Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Hapa nakataa mkuu. Jpm alikua anataka fair business kati ya tanzania na nchi nyingine. Alitaka wananchi wawe na thamani sawa na foreigners. Na kutoa dhana ya cheap labour.
Fairness unapata wapi wakati haujui dynamics za uchumi na biashara?

Angalia Mwendazake alivyojitia kidole cha matako kwenye korosho halafu ndiyo unamuamini akuamulie masuala ya fair business!!

Global business siyo ubabe wa mdomoni, unakaa swekeni Chato hata duniani huwezi kufika halafu u-dictate business terms!! No it can't happen
 
Katiba mpya ndiyo msingi wa taifa letu.

Lazima tufanye review ya mfumo wetu wa elimu.Tz tuna vyuo vingi vya ufundi na hivi vyuo vya maendeleo ya wananchi ambavyo vinaweza kutumika moja kwa moja kuibua na kuendeleza ubunifu, badala ya kung'ang'ania kila kijana aende sekondari. Tuwe na mfumo unaowafanya Vijana kujiajiri ktk sekta ya ufundi na ubunifu.Ambayo ndiyo chachu ya maendeleo ya viwanda vidogo na vya kati.

Ndiyo maana mataifa ya magharibi wanakupa msaada wa kifedha lkn hawawezi kukupa msaada wa kiufundi(technical know how) kwa sababu wanajua utajikomboa.Leo Tanzania ukitengeneza gobore una itwa mhalifu.
Kwa Tanzania katiba sio tatizo,tatizo kubwa na watu bado ni wajinga pamoja na hii katuba mbovu mengi yamefanyika pasipo kuifata but sote tunaona ni sawa tumelala usingizi wa pono.
 
Hii Katiba ni tatizo kubwa sana na isipobadilishwa tatendelea kupuyunga tu.
Kwa Tanzania katiba sio tatizo,tatizo kubwa na watu bado ni wajinga pamoja na hii katuba mbovu mengi yamefanyika pasipo kuifata but sote tunaona ni sawa tumelala usingizi wa pono.
 
Huyu jamaa usimsikilize mkuu infantry. Huyu jamaa ni very manupulative in a wrong way. Ni kama anajaribu ku misguide watu.
Anataka kutuaminisha hata ukoloni wa mzungu ulikua sawa tu. Afu intelligence haipimwi kwa kua mpole tu. Kuna njia nyingi za kupima intelligence. Cha msingi ni output. Jpm at the end of the day ametoa positive output na ameleta positive impact na amewaachia watu spirit. Kitendo cha huyu jamaa kuna ku misguide watu na kuwaambia mtu mwenye akili anatakiwa aweje ni kupotosha au kuendelea kushikilia agenda za watu unknown.
Mtu anaweza kua mbabe na bado akawa na akili vilevile kwenye huo ubabe.
Not with Mwendazake, yeye katurudisha nyuma sana. I wish CCM wangemsimamisha Samia Suluhu kama Rais mwaka 2015 na Magufuli awe Waziri Mkuu tu. Leo tungekuwa tunapaa kiuchumi.

Mnaomsifia Magufuli mnasifia propaganda za kijinga alizoziimba 24/7 kwenye vyombo vya habari and it is unfortunate bado amewafanya mateka pamoja na kwamba ameshafukiwa Chato. Kwenye karne hii kuirudishia Serikali ifanye biashara kama wanavyofanya TBA kwenye ujenzi badala ya makandarasi, Au TPDF kufanya ujenzi, kendesha kumbi za harusi, maduka ya spear na ku clear magari ni wendawazimu

Unanyang'anya shughuli za private sector unaIepeleka Serikalini, it's CRAZY
 
Gaddafi na Kwame Nkurumah walikuwa madikteta na wote waliondolewa kwa aibu katika nchi zao.
Mkuu unweza funguka kidogo kuhusu sakata la mgogoro wa Libya ukizingatia maisha yao yalikuwa mazuri sana(tetesi)
 
NILIWAHI KUMWAMBIA HAYATTI MAGUFULI, LEO NARUDIA KWA RAIS SAMIA, ILI ASIJEPOTEZA MUDA WAKE.

Na, Robert Heriel

Niliwahi kuandika hapa miaka mitatu iliyopita, niliipa makala ile kichwa kisemacho "Rais Magufuli unapoteza muda wako tuu" katika makala ile watu wengi walinitukana, wengine walinitishia, sikuwalaumu kwani niliwaelewa lakini wao hawakuwahi kunielewa.

Leo hii narudia baadhi ya maneno yaleyale niliyoyasema siku zile.

Niliandika Magufuli anapoteza muda wake nikiwa na hoja zifuatazo;

1. Magufuli nilimuona anapoteza muda kwa sababu alikuwa na mtazamo kuwa, nchi ni tajiri na itapata maendeleo kwa sababu ina Rasilimali nyingi akizitaja kama madini, mbuga, ardhi kubwa yenye Rutuba, maziwa na mito yenye viumbe maji kama samaki, vivutio vya utaliii, bahari, kuzungukwa na mataifa mengi yasiyo na bahari, n.k.
Niliona anapoteza muda kwa sababu, nchi haiendelei kwa wingi wa Rasilimali isipokuwa inaendelea kwa ya kuwa na WATU WENYE AKILI. Watu wenye akili ndio wanaleta maendeleo nchini sio uwepo wa Rasilimali nyingi.

2. Magufuli aliamini, nchi itajengwa kwa kuwanyonya wananchi wake pekee, ndio maana alishindwa kuongeza mishahara miaka yake yote aliyotawala, pia akashindwa kutoa ajira mpya.
Kama hiyo haitoshi, sio ajabu aliongeza vikodi vya hapa na pale ili kuendesha serikali yake, lakini bado mambo yalimuwia magumu hali iliyomfanya ajiingize katika hatari ya kugombana na wafanyabiashara, wengi wao aliwaita wahujumu uchumi, wapo walioisoma.

Mimi nilimwambia nchi yoyote iliyoendelea haijawahi kuendelea kwa kutegemea unyonyaji kwa watu wake pekee, bali ni lazima ivamie mataifa mengine. Nilitoa mifano kwa baadhi ya mataifa yaliyoendelea yaliyojipatia utajiri kwa kunyonya watu wake na mataifa mengine.. Biashara ya utumwa, Ukoloni, na ukoloni mamboleo vyoote vinaangukia hapa.

Taifa kama la Korea ya kusini loo, liliamua kualika mataifa mengine hasa Mataifa ya Magharibi kuja kuwekeza Korea kusini. Kwa sasa Korea ni moja ya nchi zilizopo ulimwengu wa pili.

3. Magufuli aliamini kuongoza nchi kibabe ndio suluhu ya maendeleo, wakati mbinu hiyo ilishapitwa na wakati, na kwa vyovyote lazima ingelala upande wake na angeshindwa, licha ya kujitutumua kuchelewesha muda wa anguko lake.

Mimi nilimwambia kuwa kizazi cha sasa kinaongozwa kwa akili, ujanja, maarifa na mambo yote yahusuyo akili. Ubabe ungeweza kutumika machungani kwenye mbuzi, ng'ombe, na kondoo ambao hawana utashi kama binadamu.

Hakuna uhusiano wa karibu baina ya Ubabe na biashara, hivyo kivyovyote vile anguko la kiuchumi lilikuwa ni uhakika. Kwani hakuna mfanyabiashara ambaye angependa aishi kwa hovyo wakati pesa ni zake mwenyewe.

4. Magufuli aliamini kuwakaripia wengine mbele ya halaiki na wengine kuwatukana ndio namna ya kuleta nidhamu ndani ya serikali yake.
Wakati nidhamu ndani ya serikali hutokana na jinsi sheria zinavyofuatwa na kutelekezwa. Kama mtu ni mwizi basi sheria ingechukua mkondo wake,

Masikini wengi na watu walioshindwa walifurahishwa na magufuli kwa sababu ni kawaida ya masikini kuona mwenye nacho akianguka.

5. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye matamko kuliko kuweka mfumo imara ili hata yeye akiondoka mambo yatajiendesha vyema.
Niliwahi mwambia kuwa One manshow ni kama mbio za sakafuni ambazo lazima ziishie ukingoni. Nilimwambia anapoteza muda wake.

Maendeleo ni mfumo kama mnyororo unaounganisha seti nyingi ya vitu.
Maendeleo ya nchi za Afrika niya kubahatisha kwa sababu hakuna mfumo unaoeleweka.

6. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye kujipa promo kwenye vyombo vya habari na kujisifu, na kuwazima wengine ili kuchota akili za watu wenye upeo mdogo na kuzuia wale waliokuwa wanampa challenge kwa mitazamo yao.
Hii pekee ingetosha kuonyesha kuwa anapoteza Muda wake.
Hakuwa mtu kama Anthony Mtaka ambaye hafanyi manipulation lakini matendo yake yanaonekana.

7. Magufuli alifanikiwa zaidi katika kutekeleza na kusimamia maendeleo ya miundombinu, kwa hili nampa heko, lakini nilimuambia kuwa taifa masikini linawekeza kwenye watu na sio vitu,
Hii watu walinipinga lakini huo ndio ukweli mchungu, masikini kuwekeza kwenye vitu zaidi ya watu ni kupoteza muda na kuwatesa watoto.

8. Magufuli alijitahidi kujifanya hawapendi Wazungu na kila mara alitoa maneno ya kupata ushawishi kwa watu ili wawachukie wazungu. Ndio maana hata Mambo ya Corona aliyaona kama mchezo wa kuigiza na njama za wazungu kutuangamiza.

Jambo ambalo hata mtoto mdogo akifikiri anaona ni uongo wa mchana.
Nilimuunga mkono kwenye suala la kutokuweka Lockdown, lakini masuala mengine nilimpinga.

Magufuli angepoteza muda kwa vyovyote kwa kupinga mambo ya wazungu ambayo hata huo Urais aliokuwa nao ni mfumo wa kizungu, masuala ya jeshi ni mifumo ya kizungu, jina lake lakizungu, dini yake yakizungu na hata alipokufa alizikwa kizungu, hata elimu yake ni yakizungu, hata magari na vifaa vyote alivyokuwa akivitumia ni vyawazungu, achilia mbali madawa na miwani aliyokuwa akivaa. Sijazungumzia silaha na wana usalama waliokuwa wanamlinda ambao ili wawe wa kimataifa inapaswa wapewe mafunzo ya kizungu.

Kama wazungu wangetaka kutuua wangetuua tangu miaka ya 1900 huko walipokuja kututawala. na hata wakiamua kutuua uwezo huo wanao, na hatuna uwezo wa kufurukuta.

Sasa mambo hayo hayo, nayasema kwa Rais Samia, kuwa aangalie asije akapoteza muda wake kwa kushindwa kuendana na wakati.

Maendeleo ya nchi ya USA sio lazima yawe maendeleo kwa Tanzania. Hiyo ni muhimu kuzingatiwa.

Hata hivyo Rais Samia lazima azingatie haya ili naye asijikute katika kucheza Nage na kupoteza muda wake.

1. Maendeleo ni kuwekeza kwenye watu
2. Kuwekeza kwenye watu ni kuwapa Uhuru
3. Uhuru wa watu ni pamoja na kuwapa nafasi ya kuyafurahia maisha yao kwa kutumia rasilimali za nchi yao au kuvamia mataifa mengine. Passport zitolewe watu wakahangaike huku na huko.
4. Serikali isifikiri kunyonya wananchi wake pekee(kodi na ushuru) bali pia ifikiri namna ya wananchi wake kuenda nchi zingine kunyonya mali na utajiri wa nchi zingine.

5. SHeria na utawala bora zisiachwe
6. Ubabe wa kipumbavu uachwe maana palipo na ubabe au udikteta lazima kuwa na uasi/usaliti na palipo na usaliti lazima pawe na mapinduzi.

7. Serikali isijikite kwenye matamko ya kipuuzi puuzi. Kwani kwa kufanya hivyo itaathiri vijana wengi ambao wao kila kitu watataka tamko la serikali.

Sishangai kwa nini watu wanamlaumu Mama kuwa kwa nini ni mpole, ni kutokana na kuathiriwa na matamko yasiyo na kichwa wala miguu.

Sio kila kitu kitolewe tamko kwa kutafuta sifa za kijinga kwenye Kamera ili ionekane kazi inafanyika wakati hakuna kitu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam
Unatisha mkuu..!! Safi sana!
 
