Inatokea post namba 333. (natumai sijaruka sehemu).
Babu yangu akaendelea kunielezea.
Babu; Nilipoingia chumba changu cha private, Ramses akanisalimia, kwa sauti tu, ndio mara ya kwanza. Kwa kua nilishaambiwa, sikustuka sana, nikajibu salamu yake, akawa ananisemesha Kiaarabu cha Kimisri, nashukuru nilimuelewa ingawa nilikua sina uzoefu nacho lakini nilimfahamu, nikamwambia, tuongee Kiswahili, mimi nasikia Kiarabu chako, nakuelewa lakini mzito kuongea Kiarabu hicho. Akanambia, ongea lugha yoyote unaoijua vizuri.
Arsis: Shukran sana, nafahamu kazi ulioifanya sio ndogo, watu wengi wasingeiweza, watu wanaogopa majini, lakini wewe hukuogopa, mimi nafahamu ujasiri unaupata wapi, lakini hilo sio lililonileta leo.
Leo nimekuja kutoa shukran zangu, kujitambulisha na nimekuja kuitaka idhini yako tuwekeane mkataba.
Babu; Mkataba wa nini tena?
Arsis; Mimi niliweka ahadi aytakenitoa yeyote awe jini au binadam au kimbe mwengine yoyote nitamfundisha kila ninalolijua na nitakua karibu daima, mimi nafahamu elimu nyingi sana.
Babu; Hilo nipo tayari.
Arsis; Sijamaliza, pia nitakua rafiki yako na vizazi vyako mpaka utapofikia wakati wangu, sijui lini.
babu; kwanini ulifungwa?
Arsis; Elimu yangu ndio ilinifunga? Sikufungwa kwa kufanya maovu, nimefungwa kwa kufanya mema.
Babu; Nitaamini vipi?
Arsis; Nafahamu huwezi kuamini kwa sababu wewe unawaju majini, majini wengi waongo kama binadSISam. Mimi sio jini.
Babu; Wewe nani kama sio jini?
Arsis; Mimi mtu kam wewe kwa sasa, lakini naweza kua chochote kile. Isipokua nilipenda sana kua binadam ni binadam kwa miaka mingi sasa.
Babu; Unamaanisha nini kwa miaka mingi sana ni binadam, ulikua nani kabla hujawa binadam?
Arsis; Mimi naweza kua chochote, mimi nilijaaliwa kuweza elimu ya kuweza kua ninavyotaka, lakini nimependa kua binadam.
Babu; Unaitwa nani?
Arsis; Naitwa Arsis?
Babu; Wewe katika ukoo wa kifarauni?
Arsis; Hapana lakini niliishi na Ramses na Barsis.
Babu; Hao mafirauni?
Arsis; Ndio, nitakupa kitabu uwasome ukipenda.
Babu; Ninachoi kitabu nitawasoma.
Arsis; Safi sana, una elimu nzuri kwa kupenda kusoma. Ukipenda kusoma zaidi, mimi Mwalimu wa maboi mengi.
Babu: Sikiliza Rmses. Ungfahamu kwanini tumekufungua kifungo chako?
Arsis: Nafahamu kila kitu, nimeongea na Jini Bakora. Alikuja jini wa mgunya nikakataa kuongea nae mpaka kwa niongee na wewe. Sio kwa vibaya lakini ilikua ahadi yangu niliojiwekea. Nashukuru siku ile uliponitoa hukuumia. Ulikua na ulinzi mkubwa sana.
Babu; Nieleze kilitokufanya tukufungulie.
Arsis: Mali za Wajerumani za Amboni. Kuna habari mbaya sana mbili. Ya kwanza yule kijana hayupo tena duniani, toka siku mlionifungulia. Alikua hana ulinzi wa kutosha, wachawi wa kijjini wakammaliza.
Babu; Inna li llahi wa inna ilayhi rajijuna. Habari m baya nyingine ipi?
Arsis; Wajetunmani hawakuzika mali Amboni, walizika masanduku ya bunduki zao na mabomu ya mkono. mengi yameliwa na kutu, walizika sio mbali sana na bhari, chumvi imekula masanguku, sana sana mtakuta kutu na mabaki kidogo hayafai, sema kuna masanduku mtapata mbao zake, haziharibiki. Chuma yote imekwisha. Bora wangezamisha kwenye bahari mngekuta zote. Walifanya makosa, walifukia halafu wakaweka nondo na zege, na pale chumvi nyingi. Si unajua pale watu wanatengeneza chumvi?
Babu; Najua Ambini wanapotengeza vchumvi.
Arsis; Pale pale lakini kwa juu kule sio huku wanatengeneza chumvi. Juu kule kuna alama ya miti ya mibuyu mitatu na alama za mawe chini, watu wengi wamechimba pale. Lakini hakuna mali. Hiyo ndio habari mbaya ya pili.
