Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Tutafute kuona Mungu anatukuzwa iwe katika kuishi kwetu au kufa kwetu. Hii itawezekana tukiishi maisha masafi ya kumpendeza Mungu tukiwa mbali na dhambi. Tutafakari ujumbe huu kwa pamoja ili tuweze kuandaa mioyo yetu , maana hata sisi tunaojiona ni wazima sasa tunaweza tukaondoka tukamuacha huyu ndugu akiendelea na maisha.



JEHANUM YA MOTO



zachary-kakobe.jpg
Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO LA 6: JEHANUM YA MOTO

Yesu Kristo anatufundisha waziwazi kuhusu Jehanum ya moto, akituonya kumwogopa Mungu mwenye uwezo wa kututupa Jehanum. Anaendelea kutuonya kwamba, ni heri kukubali lolote lile litupate kuliko kwenda kwenye mateso makali ya Jehanum (LUKA 12:5, MATHAYO 5:22, 29-30). Maandiko pia yanaendelea kusisitiza kwa msisitizo mkubwa kwamba, ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai na kutupwa katika Jehanum ya moto (WAEBRANIA 10:26-27, 31). Jehanum hii ya moto inaitwa pia kuzimu (ZABURI 9:17) na tena inaitwa Tofeni (ISAYA 30:33). Hatupaswi kulipuuza jambo hili na kulifanya juu juu tu. Kwa sababu hii, leo, tutajifunza kwa undani kuhusu Jehanum ya moto, na tutaligawa somo letu katika vipengele vinne:-

(1) HUKUMU BAADA TU YA KUFA

(2) JEHANUM YA MOTO IKO WAP?

(3) HALI HALISI YA JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO

(4) JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO

( 1 ). HUKUMU BAADA YA KUFA

Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu (WAEBRANIA 9:27). Watu wanaofundisha kinyume na kweli ya neno, hufundisha kwamba mtu anapokufa analala tu na hakuna lolote la hukumu ya mara moja. Wanatumia maandiko yanayozungumzia kulala kwa kuyatafsiri isivyo (MATHAYO 27:52; 1 WAKORINTHO 15:20; YOHANA 11:11-14 n.k ) na pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo ni kwamba kinachobaki kaburini ni mwili tu. Nafsi na roho ya mtu huondoka kwa kuvalishwa mwili mwingine ( 1WAKORINTHO 15:40 ). Mwili unaobaki kaburini ndiyo ambao umelala haujui lolote na hauna kumbukumbu, lakini pasipo mwili huo mtu atamwona Mungu ikiwa ameishi katika mapenzi yake (AYUBU 19:26). Mwili hubaki kaburini, lakini roho ya mtu huondoka (MHUBIRI 12:7). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu mara tu ya kufa huchukuliwa mbinguni na malaika kwa kutumia magari maalum ya mbinguni (LUKA 23:43; 16:22; 2WAFALME 2:11-12; ZABURI 68:17; WAEBRANIA 1:7, 14). Ikiwa ameishi katika dhambi hukumu yake huwa kutupwa katika Jehanum ya moto mara tu baada ya kufa (MITHALI 9:13-18; ISAYA 5:11-15; MITHALI 17:24-27).

( 2 ). JEHANUM YA MMOTO IKO WAPI?

Mtu anapokufa tu, huwa kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni, hata hivo ikiwa jina lake haliko katika kitabu cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni na hulazimika kukamatwa na kutupwa Jehanum (UFUNUO 19:20; 20:10). Mbinguni ni juu (mbingu ya tatu) lakini kuzimu au Jehanum ya moto ni chini (pande za chini za nchi) 2WAKORINTHO 12:1-4; ITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14.

