Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Maisha haya ni fumbo kubwa sana tulilopewa na Mwenyezi Mungu.pumzika kwa amani ndugu yetu uliyetutangulia mwanga wa milele ukuangazie.inauma zaidi ya maelezo yote tunayoweza kuandika bye bye broo till we met again [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Jaribu kuja kanisa la korogwe Kkkt hapa kwa mvhungaji mastay anaombea sana hizo kansaa utapona nakuhakikishia na hutatoa ata sh kumii wala hutakufa, pole sana kwa maumivu kuwa tu na imanii Mungu ndio mponyaji
Unaemwambia aende kwa Mastai ni nani, ni hawa wanaocomment au marehemu folk?
 
Unfortunately enough, Folk hakuwahi kuomba hela, msaada wala mchango wowote kuanzia matibabu yake hadi kifo chake.

Hivyo, kwa mtu mwenye credibility kubwa hapa JF kama wewe kuibuka na allegations na accusations kama hizi kumhusu marehemu inasikitisha saana.

Muombe radhi marehemu.
Ahsante chief..
Nakumbuka kijana liomba na akatamani kumlipa yeyote ambae angeeza saidia yalio msibu wakati wa uhai wake...
 
Dah, inauma sana. Mwenzetu kapitia mateso makubwa ila kaufaham mwisho wake na najua alijinyenyekeza kwa mola wake. Mpaka kupata mda wa kuaga watu ni dhahiri kua ni mtu mwenye bahati sana ya kutubia dhambi zake.
Wengi wanakosa hiyo nafasi kwani mauti yamekua yakiibuka ghafla bila kujiandaa.

Bwana akurehemu na akupe maisha ya milele ya amani.


Inategemea alikuwa wa imani ipi.
 
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى
Iymaan-Taqwa
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور
((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]

Tokea kuumbwa kwa Nabii Aadam عليه السلام hadi leo na mpaka siku ya Qiyaamah hakuna kiumbe kitakachobakia isipokuwa Mwenyewe Mola Mtukufu kama Anavyosema:
كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ
((Kila kitu kitaangamia isipokuwa Yeye)) [Al-Qaswas: 88]

Vile vile Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ))
((وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَام))

((Kila kilioko juu Yake kitatoweka))
((Na Atabakia Mwenyewe Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu)) [Ar-Rahmaan: 26-27]

Baada ya kupulizwa Swuur (baragumu) siku ya Qiyaamah viumbe vyote vitakufa kwa mpangilio Anaoutaka Mwenyewe Allaah سبحانه وتعالى. Kisha mwisho atabakia Malakul Mawt (Malaika mtoaji roho) na Allaah سبحانه وتعالى. Kisha Allaah سبحانه وتعالى Atamuamrisha Malakul Mawt ajitoe roho yake mwenyewe. Atakapokufa Malakul Mawt Atabakia Allaah سبحانه وتعالى Pekee wa Mwanzo na wa Mwisho, Al-Hayyul-Qayyuum (Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo). Allaah سبحانه وتعالى Siku hiyo Atazikusanya ardhi na mbingu katika Mikono Yake,

((وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ))

((Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume)) [Az-Zumar: 67]

Na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنه kwamba:

((يطوي السموات والأرض بيده، ثم يقول: أنا الملك، أنا الجبار، أنا المتكبر، أين ملوك الأرض؟ أين الجبارون؟ أين المتكبرون؟)) مسلم

((Allaah Atazikunja mbingu kwa Mikono Yake, kisha Atasema, Mimi ni Mfalme, Mimi ni Al-Jabbaar (Mwenye Kushurutisha), wako wapi wafalme wa dunia? Wako wapi majabbaar (wanaolazimisha), wako wapi wanaotakabari?)) [Muslim]

Hapo tena Atauliza mara tatu:
((لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ))
((Ufalme ni wa nani leo?)) [Ghaafir:16]

Hakutakuwa na mtu wa kujibu, basi Atajibu Mwenyewe,
((لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّار))

((Ni wa Allaah Mmoja Mtenda Nguvu)) [Ghaafir 16]

Na hapo tena ndipo kila mtu atakuta hesabu yake ya matendo aliyoyatenda duniani ikiwa ni mema au mabaya, hakuna atakayedhulumiwa hata chembe, kwani Allaah سبحانه وتعالى Atahukumu kwa uadilifu baina ya viumbe Vyake. Kila jema Atalilipa kwa mara kumi na kila ovu atahesabiwa mja kwa ovu moja.

((الْيَوْمَ تُجْزَى كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ))

((Leo kila nafsi italipwa kwa iliyochuma. Hapana dhulma leo. Allaah ni Mwepesi wa kuhisabu)) [Ghaafir: 17]
 
Huyu jamaa mbona yuko online ?
Screenshot_20190530-150308.jpg
 
RIP mkuu Folk,hii inaumiza sana sana,hivi mkuu Folk ana mtoto au mzazi ambaye naweza kutoa hata ubani kidogo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom