habari wakuu. Weekend nyingine ya mwanzo wa mwezi february sasa.
mimi ni kijana (me) wa umri wa miaka 27 nilianza kuvuta sigara mwaka 2016 nikiwa advance.
NImevuta miaka sasa pamoja na kunywa pombe japo sikuwa addicted sana nilikua naweza kupitisha hata week bila kuvuta wala kunywa.
Lakini mwaka jana 2024 baada ya x mass niliamua kuacha kunywa pombe na kuvuta sigara nimefanikiwa sasa nina mwezi sijagusa pombe wala sigara.
Lakini napata tabu sana mchana najaribu ku keep busy na ikifika jion naenda mazoezi uwanjan napiga ball na aerobics nyingine ili kupunguza ashk ya kuludi nilipotoka.
Lakin hivi karibuni nimekuwa nakosa au napata usingizi kwa tabu na kwa kuchelewa sana huku nikiwa na hamu ya kuvuta. Hapo awali hadi mikono ilikua iktetemeka kama sijavuta. Lkn nilishinda hiyo hali sahivi nakosa usingizi.
Watu wa karibu ikiwemo jamaa na rafiki ndugu hawajui wala sijawai vuta mbele yao pombe at list walikua wananiona mara moja moja nikiwa nimechangamka
naomba ushauli ndugu wataalam wa afya na wengine ambao mlichukua maamuzi kama yangu kuacha hivi vitu ili nisiludi nilipotoka. Mtanisamehe kwa uandishi mmbovu