Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Mtu anaumwa hálafu unamletea haya maporojo yako marefu ya kukopi na kupesti atayasoma saa ngapi, kwann usimshauri tu amuombe Mungu kwa ímani yake
 
Bora ulivyokuwa muwazi kuliko hão wanaomdanganya akapigwe pesa na TB jushoa
 
mimi kusema pole ila unaweza ukawa kweli umeombewa na nikwambie maombi hayo ndo labda yamekuweka hai hadi leo sasa fanya hivi na mimi nishiriki kutoa msaada fulani nii box walau nianze maombi kwa ajili yako. Yeye ni Mungu wa wote wenye mwili kuna neno lolote nisiloliweza? nikipata walau jina lako tuu maana walitambuliwa kwa majina yao.
 
Na waliomwamini Mungu wakafa wao inakuaje kifo ni sayansi na wote tutakufa mnataka apoteze tena dola 3000 ebu kuweni na huruma au mnataka mumuue kabla ya muda
 
Hao madakitari bingwa hájui hizo porojo ulizoziandika hapo pamoja na utaalamu wao wote
 
Najua hili bandiko umelicopy mkuu halikuhusu kabisa ila ulivyolileta kama linakuhusu vile
Ila kama ni inakuhusu basi bila kujali dini au dhehebu lako sali sala ya salaam maria, atukuzwe baba mwana na roho mtakatifu, na tunaukimbilia ulinzi wake Mungu kila siku usiku wa manane maana utakutana na haja ya moyo wako najua unataka kupona we sali tu hiyo sala matokeo ni ndani ya miezi 3 kama ukiwa mwaminifu kusali
 
Walau umepata muda wakutubu na kutengeneza njia yako kwa miezi iliyo baki.. Tumia muda huo kuandaa safari yako na pumziko lako la muda. Mana punde utaamka tena kwa uzima wa milele... Walau wewe umepata hata muda wakujua utalalaje kuliko yule afae ghafla kwa ajali ama namna ingine.. Hutakufa rafiki utalala ama kupumzika.. Tupo njiani yawezekana hata tukawahi kabla yako hiyo miezi 4.
 
Mmh!! Kama anaongopa lengo lake ni sasa?
 
Sali sana mwombe mungu atende miujiza yake hakuna linaloshindikana mbele ya mungu....... Nimeumia sana kwani juzi rafiki yangu amezikwa na alijua kifo chake ni lini....... Mungu akupe imani uzidi kumtumainia yeye
 
Pole sana jamani... Toka asubuhi nasoma tuu huu uzi, nimekosa hata la kuandika zaidi ni machozi.

Uko kwenye kipindi kigumu mnooo, kwa akili yangu ndogo nawaza labda wasingekuambia kabisaaa! Hiyo ya kusubiria siku ndo yakuumiza zaidi, najua sote tutakufa lakini hakuna alotayari kutangulia!!

Mungu azidi kukutunza jamanii!! Daaah
 
Madaktari ni wapiga Ramli tu wakati mwingine kama walivyo wale wababaishaji wengine wa Tiba asilia
Ukiwa na Imani nao utawaamini kwa lolote.

Kwanza;
Wanawezaje kujua mwisho wa maisha ya binadamu?

Najua wapo watakaomwaga Povu hapa.
Ila,sikilizeni;
Yupo mzee mmoja (Sasa Marhum),
Yeye aliugua sana hadi watoto wake wakaelezwa na Dakitari kuwa mzee wao alipofikia hana hata Mwezi atapoteza Maisha.

Ndugu hadi nao wakakata tamaa baada ya kuchomwa na ramli hiyo ya
Dakitari, -Tena Mzungu,
Wazazi waliposikia taarifa hiyo kumhusu mwanawao mgonjwa,
Wakasema tuleteeni mwanetu kijijini japo atufie mikononi mwetu.

Basi,
Amini usiamini mzee yule afya ilimrejea alipofikia kijijini na alipona kabisa.

Mzee yule alifariki miaka kumi na tano (15) baadae tena kwa maradhi yasiyokuwa na uhusiano kabisa na yale ya mwanzo.