Hakuwa na uwezo huo. Hata wazungu walijua he was just stupid with no impact.

Na kuthibitisha hilo, Tundu Lissu ( Mwanasiasa ambaye Magufuli alimchukia to the moon ) alihifadhiwa kwenye ubalozi wa Ujerumani na badaye wazungu wakamsindikiza kwenda Airport kupanda ndege mchana kweupeee huku akihitajika mahakamani.

Hao wazungu baada ya kumsindikiza wakarudi ubalozi na wako hapa hapa na hakuna kitu Magu angeweza kuwafanya.
Mabeberu yalikuwa yanatembea vifua mbele kumsindikiza mwamba lissu uku serikali ya jiwe ikiona hivi hivi[emoji23][emoji23]
 
Jpm was in a right direction. Kubali tu mkuu. Hata kama hakua smart jinsi ulivotaka ww. Tofautisha kuwa evil smart na kua mzalendo. Its better kua mzalendo. No matter how much upo smart. Lakini kama una misguide wananchi bado hai count.at the end of the day wananchi watakudai basic needs, justice, employment, land
Kwani walio kumbwa na madhira ya utawala wa JPM hawa kuwa raia wa nchii hii? nao hawakuhitaji mahitaji muhimu kama wengine?
 
Maisha ya Walibya chini ya Gaddafi hayakuwa mazuri kama ya wenzao wanaoishi kwenye tawala za Kidikteta za China, Saudi Arabia na Russia. Vijana hawakuwa na ajira kwa sababu hakukuwa na biashara nyingine zaidi ya uchimbaji mafuta.

Gaddafi Alitorosha matrilioni ya pesa kuweka kwenye akaunti zake binafsi nje ya nchi.

Aliitenga nchi upande wa Mashariki kwa sababu makabila ya huko hayakuukubali utawala wake.

Wimbi la Arab spring kupinga udikteta ilikuwa ni kudodonsha njiti tu kwa milipuko ambayo ilikuwa tayari kulipuka muda wowote.
Mkuu unweza funguka kidogo kuhusu sakata la mgogoro wa Libya ukizingatia maisha yao yalikuwa mazuri sana(tetesi)
 
Hakuwa na uwezo huo. Hata wazungu walijua he was just stupid with no impact.

Na kuthibitisha hilo, Tundu Lissu ( Mwanasiasa ambaye Magufuli alimchukia to the moon ) alihifadhiwa kwenye ubalozi wa Ujerumani na badaye wazungu wakamsindikiza kwenda Airport kupanda ndege mchana kweupeee huku akihitajika mahakamani.

Hao wazungu baada ya kumsindikiza wakarudi ubalozi na wako hapa hapa na hakuna kitu Magu angeweza kuwafanya.
Unajua taratibu za ku-deal na diplomatic envoy ya nchi nyingine wanapokuwa Tanzania?
 
NILIWAHI KUMWAMBIA HAYATTI MAGUFULI, LEO NARUDIA KWA RAIS SAMIA, ILI ASIJEPOTEZA MUDA WAKE.

Na, Robert Heriel

Niliwahi kuandika hapa miaka mitatu iliyopita, niliipa makala ile kichwa kisemacho "Rais Magufuli unapoteza muda wako tuu" katika makala ile watu wengi walinitukana, wengine walinitishia, sikuwalaumu kwani niliwaelewa lakini wao hawakuwahi kunielewa.

Leo hii narudia baadhi ya maneno yaleyale niliyoyasema siku zile.

Niliandika Magufuli anapoteza muda wake nikiwa na hoja zifuatazo;

1. Magufuli nilimuona anapoteza muda kwa sababu alikuwa na mtazamo kuwa, nchi ni tajiri na itapata maendeleo kwa sababu ina Rasilimali nyingi akizitaja kama madini, mbuga, ardhi kubwa yenye Rutuba, maziwa na mito yenye viumbe maji kama samaki, vivutio vya utaliii, bahari, kuzungukwa na mataifa mengi yasiyo na bahari, n.k.
Niliona anapoteza muda kwa sababu, nchi haiendelei kwa wingi wa Rasilimali isipokuwa inaendelea kwa ya kuwa na WATU WENYE AKILI. Watu wenye akili ndio wanaleta maendeleo nchini sio uwepo wa Rasilimali nyingi.

