Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Katiba mpya ndiyo msingi wa taifa letu.

Lazima tufanye review ya mfumo wetu wa elimu.Tz tuna vyuo vingi vya ufundi na hivi vyuo vya maendeleo ya wananchi ambavyo vinaweza kutumika moja kwa moja kuibua na kuendeleza ubunifu, badala ya kung'ang'ania kila kijana aende sekondari. Tuwe na mfumo unaowafanya Vijana kujiajiri ktk sekta ya ufundi na ubunifu.Ambayo ndiyo chachu ya maendeleo ya viwanda vidogo na vya kati.

Ndiyo maana mataifa ya magharibi wanakupa msaada wa kifedha lkn hawawezi kukupa msaada wa kiufundi(technical know how) kwa sababu wanajua utajikomboa.Leo Tanzania ukitengeneza gobore una itwa mhalifu.
 
Umeongea ukweli,hii nchi imejaa watu dizaini ya mtoto wa kambo au yatima kulia Lia tuu na hakuna suluhu huku wakiwaza misaada ya serikali.

Mbaya zaidi kuna watu maskini wengi na wajinga si wanaojiita wasomi au hata wasio soma.

Mama fungua nchi tutoke tupate exposure na tukanyonye wengine nao waje kwetu ,maisha ya kujifunga funga ni kuwa maskini wa milele.

Pili pesa zielekezwe kwenye mambo yenye tija hii habari ya kufurahisha washabiki wajinga wa mwendazake ni wehu,hakuna haja ya kutekeleza miradi ya ma sgr na mingine ya dizaini hiyo kwa pupa
 
Rasilimali si utajiri, rasilimali zitakuwa utajiri baada ya kuweza kuzivuna kwa manufaa na kuzigeuza kuwa utajiri.Kitu ambacho Tanzania imeshindwa.Jpm alikuwa sehemu ya mfumo ulioshindwa kazi ya kuzivuna rasilimali zetu kwa faida ya taifa hili.

JPM alikuwa anacheza na akili za watanzani wajinga kwa kuwafanya wajione ni wanyonge na hivyo kila alichokuwa anafanya ni hisani na si wajibu wa kiongozi. Wakati anafanya haya yeye na genge lake waliendelea kujineemesha na rasilimali za NCHI huku wakiwatupia hao wanyonge mfupa usiokuwa na mnofu.
 
Mara zote nasema rasilimali ya nchi yoyote ni watu wake. Hata wazee wa zamani waliamini msingi wa maendeleo ni watu. Hapa kwetu huwa nashangaa viongozi wetu wakisema hii nchi tajiri wanataja madini n.k lakini hawataji watu.

Ni kwa sababu tumeamua kutelekeza watu sasa maendeleo yataletwa na nani.

Kwa mfano hata sera zetu za kuvutia wawekezaji zinatakiwa zielekezwe maeneo ambao watu wetu hawawezi kuwekeza.

Ni lazima tuwe na mkakati wa kuiba ujuzi toka nchi mbalimbali. Usalama wetu wa taifa badala ya kujikita kwenye ujasusi wa kiuchumi wao wanakimbizana na upinzani. Busy kila siku na kutumia rasimali kudhibiti wapinzani.

Kuna baadhi ya mbinu ambazo tunaweza kuzitumia kama.

1. Kutoa nafasi za uraia kwa raia wa nje wenye ujuzi (strategically)
2. Kutoa scholarship za vijana makininkwenda kusoma na kufanya kazi nje ya nchi kimkakati.
3. Kusaidia watu wetu walioko nje kufanya kazi katika strategic companies na hatimaye kurudi.
4. Kuwezesha watu kuingia ubia na wageni wanaowekeza hapa nchini.
5. Kuhakikisha tunajitosheleza kwa chakula na kuzalisha kwa gharama nafuu na ziada ambayo inaweza kuuzwa nje.
 
Kuna ndugu yangu aliwahi kupoteza mtoto katika foleni ya ubungo wakati akiwa anampeleka hospitali. Jamaa ana pesa nzuri tu (maendeleo ya watu) lakini miundombinu mibovu (maendeleo ya vitu) ilifanya apoteze mtoto.
Hiyo miundombinu ya kujengwa lazima iangaliwe sio ma sgr sijui mastendi na miradi ya kijinga kama hiyo.Nchi za wenzetu kama Ghana wanajenga barabara za uhakika Ili kuondoa hayo matatizo sio kukurupuka na kusema tumenunua ndege kwa cash.

Kwa nini ndege za cash hazikumsaidia huyo ndugu yako?
 
Mimi nakuunga mkono ndugu mleta mada, bahati nzuri rais ana watu wengi anaofanya nao kazi katika uongozi, matumaini yangu mada hii wataiona na watamuwasilishia yaliyomo, ikimpendeza atekeleze Lau apotezee maadam maisha yanaenda.
 