Ndugu,
Uamuzi ni wako aidha kuanza kujiua kabla ya wakati wako kwa kujiumiza na mawazo hasi Badala ya kuwa na Imani chanya kuwa Mungu pekee ndie mwenye uwezo na milki ya Uhai wako.

Wewe upo hai na utaendelea kuwa na uhai Nasi pia wote tutabaki kuwa hivyo hadi pale mwenye milki yetu atakapoamua vinginevyo.

Uhai ni Vita tupambane,
Maradhi ni changamoto,
Tuzishinde kwa jasho hadi pumzi ya mwisho.

Na kisha siamini kuwa ni sahihi na maadili kwa Dakitari kumpa mgonjwa taarifa za aina hii au unatutengeneza?

Kama kafanya hivyo amekosea huyo Dakitari
Na amepotoka.
 
Ni heri umwamini Yesu yupo,, anaokoa na anaponya na baada ya maisha haya atahukumu wazima na wafu, kuliko kutokuamini halafu siku ukifa ukutane nae.

Nakushauri mtafte mchungaji wa kanisa la kirhoho akuongoze sara ya toba ili uwe tayari hata ikitokea umeondoka.
 
Sio kweli. Wanatumia vipimo. Mm mama yangu alikufa kwa kansa hii hii. Tuliambiwa kuwa ana siku 40 za kuishi. Na yeye aliambiwa pia na mama aliaga watu wote na kusameheana na wale ambao alikuwa nao vibaya . Mm nlienda kuandaa mazishi ya mama kabla akiwa hai zilivyobaki wiki moja. Na nlimuaga kuwa naenda kuandaa mazishi yake. I was happy mama alikufa akiwa kaweka mambo sawa. Na sikulia hata kidogo
 
Nimedhoofika sana. Nitakufa punde.
Hapana kaka angu siku yako ya kufa mungu anaijua usiumie kiasi hicho wanadamu wote tutapitia huko lakini siyo kwa namna ambavyo doctor kasema,pole ndugu
 
Pole sana kijana.Lakini USIMLAUMU Mungu hata kidogo. Anajua anachofanya. Sisi wote tutakufa. Lakini wewe Mungu amekupa 'priviledge' (bahati) ya kujua utakufa lini. Mshukuru kwa hilo. Mshukuru kwa kuwa sisi wote tutakaobaki duniani, na wale ambao watakuzika hakuna hata mmoja anayejua atakufa lini. Lakini wewe unajua. Leo, kuna watu waliokuwa wanaenda kuzika mwanafamilia lakini familia nzima ya watu wanane wakafia kwenye ajali gari lao lilipogonga basi.

Ndio maana nakwambia wewe mshukuru Mungu. Mshukuru Mungu kwa kukupa nafasi ya kutubu dhambi zako. Kwa hicho kipindi ambacho unangojea kifo, tubu dhambi zako zote ulizomtendea. Waombe samahani wale wote unaodhani uliwakosea. Nakuhakikishia utakapokuwa unawaaga ndugu jamaa na marafiki zako, wao watakuwa na uchungu hata kuliko wewe. Halafu kubali kungojea kifo. Waambie marafiki zako wakuletee kile unachotaka kula au kunywa na ukikipata ukitumie kwa furaha.

Usiogope kufa. Wala usijali kwamba unakufa ukiwa bado kijana. Kuna vijana hata wadogo kuliko wewe ambao tayari wamehukumiwa kifo kwa kuua wakati katika maisha yao hawakuwa kamwe wanawaza wataweza kumuua mtu. Aliyehukumiwa hivyo anangoja kufia jela bila faida yoyote kwa maisha yake. Labda Mungu ameamua utoke duniani sasa maana labda huko baadaye ungejikuta uko jela umefungwa maisha. Mambo ya Mungu hayachunguziki.

Ni kweli kabisa sio rahisi kabisa kukubali kifo. Lakini narudia tena. Mshukuru Mungu maana amekupa nafasi ya kufa kwa amani ukiwa huna tena kinyongo na mtu na umeshaelezea ndugu na jamaa yote ya kukupa amani moyoni.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…