( 3 ). HALI HALISI YA JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO

Jehanum ya moto ni kuzimu au shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Moto huu huwashwa mfululizo kwa pumzi ya Bwana (ISAYA 14:15; 30:33). Moto ni mkali kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani, uwe gesi, umeme, makaa yam awe au lolote jingine (WAEBRANIA 10:27). Moto huu ni mweusi unaosababisha giza na kufanya mtu awaone wenzake wachache tu wa karibu naye (MATHAYO 11-12; 22:13; 25:30 YUDA 1:6).Moto huu una uwezo wa kula na kutafuna, kwa hiyo huwatafuna au kuwala wale walioko motoni (KUMBUKUMBU LA TORATI 32:22; WAEBRANIA 10:36-27). Hata hivyo, kama jinsi ambavyo chumvi inavyozuia nyama kuharibika, moto humtafuna mtu lakini hamaliziki (MARKO 9:43-49). Ni moto wa milele (MATAYO 25:41). Mafundisho potofu ysnswafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa au kupotea na kuangamia kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 ( kuangamizwa ) na YOHANA 3:16 ( kupotea ). Kuangamia hakumaanishi kualizika kabisa (ESTA 4:16). Kondoo akipotea haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na mchungaji (angalia ISAYA 57:1-3). Vilevile neno “kuharibu” linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni la kuzdhibu vikali ( 1WAKORINTHO 3:16-17 ). Waalimu hawa wa uongo hufundisha pia kwamba ati watu watatoweshwa kama moshi baada kwa kuunguzwa kwa kutumia ZABURI 37:20. Kutoweshwa hapa ni kutenganishwa mbali na Mungu. Moto wa milele, huambatana na madini yanayoitwa kiberiti (lugha ya kitaalam, “sulphur”). Madini haya yakiwaka huwa kama mpira na hutoa harufu kama ya mayai yaliyooza. Harufu ya namna hii inafunika kuzimu yote. Siyo hayo tu, katika moto huu wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi katika miili yao wakiingia na kutoka. Hii hufanya sura zao kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA 14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24).Jehanum ya moto, huitwa pia mauti ya pili (UFUNUO 21:8). Uchungu wa mauti unaompata mtu anapokufa, huwa juu ya mtu motoni, milele na milele (UFUNUO 20:10). Watu walioko motoni hujawa wakati wote na vilio na tena husaga meno yao kama mtu anayeona baridi kali MATHAYO 8:12). Kuzimu, urikalo ni pigo lif urikalo ambalo huwachukua wenye dhambi asubuhi, mchana na usiku (ISAYA 28:15, 18-19). Walioko motoni wanajifahamu, na kuwakumbuka wenzao waliowaacha duniani na tena hutoa ndimi zao nje wakitamani maji kidogo kupoza ulimi (LUKA 16:19-24). Juu ya yote hayo, katika vilio vyao, humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Yeye amekwishasema, “Nami jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma” (EZEKIELI9:10;8:18).

USEMI NA FIKRA ZA WALE WALIOKO MOTONI

Watu walioko motoni hutamani mtu mmoja kati yao aje awashuhudie ndugu zao ili wayoache dhambi na kukwepa mateso yao (LUKA 16:27-31). Wale walioko huko wajiopata mafundisho haya kabla, husema, “Jinsi nilivyochukia maonyo, na na moyo wangu ukadharau kukemewa; wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, wala sikuwategea sikio langu walionifundisha (MITHALI 5:11-13)” Wakimwona yeyote anayejiunga nao, humwambia, “Jew ewe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe ummekuwa kama sisi!” ( ISAYA 14:9-10).

WALIO MBINGUNI HUPEWA NAFASI YA KUWACHUNGULIA

Walioko mbinguni watatoka kidogo kuwaangalia (ISAYA 66:24) ila hawatakuwa na machozi yoyote juu yao.

