Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Big up mkuu, appreciation for you. Nuru imepenya gizani
 
Kwahiyo mnataka nchi ya miaka 60 ya uhuru ifanye vile nchi yenye miaka 300 inafanya!!
 
Na sasa wakawa wanaitwa wanyonge, wakaambiwa wapnge vitu mpaka njia za miguu
 
Nawaza nao wazungu wangesema msipelekee misaada wale nyani wa africa maana wao ni mabeberu jpm aliwaita na wao wangemuita nyani daaa
Kiluitwa beberu kwani ni tusi. Ukiitwa beberu si ndo inaashiria ww ni mtawala. Kwa hiyo kuwaita mabeberu naona kama ni sifa unawapa
 
Kumbe ukiambiwa wazungu akili yako inakwambia ni wazungu waliopo nchini!!!??

Ni biashara ngapi za wazungu hapa nchini ww, ule ujinga alikuwa anawaambia jiwe na nyie mkawa mnatembelea humohumo.
 
Upo sahihi 💯. Nashangaa Congo Ipo hapo na ni marafiki zetu. Kwanini hatujiongezi tukajifanye tunaenda kuimarisha ulinzi mashariki ya Congo tuchukue ule utajiri. Kanchi kadogo kama Rwanda kamejiongeza kanavuna tu, sisi tupo tu tunashangaa,na tuna jeshi bora kabisa
 
AMEN
 
Umejikita sana kwenye kukosoa na Bahati mbaya unazani umepatia kwenye mapendekezo.

Nikwambie tu kwamba umekosea mno.

Maendeleo ni Mchakato.
 
Jpm at the end of the day ametoa positive output na ameleta positive impact na amewaachia watu spirit.
Ndugu yangu watia huruma.
Eti watu hata wakiuawa, kubomolewa nyumba zao, kufungiwa account zao, kubambikiwa kesi, kutukanwa hovyo kwako ni sawa tu mradi inaleta positive impact?
Unaelewa maana yake kweli?
Huo ndio udikteta, udhalimu, ukandamizaji na dhambi kubwa kwa viwango vyovyote.
Au kwa vile hakuna mzazi wako/nduguyo aliyedhurika ndio wajitoa fahamu?
 
Magufuli was a hero. Itachukua muda sana kulifahamu hili. He was ahed of time.
 
Mwenda zake Kesha kwenda tuliobaki ni sisi AMA ZETU, AMA ZETU. Yapo yanayofikirisha ijapokua si kila mwenye akili anaweza kufikiria wengine hukariri.

Mkuu sifahamu umri wako, ila kwa uzoefu wa kutumia umri wangu, ukiwachekea watanzania utashika adabu yako.

Mwalimu Nyerere alisema, hakuna nchi inayoendeshwa bila Miko, akatupa AZIMIO LA ARUSHA.

Alhaj Mwinyi aliwahi sema nilipofungua milango wengine waliamua kupitia madirishani.

Mzee Mkapa akasema, MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE watu wakajibinafsisha serikali wakayaishi maisha, wakahomola.

Mzee wa Msoga yeye kaamua kucheka nasi tukamchekesha akacheka akagonga wakajua kalegea wakapiga wakagawana kwenye mifuko ya sandarusi.

Mwendazake akapitia historia akatumia uzoefu wake kitalani akaachana na mfumo akaunda Taski force akainyoosha nchi wazawa na wenyeji tukanyooka. Aliteleza kama mwanaadamu na alipatia pakubwa nchi ikajulikana kwamba mwamba akisema huwezi kujitikisa, tukalalamika tukaandika, tukafyonza lakini yeye alisema hajali anachotaka ni nchi isonge mbele na ikasonga.

THE END JUSTIFY THE MEANS

R.I.P Jiwe ulitoonyesha njia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…