa atayaambia mataifa ya Kikatoliki ya Marekani Kusini yamuunge mkono. Vatican ndiyo lilikuwa taifa la kwanza kuitambua The Confederacy kama nchi wakati inapigana vita dhidi ya The Union. The Jesuits walishindwa vibaya sana na Lincoln akainuka kidedea, mwishowe wakamtuma John Wilkes Booth (A Devout Catholic) kumpiga risasi Lincoln. Kichekesho ni kwamba baada ya kumuua Lincoln, bwana Booth alikutwa yuko Vatican kama moja ya walinzi wa Papa. Ulysses Grant akaomba jamaa arejeshwe Marekani, lakini jamaa akakimbilia Uingereza.

Kichekesho kikubwa zaidi ni pale ambapo Papa na genge lake la Jesuits walibagazwa na kudhalilishwa na mwanamke hodari kabisa, Elizabeth I. Mwaka 1588 Kanisa Katoliki liliwatuma wahispania na meli zaidi ya 130 (The Spanish Armada) ili walivamie dola la Uingereza ambalo lilikuwa limeukana Ukatoliki na kugeuka dola la Kiprotestanti. Meli zote zile na maelfu ya wanajeshi kutoka Ulaya, walishindwa kuivamia Uingereza na mpaka leo dola lile ni la Kianglikani. Baada ya vita Waingereza walitunga wimbo wa Kilatini usemao Flavit Jehovah et dissipat sunt (Jehovah blew his winds, and they were scattered). Baada ya kushindwa vita na mwanamke Kanisa Katoliki likaamua kuiadhibu Uingereza kibiashara na vikwazo, lakini dola la Kituruki chini ya Sultani Murad III waliiokoa Uingereza isiangamie.

Kichekesho cha mwisho Kabisa ni jinsi ambavyo The Jesuit Order ilishindwa kuzuia mwanafunzi wao mpendwa mwenye akili kabisa Adam Weishaupt kutengeneza The Bavararian Order of the Illuminati mwaka 1776, chombo ambacho kilitumika kupambana na Kanisa Katoliki hadi kupelekea mapinduzi makubwa yaliyoleta mabadiliko makubwa kisayansi na kifikra barani Ulaya hadi kupelekea kanisa Katoliki kubomolewa vipande vipande na Vatican kuvamiwa.

Mnamo karne ya 13, Mongke Khan na jeshi la Mongolia walijipanga kuvamia Ulaya Magharibi, hadi wafike Vatican lakini Mungu hakupenda na Mongke akafa wakati jeshi linaenda Ulaya. Lakini Kanisa Katoliki lilikuwa linauogopa sana utawala wa Mongolia hadi kufikia hatua kumtukana Qublai Khan kama The Spawn of Satan. Alivyoona hali inazidi kuwa mbaya Papa akaanza kutuma zawadi Mongolia ili kumshawishi Qublai ashirikiane naye hasa kuruhusu Ulaya itumie The Great Silk Road.

Nafahamu na nakubali kwamba Kanisa Katoliki lina ushawishi mkubwa sana duniani, lakini kuna sehemu huwa linakanyaga kwa utaratibu. Hizo nguvu ambazo mnataka kuwapa nadhani nyingine mnazidisha na pengine mnakuwa na mawazo sana yasiyo na kichwa wala miguu. Hapa Tanganyika wakati wa Ukoloni kuna baadhi ya Mapadri wa Kizungu ambao walimshawishi Chief Edward wa Wamassai adai uhuru wa Wamassai peke yake nje ya Tanganyika lakini, hola, akashindwa.

Mwisho kabisa, Kanisa Katoliki lilipotawala Ulaya kuanzia karne ya 5, kipindi hiki kiliitwa KIPINDI CHA GIZA (THE DARK AGES), ambako Ulaya ambayo ilitawala dunia kwa uvumbuzi, sanaa, majeshi na utaalamu mbalimbali ilioza na kupoteza mwelekeo. Watu hawakuruhusiwa kusoma wala kufikiri (lilikuwa ni kosa kufikiri kama mtu huru). Walificha na Biblia na kusema kwamba mwenye mamlaka ya kutafasiri Biblia ni Papa (The Pontifex Maximus a.k.a The Pontiff) ambaye ndiye alikuwa ni mjumbe wa Mungu duniani (The Vicar of Christ). Baada ya Kanisa Katoliki kupoteza nguvu Ulaya baada ya kuzaliwa Uprotestanti, Vita ya Miaka Thelathini (thirty years war) na kutokea mapinduzi ya kisiasa Ulaya ndiyo kikaanza kipindi cha The Enlightenment ambacho kilizaa dunia ya leo ambayo tunaishi.

Kikubwa kinachonichekesha juu ya hizi siasa za Waprotestanti na Wakatoliki, ni kiwango cha Ujinga kilichopo kichwani kwao. Mtu anakaa kabisa anaanzisha uzi akisifia dini ambayo Mzungu Kaisari Constantine, Martin Luther au Ellen G, White walianzisha (Upuuzi, puuzi tu wa mwafrika): Wengine wasiokuwa na akili pia kama yeye wanakuja kumuunga mkono kutetea hii nadharia ya kijinga ambayo kama ina ukweli wowote ule basi Taifa hili haliwezi kuendelea na kuwa taifa la watu huru. Maana watu wanakaaa kabisa wanafurahia nchi yao kuongozwa tokea The Vatican.

Pik Botha aliposema mwafrika hana akili wala hana tofauti na mnyama, nikiangalia huu uzi na wachangiaji wengi nadhani kuna sehemu alipatia. Mwafrika hata umpe bunduki ataanza kuua mwenzake na wala siyo mzungu (Huu uzi ni ushahidi tosha).......


WALE RELIGIOUS ZEALOTS AND ENEMY OF REASON & COMMON SENSE POVU RUKSA !!!!!!!!!
 
Wakati wa kikwete, makamu alikua dr shein, waziri mkuu lowasa..
hakuna mkatoliki hapo..
acha upupu ww
 
Umepuyanga sana mzee, hivi wakati unaandika huu upupu hukushtuka tu kuwa Kikwete na Dr. Bilali sio Wakatoliki? Na walikuwa katika nafasi ulizotaja ya kuwa mmoja wapi ni lazima awe Mkatoliki?

Umekula maharage ya wapi mkuu mpaka umevimbiwa? Malizia pilau kwa shemeji yako ulale!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app

Hiyo ilikuwa ni Dharula tu iliyomgharimu vilivyo JK katika Utawala wake kwa Mambo ambayo siyo kwa Faida yako Wewe Juha Mwandamizi.

Wafuatiliaji wa 'Masuala' wamenielewa.
 
Back
Top Bottom