TOFAUTI KATI YA JEHANUM YA MOTO NA ZIWA LA MOTO

Jehanum ya moto ni tofauti na ziwa la moto linalotajwa katika UFUNUO 20:14-15; 21:8 kwa jinsi ileile mbingu ya sasa ilivyo tofauti na mbingu mpya inayotajwa katika UFUNUO 21:1. Ziwa la moto kwa sasa halina mkazi ndani yake. Watakaokuwa wa kwanza kuingia humo watakuwa mnyama (Mpinga Kristo) na nabii wa uongo (UFUNUO 19:20). Kisha atafuata ibilisi ambaye atatupwa humo baada ya vita ya Gogu na Magogu (UFUNUO 20:7-10). Baada ya hapo kutafuata hukumu ya jiti cha enzi, kikubwa cheupe. Hukumu hii itatolewa baada ya ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu ambao utawafufua walioko Jehanum ya moto.Baada ya hawa kuelezwa kwa nini wamehukumiwa adhabu ya matesoya milele, ndipo watakapotupwa katika ziwa la moto. Mateso yaliyoko ziwa la moto ni zaidi sana kuliko mateso ya Jehanum ya moto. Ni kama Jehanum walikuwa mahabusu na sasa wanapelekwa gerezani. Kama mbingu mpya itakavyokuwa nzuri zaidi kuliko mbingu ya sasa, vivyo ziwa la moto litakuwa na mateso yaliyokithiri kuliko Jehanum ya moto.

( 4 ). JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO

1 .Kuungama dhambi na kuziacha (MITHALI 28:13).

2. Kulishika Neno la Mungu kwa kufanya maagizo yote ya Mungu na kuwakata wafariji wenye kutaabisha wanaosema kufanya hili na lile siyo lazima ( YOHANA 8:51; ZABURI 119:6; AYUBU 16:1-2 ).

3. Kutohesabu sheria kuwa kutu kigeni. Kukubali kuongozwa na sheria ya Kristo. Hakuna mwanafunzi asiyeishi kwa sheria ( HOSEA 8:12; WAGALATIA 6:2; ISAYA 8:16 ).

4. Kuwa mtakatifu na kutoifuatisha namna ya dunia hii katika mavazi, usemi, matendo n.k. ( WAEBRANIA 12:14; WARUMI 12:2; YAKOBO 4:4; 1YOHANA 2:15-17 )

JE! WEWE NAWE UMEKUWA DHAIFU KAMA SISI!

ISAYA 14:9-10


Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya , usifanye moyo wako kuwa mgumu. Hii ni nafasi ya kipekee ya juisalimisha na hatari ya kutupwa katika jehanam ya moto . Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo? Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2). Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje? Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77). Je, uko tayari kuokoka sasa hivi? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, “Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
KUNYAKULIWA KWA KANISA
2. DHIKI KUBWA
DHIKI KUBWA
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO– ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA YA HAR-MAGEDONI
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
6. UFUFUO WA WAFU
UFUFUO WA WAFU
7. JEHANUM YA MOTO
JEHANUM YA MOTO
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/229-2/
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
Mtu anaumwa hálafu unamletea haya maporojo yako marefu ya kukopi na kupesti atayasoma saa ngapi, kwann usimshauri tu amuombe Mungu kwa ímani yake
 
Acheni kumdanganya!!! Pancreatic cancer stage 4 has no treatment. Only he supposed to palliative care including psychosocial support.
Duniani wote tunapita!!! Tangulia kamanda na sisi tutakufuata, tuandalie makazi yetu huko.
Inauma sana hii!!! Mungu akupe nguvu katika wakati huu mgumu.
Wakati mwingine huwa nawaza ni nani alianzisha maradhi yote haya makali.
Bora ulivyokuwa muwazi kuliko hão wanaomdanganya akapigwe pesa na TB jushoa
 
mimi kusema pole ila unaweza ukawa kweli umeombewa na nikwambie maombi hayo ndo labda yamekuweka hai hadi leo sasa fanya hivi na mimi nishiriki kutoa msaada fulani nii box walau nianze maombi kwa ajili yako. Yeye ni Mungu wa wote wenye mwili kuna neno lolote nisiloliweza? nikipata walau jina lako tuu maana walitambuliwa kwa majina yao.
 