2. Magufuli aliamini, nchi itajengwa kwa kuwanyonya wananchi wake pekee, ndio maana alishindwa kuongeza mishahara miaka yake yote aliyotawala, pia akashindwa kutoa ajira mpya.
Kama hiyo haitoshi, sio ajabu aliongeza vikodi vya hapa na pale ili kuendesha serikali yake, lakini bado mambo yalimuwia magumu hali iliyomfanya ajiingize katika hatari ya kugombana na wafanyabiashara, wengi wao aliwaita wahujumu uchumi, wapo walioisoma.

Mimi nilimwambia nchi yoyote iliyoendelea haijawahi kuendelea kwa kutegemea unyonyaji kwa watu wake pekee, bali ni lazima ivamie mataifa mengine. Nilitoa mifano kwa baadhi ya mataifa yaliyoendelea yaliyojipatia utajiri kwa kunyonya watu wake na mataifa mengine.. Biashara ya utumwa, Ukoloni, na ukoloni mamboleo vyoote vinaangukia hapa.

Taifa kama la Korea ya kusini loo, liliamua kualika mataifa mengine hasa Mataifa ya Magharibi kuja kuwekeza Korea kusini. Kwa sasa Korea ni moja ya nchi zilizopo ulimwengu wa pili.

3. Magufuli aliamini kuongoza nchi kibabe ndio suluhu ya maendeleo, wakati mbinu hiyo ilishapitwa na wakati, na kwa vyovyote lazima ingelala upande wake na angeshindwa, licha ya kujitutumua kuchelewesha muda wa anguko lake.

Mimi nilimwambia kuwa kizazi cha sasa kinaongozwa kwa akili, ujanja, maarifa na mambo yote yahusuyo akili. Ubabe ungeweza kutumika machungani kwenye mbuzi, ng'ombe, na kondoo ambao hawana utashi kama binadamu.

Hakuna uhusiano wa karibu baina ya Ubabe na biashara, hivyo kivyovyote vile anguko la kiuchumi lilikuwa ni uhakika. Kwani hakuna mfanyabiashara ambaye angependa aishi kwa hovyo wakati pesa ni zake mwenyewe.

4. Magufuli aliamini kuwakaripia wengine mbele ya halaiki na wengine kuwatukana ndio namna ya kuleta nidhamu ndani ya serikali yake.
Wakati nidhamu ndani ya serikali hutokana na jinsi sheria zinavyofuatwa na kutelekezwa. Kama mtu ni mwizi basi sheria ingechukua mkondo wake,

Masikini wengi na watu walioshindwa walifurahishwa na magufuli kwa sababu ni kawaida ya masikini kuona mwenye nacho akianguka.

5. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye matamko kuliko kuweka mfumo imara ili hata yeye akiondoka mambo yatajiendesha vyema.
Niliwahi mwambia kuwa One manshow ni kama mbio za sakafuni ambazo lazima ziishie ukingoni. Nilimwambia anapoteza muda wake.

Maendeleo ni mfumo kama mnyororo unaounganisha seti nyingi ya vitu.
Maendeleo ya nchi za Afrika niya kubahatisha kwa sababu hakuna mfumo unaoeleweka.

6. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye kujipa promo kwenye vyombo vya habari na kujisifu, na kuwazima wengine ili kuchota akili za watu wenye upeo mdogo na kuzuia wale waliokuwa wanampa challenge kwa mitazamo yao.
Hii pekee ingetosha kuonyesha kuwa anapoteza Muda wake.
Hakuwa mtu kama Anthony Mtaka ambaye hafanyi manipulation lakini matendo yake yanaonekana.

7. Magufuli alifanikiwa zaidi katika kutekeleza na kusimamia maendeleo ya miundombinu, kwa hili nampa heko, lakini nilimuambia kuwa taifa masikini linawekeza kwenye watu na sio vitu,
Hii watu walinipinga lakini huo ndio ukweli mchungu, masikini kuwekeza kwenye vitu zaidi ya watu ni kupoteza muda na kuwatesa watoto.