Babu; Kweli hizo habari mbaya. Sisis tupo salama na hao majini?
Arsis; Mpo salama kabisa, wala usiwe na shaka wala hamtafutwi na jini yoyote. Jini Bakora ni hodari sana. Ameshafanya mikataba ya amani.
Babu: Nitaamini vipi unayonambia?
Arsis: Kwanza sina sababu ya kukudanganya, halafu utaona mwenyewe. Wewe nitumie, ninachoweza kufanya nitafanya.
Babu; Utataka malipo gani na kwanini nikutumie?
Arsis; Hakuna malipo yoiytite, mimi sio mchawi na sihitaji kitu chochote kutoka kwa binadam wala jiniyoyote. Naishi kwa uwezo wa Muumba wetu.
Babu; Kwanini usiwe na maisha yako.
Arsis; Mimi namisha yangu lakini nilipokua kifungoni nilikua naomba sana. Mwenyezi Mungu akakufanya wewe ndio sababu ya mimi kupata uhuru wangu. Niliahidi kwa nafsi yangu na kwa Mwenyezi Mungu, siwezi kuvunja ahadi yangu.
Babu; Sasa kazi tuliodhani utatufanyia hakuna tena. Dah sijui itakuaje, itabidi niongee na wenzangu.
Arsis; Sawa kabisa ongea nao lakini wao hawana haki na mimi kabisa sina ahadi nao, ahadi yangu inakua kwako uliekata ile mfuniko. Ile ndio kai kubwa kuliko zote; Ilifyngwa na mabiungwa wa uchawi wa kijini.
Babu; Kifungo chote hicho? unasema kwa ajili ya mema sio uovu?
Arsis; Ndio kama nilivyokueleza, hakuna sababu nyingine, ni isa kirefu.
babu; sasa mkataba wanini na mimi?
Arsis; Mkataba sio lazima wa kuandikiana mkataba ni kukubali tu ili wewe uelewe mimi niko na mimi nielewe upo na sisi ni marafiki na wewe ndio mwenye kauli kwangu. Tukikubaliana nitakupa mawasiliano yangu, nitakutengenezea pete kama hii yangu lakini kwa 'mada" za duniani.
Babu; akanambia mimi "Hapo ndipo aliponionesha pete hio ulioivaa bwana mkubwa".
Arsis: Wewe ongea na wenzako wote na wengine pia. Ukiona kuna ubaya, mimi nitakua mbali kabisa na wewe lakini ukinihitaji nitakuja haraka sana.
Babu; Sawa; Hauna kingine cha kunieleza.
Arsis; Kuna mengi sana ya kukukuele lakini kwanza malizeni mauzungumzo yenu, mtulizane mrudi kwenye kazi zenu, mimi yangu siyamalizi.
Babu: Sawa nimekuelew, nikikuhitaji niytakuita lakini mkataba kwa sasa tusubiri na mimi nifikiri, maana mambo yamekua mengi sasa.
Arsis; Sawa kabisa kwaheri.
Arsis akaenda zake.
Babu: haya bwana mkubwa swali lako limepata ufumbuzi au bado, hicho ndicho kisa cha kukutana na Ramses.
Mimi; Bbu sasa kuna maswali megi zaidi.
Babu: nakushauri suniri kwanza maswali yafikirie vizuri utaniuliza wakati wowote, sasa hivi subiri kwanza.
Mimi : sawa babu. Jitayarushe kunijibu kwanini Arsis akanipa mimi pete yake?
Babu: Hilo nitakujibu sasa hivi. Baada ya kua na Atsis miaka mingi akawa ananisisitiza nianze kuwarothisha wanagu ujuzi wangu lakini hakuna aliyeelekea isipokua wa kike, wote wengi e walikua wanapuuza, ulipozaliwa wewe tukaena huyu tumweke karibu tupate mrithi na mengine tumwachia Allah ndio ulipobalehe, Arsis akanambia ameona anaweza kua karibu sana na wewe, na kwa fadhila yake atakupa pete kama kwana zawadi yake na urafiki wetu na hana mpaka sasa wa kumpa jio pete, kwao huko unasema kabaki peke yake katika vizazi vyake. haya bwana mkuba usichomekee lingine.
Mimi haya babu: Ahsante, nitamuuliza mengine Arsis.
babu; tena atafurahi sana, anapenda sana maswali na kufundisha, kanikuta mimi sio mtru wa kuuliza uliza sana, sasa umri huu nisome nini tena, umri huu mimi wa kyfanya toba na kazi njema za watu. kwaheri babu.
Mimi; kwaheri babu.
Itaendelea.