Kwako wewe usiyemwamini Mungu hakuna treatment. Kumbuka kuwa Daktari Mkuu kabisa ni Mungu. Yeye ndiye aliyemuumba na yeye ana uwezo na afya yake. Tumeshuhudia waliokuwa na hali mbaya kuliko Folk, lakini kwa uwezo wa Mungu wamepona na wako hai. Acha kumfanya mwenzio akate tamaa. Mwache apambane na Mungu wake.
Na waliomwamini Mungu wakafa wao inakuaje kifo ni sayansi na wote tutakufa mnataka apoteze tena dola 3000 ebu kuweni na huruma au mnataka mumuue kabla ya muda
 
Nikufafanulie vizuri hapo kwenye kuchemsha mihogo. Hakikisha mihogo inayonunuliwa ni fresh kabisa na isiwe imeshaanza kuwa bluu. Wakati wa kuchemsha hakikisha maji yanafunika mihogo na tafadhali sana usifunike sufuria na mfuniko iache wazi ili mvuke uondoe kisichohitajika ndani ya mihogo. Ikiishaiva toa mihogo kwenye maji haraka sana uiweke kwenye chombo safi. Wakati wa kuchemsha usichanganye na chochote, hata chumvi usiweke.
Kwa kipindi chote utakachokuwa unakula mihogo kama tiba tafadhali usitumie tangawizi (ginger) wala chochote chenye tangawizi i.e. soda, biscuits etc. Kama unataka kujua kwa nini imekatazwa kufunika wakati wa kuchemsha au kutumia tangawizi, tafadhali nenda Google andika "Cassava for Cancer" utapata majibu mazuri kabisa ya kisayansi.
Nafikiri hii itakuwa imesaidia wengi pia wenye tatizo kama la Folk. Mungu awafanyie wepesi.
Hao madakitari bingwa hájui hizo porojo ulizoziandika hapo pamoja na utaalamu wao wote
 
Najua hili bandiko umelicopy mkuu halikuhusu kabisa ila ulivyolileta kama linakuhusu vile
Ila kama ni inakuhusu basi bila kujali dini au dhehebu lako sali sala ya salaam maria, atukuzwe baba mwana na roho mtakatifu, na tunaukimbilia ulinzi wake Mungu kila siku usiku wa manane maana utakutana na haja ya moyo wako najua unataka kupona we sali tu hiyo sala matokeo ni ndani ya miezi 3 kama ukiwa mwaminifu kusali
 
Walau umepata muda wakutubu na kutengeneza njia yako kwa miezi iliyo baki.. Tumia muda huo kuandaa safari yako na pumziko lako la muda. Mana punde utaamka tena kwa uzima wa milele... Walau wewe umepata hata muda wakujua utalalaje kuliko yule afae ghafla kwa ajali ama namna ingine.. Hutakufa rafiki utalala ama kupumzika.. Tupo njiani yawezekana hata tukawahi kabla yako hiyo miezi 4.
 
Najua hili bandiko umelicopy mkuu halikuhusu kabisa ila ulivyolileta kama linakuhusu vile
Ila kama ni inakuhusu basi bila kujali dini au dhehebu lako sali sala ya salaam maria, atukuzwe baba mwana na roho mtakatifu, na tunaukimbilia ulinzi wake Mungu kila siku usiku wa manane maana utakutana na haja ya moyo wako najua unataka kupona we sali tu hiyo sala matokeo ni ndani ya miezi 3 kama ukiwa mwaminifu kusali
Mmh!! Kama anaongopa lengo lake ni sasa?
 
Sali sana mwombe mungu atende miujiza yake hakuna linaloshindikana mbele ya mungu....... Nimeumia sana kwani juzi rafiki yangu amezikwa na alijua kifo chake ni lini....... Mungu akupe imani uzidi kumtumainia yeye
 
Pole sana jamani... Toka asubuhi nasoma tuu huu uzi, nimekosa hata la kuandika zaidi ni machozi.