8. Magufuli alijitahidi kujifanya hawapendi Wazungu na kila mara alitoa maneno ya kupata ushawishi kwa watu ili wawachukie wazungu. Ndio maana hata Mambo ya Corona aliyaona kama mchezo wa kuigiza na njama za wazungu kutuangamiza.

Jambo ambalo hata mtoto mdogo akifikiri anaona ni uongo wa mchana.
Nilimuunga mkono kwenye suala la kutokuweka Lockdown, lakini masuala mengine nilimpinga.

Magufuli angepoteza muda kwa vyovyote kwa kupinga mambo ya wazungu ambayo hata huo Urais aliokuwa nao ni mfumo wa kizungu, masuala ya jeshi ni mifumo ya kizungu, jina lake lakizungu, dini yake yakizungu na hata alipokufa alizikwa kizungu, hata elimu yake ni yakizungu, hata magari na vifaa vyote alivyokuwa akivitumia ni vyawazungu, achilia mbali madawa na miwani aliyokuwa akivaa. Sijazungumzia silaha na wana usalama waliokuwa wanamlinda ambao ili wawe wa kimataifa inapaswa wapewe mafunzo ya kizungu.

Kama wazungu wangetaka kutuua wangetuua tangu miaka ya 1900 huko walipokuja kututawala. na hata wakiamua kutuua uwezo huo wanao, na hatuna uwezo wa kufurukuta.

Sasa mambo hayo hayo, nayasema kwa Rais Samia, kuwa aangalie asije akapoteza muda wake kwa kushindwa kuendana na wakati.

Maendeleo ya nchi ya USA sio lazima yawe maendeleo kwa Tanzania. Hiyo ni muhimu kuzingatiwa.

Hata hivyo Rais Samia lazima azingatie haya ili naye asijikute katika kucheza Nage na kupoteza muda wake.

1. Maendeleo ni kuwekeza kwenye watu
2. Kuwekeza kwenye watu ni kuwapa Uhuru
3. Uhuru wa watu ni pamoja na kuwapa nafasi ya kuyafurahia maisha yao kwa kutumia rasilimali za nchi yao au kuvamia mataifa mengine. Passport zitolewe watu wakahangaike huku na huko.
4. Serikali isifikiri kunyonya wananchi wake pekee(kodi na ushuru) bali pia ifikiri namna ya wananchi wake kuenda nchi zingine kunyonya mali na utajiri wa nchi zingine.

5. SHeria na utawala bora zisiachwe
6. Ubabe wa kipumbavu uachwe maana palipo na ubabe au udikteta lazima kuwa na uasi/usaliti na palipo na usaliti lazima pawe na mapinduzi.

7. Serikali isijikite kwenye matamko ya kipuuzi puuzi. Kwani kwa kufanya hivyo itaathiri vijana wengi ambao wao kila kitu watataka tamko la serikali.

Sishangai kwa nini watu wanamlaumu Mama kuwa kwa nini ni mpole, ni kutokana na kuathiriwa na matamko yasiyo na kichwa wala miguu.

Sio kila kitu kitolewe tamko kwa kutafuta sifa za kijinga kwenye Kamera ili ionekane kazi inafanyika wakati hakuna kitu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam
Well noted mkuu. Mungu akubariki sana.

Hasa hapo kwenye kunyonya mataifa mengine nimependa sana.
 
Maisha ya Walibya chini ya Gaddafi hayakuwa mazuri kama ya wenzao wanaoishi kwenye tawala za Kidikteta za China, Saudi Arabia na Russia. Vijana hawakuwa na ajira kwa sababu hakukuwa na biashara nyingine zaidi ya uchimbaji mafuta.

Gaddafi Alitorosha matrilioni ya pesa kuweka kwenye akaunti zake binafsi nje ya nchi.

Aliitenga nchi upande wa Mashariki kwa sababu makabila ya huko hayakuukubali utawala wake.

Wimbi la Arab spring kupinga udikteta ilikuwa ni kudodonsha njiti tu kwa milipuko ambayo ilikuwa tayari kulipuka muda wowote.
Shida wabongo tunapenda sana story za kusimuliwa mara ooh ukioa unapewa nyumba,kila mwisho wa mwezi unalipwa nk
 
Back
Top Bottom