Pole sana Folk, Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema akatende jambo jema katika afya yako. Ninakushauri uende kwa TB Joshua. Nimeshuhudia wagonjwa wengi wa Cancer za aina mbali mbali wakiponywa. Cha muhimu kwako ni kuwa na IMANI kuwa YESU anaweza. Mara nyingi magonjwa yanakuwa chanzo chake ni mapepo. Kama ulivyosema katika andiko lililopita kuwa katika familia yenu kuna watu wanawaonea husda na chuki. Hiyo tu inaweza kusababisha kuwa na hiyo hali uliyo nayo leo. Hata kama hakuna aliyekuloga au kutumia uchawi juu yako, Shetani anapenda kutumia hali ya kutokuelewana katika jamii kuleta mateso na haswa kwa anayeonekana kuwa tegemeo la familia kama ilivyotokea kwako.
Najua kabisa kuwa unaweza usiwe na uwezo wa kwenda kumuona TB Joshua leo kutokana na hali ngumu ya maisha. Ninakuomba basi utembee kidogo kama mtu anayefanya mazoezi, ufike pale Mbezi Beach Secondary, Just opposite na gate la ukumbi wa Kiramuu utaona Gate limeandikwa SCOAN. Ingia pale na utapata msaada mkubwa sana. Hapo panatumika kama kituo cha sala na maombi kwa wafuasi na wanaoamini uponyaji kupitia TB Joshua. Pia panatumika kuandaa safari za kwenda kwa TB Joshua kwa wale wanaohitaji kufanya hivyo. Lakini pia kuna waombeaji makini sana na unaweza ukajikuta tatizo lako linaishia hapo na wala usiwe tena na haja ya kwenda kwa TB Joshua. Nina uhakika wa asilimia 100 kuwa utarudi kwenye jukwaa hili kutoa ushuhuda.
Wakati ukifuatilia hayo yote, nakuomba uwe unakula kipande cha mhogo fresh wa kuchemsha kila siku asubuhi, mchana na jioni. Kiasi ni gram 10 na hakikisha anayechemsha asifunike sufuria. Cha muhimu zaidi ni kuhakikisha unapata mhogo fresh ambao haujaanza kuwa na rangi ya blue. Ndani ya mihogo kuna vitamin B17 ambayo inatumika kupambana na cancer cells. Naomba uingie google usome zaidi ili kujiridhisha. Nina rafiki yangu ana cancer ya damu na amefanikiwa sana sana kwa kula mihogo na kunywa glass moja ya juice ya majani ya mastaferi hivyo hivyo asubuhi, mchana na jioni.
Kwa waliozingatia kula mihogo kama nilivyokuambia hapo juu baadhi yao wamekuwa cancer free baada ya mwezi mmoja tu. Wengine iliwachukua miezi miwili hadi mitatu kutegemeana na stage waliyoko. Kwa kuwa mihogo ni chakula, nakuomba ujaribu maana huna utakachopoteza.
Nakutakia Afya njema na Mkono wa Bwana wetu YESU Kristo ukuguse.