Uko kwenye kipindi kigumu mnooo, kwa akili yangu ndogo nawaza labda wasingekuambia kabisaaa! Hiyo ya kusubiria siku ndo yakuumiza zaidi, najua sote tutakufa lakini hakuna alotayari kutangulia!!

Mungu azidi kukutunza jamanii!! Daaah
 
Madaktari ni wapiga Ramli tu wakati mwingine kama walivyo wale wababaishaji wengine wa Tiba asilia
Ukiwa na Imani nao utawaamini kwa lolote.

Kwanza;
Wanawezaje kujua mwisho wa maisha ya binadamu?

Najua wapo watakaomwaga Povu hapa.
Ila,sikilizeni;
Yupo mzee mmoja (Sasa Marhum),
Yeye aliugua sana hadi watoto wake wakaelezwa na Dakitari kuwa mzee wao alipofikia hana hata Mwezi atapoteza Maisha.

Ndugu hadi nao wakakata tamaa baada ya kuchomwa na ramli hiyo ya
Dakitari, -Tena Mzungu,
Wazazi waliposikia taarifa hiyo kumhusu mwanawao mgonjwa,
Wakasema tuleteeni mwanetu kijijini japo atufie mikononi mwetu.

Basi,
Amini usiamini mzee yule afya ilimrejea alipofikia kijijini na alipona kabisa.

Mzee yule alifariki miaka kumi na tano (15) baadae tena kwa maradhi yasiyokuwa na uhusiano kabisa na yale ya mwanzo.

Ndugu,
Uamuzi ni wako aidha kuanza kujiua kabla ya wakati wako kwa kujiumiza na mawazo hasi Badala ya kuwa na Imani chanya kuwa Mungu pekee ndie mwenye uwezo na milki ya Uhai wako.

Wewe upo hai na utaendelea kuwa na uhai Nasi pia wote tutabaki kuwa hivyo hadi pale mwenye milki yetu atakapoamua vinginevyo.

Uhai ni Vita tupambane,
Maradhi ni changamoto,
Tuzishinde kwa jasho hadi pumzi ya mwisho.

Na kisha siamini kuwa ni sahihi na maadili kwa Dakitari kumpa mgonjwa taarifa za aina hii au unatutengeneza?

Kama kafanya hivyo amekosea huyo Dakitari
Na amepotoka.
 
Ni heri umwamini Yesu yupo,, anaokoa na anaponya na baada ya maisha haya atahukumu wazima na wafu, kuliko kutokuamini halafu siku ukifa ukutane nae.

Nakushauri mtafte mchungaji wa kanisa la kirhoho akuongoze sara ya toba ili uwe tayari hata ikitokea umeondoka.
 
Madaktari ni wapiga Ramli tu wakati mwingine kama walivyo wale wababaishaji wengine wa Tiba asilia
Ukiwa na Imani nao utawaamini kwa lolote.

Kwanza;
Wanawezaje kujua mwisho wa maisha ya binadamu?

Najua wapo watakaomwaga Povu hapa.
Ila,sikilizeni;
Yupo mzee mmoja (Sasa Marhum),
Yeye aliugua sana hadi watoto wake wakaelezwa na Dakitari kuwa mzee wao alipofikia hana hata Mwezi atapoteza Maisha.

Ndugu hadi nao wakakata tamaa baada ya kuchomwa na ramli hiyo ya
Dakitari, -Tena Mzungu,
Wazazi waliposikia taarifa hiyo kumhusu mwanawao mgonjwa,
Wakasema tuleteeni mwanetu kijijini japo atufie mikononi mwetu.

Basi,
Amini usiamini mzee yule afya ilimrejea alipofikia kijijini na alipona kabisa.