Angekuwa hawapendi wazungu, angewafukuza mabalozi basi mkuu. JPM alikuwa anataka fair play kati ya Tanzania na nchi zingine.
Fair play kwa kumtukana mtu anayesapoti bajeti yako kwa karibia nusu.Fair play wakat diplomasia umetia kapuni.Umejitenga na dunia umejifungia kwako ukiwakamua raia wako kile kidogo Tena wakati mwingine kwa kuwapora mchana kweupe.
 
Rais ndiye kiongozi mkuu wa taifa
Tofautisha taifa na kiongozi,Tz itakuwepo milele lkn viongozi wanapita.Tuipiganie Tz na si kiongozi.Na mawazo yako haya ndiyo yataliumiza taifa hili kwa muda mrefu,badala ya kujenga misingi ya kiungozi km taasisi tunapambana kumjenga mtu ambae leo yupo kesho hayupo.Ujinga!!

Uzalendo ni kuyapigania maslahi ya nchi na si maslahi ya kiongozi.
 
Mwanangu umenikosha Sana , hii nchi ya jabu Sana , kwanini haijaruhusu malipo ya PayPal till now? Visa ni ngumu Sana kwenye hii nchi , Ila wakenya hawana hzo mambo wanatoboka kirahsi Sana , na nje ndo kuna hela Yani ili upate hela lazima jirani umnyonye, umpore au akulipe, ndo mana tunashangaa Leo majamaa kuwekeza hapa nchini Zaid ya makampuni 500 why ? Mitaji wanayo na akili wanayo wameitoa wapi ? Nchi Yao ipo connected na dunia ....

Maghufuli alikuwa anaididimiza sana hii nchi kwenye masuala ya uchumi ....

Mama Samia hawezi kufanya lolote la maana , kete yake ya mwisho ni kuruhusu kusukwa katiba mpya ......Kwa katiba hii hataweza lolote Sana Sana tutakuja kumlaumu , miaka miwili ni mingi Sana atakuwa tayar exhausted... Kama ana sikio la uelewa aruhusu mchakato wa katiba mpya quickly as possible before haijawa toolate .....
Pili mikodi mingi,mikubwa na ya kinyonyaji haiwezi kusogeza nchi mbele.

Ningekuwa kwenye nafasi ya kushauri mambo ya uchumi basi ningeshauri kupunguzwa kwa kodi hasa VAT na kufuta ushuru za kijinga mfano vitambulisho vya machinga na tozo za kwenye madini ya ujenzi kwa uchache tuu.

Ningewekeza zaidi kwenye miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege strategic huku Nikiviwekea miundombinu stahiki.

Ningeipa nguvu sekta binafsi yaani kiufupi ningejenga demand side Ili ichochechee production na kwa njia hiyo ndani ya miaka 2 ningeanza kupata pesa nyingi kwa njia ya kodi
 
Tofautisha taifa na kiongozi,Tz itakuwepo milele lkn viongozi wanapita.Tuipiganie Tz na si kiongozi.Na mawazo yako haya ndiyo yataliumiza taifa hili kwa muda mrefu,badala ya kujenga misingi ya kiungozi km taasisi tunapambana kumjenga mtu ambae leo yupo kesho hayupo.Ujinga!!

Uzalendo ni kuyapigania maslahi ya nchi na si maslahi ya kiongozi.
Huko Marekani sera za Bush Jr. na Obama zilikuwa zinafanana?
 
Angekuwa hawapendi wazungu, angewafukuza mabalozi basi mkuu. JPM alikuwa anataka fair play kati ya Tanzania na nchi zingine.
Huyu jamaa usimsikilize mkuu infantry. Huyu jamaa ni very manupulative in a wrong way. Ni kama anajaribu ku misguide watu.
Anataka kutuaminisha hata ukoloni wa mzungu ulikua sawa tu. Afu intelligence haipimwi kwa kua mpole tu. Kuna njia nyingi za kupima intelligence. Cha msingi ni output. Jpm at the end of the day ametoa positive output na ameleta positive impact na amewaachia watu spirit. Kitendo cha huyu jamaa kuna ku misguide watu na kuwaambia mtu mwenye akili anatakiwa aweje ni kupotosha au kuendelea kushikilia agenda za watu unknown.
Mtu anaweza kua mbabe na bado akawa na akili vilevile kwenye huo ubabe.
 
Sawa hakuwa malaika, lakini unapokuwa kiongozi wa nchi(raisi) huwezi kuropoka hovyo hovyo kwa kisingizio eti siyo malaika ana upungufu kama binadamu wengine. Kiongozi lazima ajiheshimu. "Baki na mavi yako nyumbani" hayo siyo maneno ya kusemwa na raisi wa nchi hadharani tena kwenye umati wa watu.

Alikuwa mgonjwa sana watu walikuwa hawajui tu!! Ndio maana alikuwa anazungumzia kifo sana.
 
Back
Top Bottom