Mzee yule alifariki miaka kumi na tano (15) baadae tena kwa maradhi yasiyokuwa na uhusiano kabisa na yale ya mwanzo.

Ndugu,
Uamuzi ni wako aidha kuanza kujiua kabla ya wakati wako kwa kujiumiza na mawazo hasi Badala ya kuwa na Imani chanya kuwa Mungu pekee ndie mwenye uwezo na milki ya Uhai wako.

Wewe upo hai na utaendelea kuwa na uhai Nasi pia wote tutabaki kuwa hivyo hadi pale mwenye milki yetu atakapoamua vinginevyo.

Uhai ni Vita tupambane,
Maradhi ni changamoto,
Tuzishinde kwa jasho hadi pumzi ya mwisho.

Na kisha siamini kuwa ni sahihi na maadili kwa Dakitari kumpa mgonjwa taarifa za aina hii au unatutengeneza?

Kama kafanya hivyo amekosea huyo Dakitari
Na amepotoka.
Sio kweli. Wanatumia vipimo. Mm mama yangu alikufa kwa kansa hii hii. Tuliambiwa kuwa ana siku 40 za kuishi. Na yeye aliambiwa pia na mama aliaga watu wote na kusameheana na wale ambao alikuwa nao vibaya . Mm nlienda kuandaa mazishi ya mama kabla akiwa hai zilivyobaki wiki moja. Na nlimuaga kuwa naenda kuandaa mazishi yake. I was happy mama alikufa akiwa kaweka mambo sawa. Na sikulia hata kidogo
 
Nimedhoofika sana. Nitakufa punde.
Hapana kaka angu siku yako ya kufa mungu anaijua usiumie kiasi hicho wanadamu wote tutapitia huko lakini siyo kwa namna ambavyo doctor kasema,pole ndugu
 
Pole sana kijana.Lakini USIMLAUMU Mungu hata kidogo. Anajua anachofanya. Sisi wote tutakufa. Lakini wewe Mungu amekupa 'priviledge' (bahati) ya kujua utakufa lini. Mshukuru kwa hilo. Mshukuru kwa kuwa sisi wote tutakaobaki duniani, na wale ambao watakuzika hakuna hata mmoja anayejua atakufa lini. Lakini wewe unajua. Leo, kuna watu waliokuwa wanaenda kuzika mwanafamilia lakini familia nzima ya watu wanane wakafia kwenye ajali gari lao lilipogonga basi.

Ndio maana nakwambia wewe mshukuru Mungu. Mshukuru Mungu kwa kukupa nafasi ya kutubu dhambi zako. Kwa hicho kipindi ambacho unangojea kifo, tubu dhambi zako zote ulizomtendea. Waombe samahani wale wote unaodhani uliwakosea. Nakuhakikishia utakapokuwa unawaaga ndugu jamaa na marafiki zako, wao watakuwa na uchungu hata kuliko wewe. Halafu kubali kungojea kifo. Waambie marafiki zako wakuletee kile unachotaka kula au kunywa na ukikipata ukitumie kwa furaha.

Usiogope kufa. Wala usijali kwamba unakufa ukiwa bado kijana. Kuna vijana hata wadogo kuliko wewe ambao tayari wamehukumiwa kifo kwa kuua wakati katika maisha yao hawakuwa kamwe wanawaza wataweza kumuua mtu. Aliyehukumiwa hivyo anangoja kufia jela bila faida yoyote kwa maisha yake. Labda Mungu ameamua utoke duniani sasa maana labda huko baadaye ungejikuta uko jela umefungwa maisha. Mambo ya Mungu hayachunguziki.

Ni kweli kabisa sio rahisi kabisa kukubali kifo. Lakini narudia tena. Mshukuru Mungu maana amekupa nafasi ya kufa kwa amani ukiwa huna tena kinyongo na mtu na umeshaelezea ndugu na jamaa yote ya kukupa amani moyoni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom