Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Yupo hapa dar kama unaenda mbweni aende pale au hata mwenge vinyago wote hao Mungu anawatumia, kifo ni siri ya Mungu basi
Hivi huyu jamaa yupogi real kweli, nilishaangaliaga shows zake channel 10 watu wanaponeshwa kwa maombi.
 
Usihofu my young brother. Kila siku "tunakufa' bahati nzuri tunaamka au kwa usahihi zaidi tunaamshwa. Hakuna anayefanya jitihada ya kujiamsha mwenyewe. Kama ni kweli daktari anavyosema, basi "ukifa" utaamshwa tu wakati wake ukifika na wakati ukiwa "umekufa" hutajua kuwa umekufa kama vile wakati umelala. Kama wakristo wanavyoamini, waliokufa huwa wamelala tu.
 
Kama alivyokushauri mkuu TL.Marandu,nami narudia tena,nenda KKKT Kijitinyama kwa Mch. Eliona Kimaro,nenda na imani yako,naamini roho ya mauti itatoweka.
 
Uyo dokta hakufaa kukwambia ivyo sijapenda hajui miiko......kila mtu atakufa najua ivyo ila ni siri kati ya mungu na wewe .....sasa iyo miezi4 ikifika kama hujafa.
Hajui miiko ya kazi sijapenda ila usife moyo mungu ndie ajuae kesho yako
 
Pole sana Folk! Amini na Mtumaini Mungu/Allah! Yeye Anakupenda Atakulinda na Kukuponya!
Alikuleta kwa sababu na atakuchukua atakapo yeye kwa sababu! Usihuzunike! Usiache kumcha yeye na kumshukuru kwa kila pumzi!
Wapo waliokuwa wazima wa afya jana leo hatuko nao! Wewe ni mshindi na Mungu ataendelea kuwa nawe sikuzote hatokuacha!
 
Dah nimekosa cha kusema ila walau wewe utapata muda wa kutubu sie wengine tutakufa hatajui saa wala siku ...
 
Pole sana ndugu. Lakini kumbuka kifo katika Yesu ni usingizi tu. Kwa wale tumwaminio Yesu, tutafufuliwa siku atakaporudi mara ya pili hapa duniani. Na baada ya ufufuo, tutakwenda kuishi naye katika makao ambao anayaandaa kwa ajili yetu kipindi hiki. Kwa hiyo hata kama utaondoka, ondoka katika Yesu. Jikabidhi kwa Yesu. Tumia kipindi cha uhai wako kumjua zaidi Yesu. Zaidi ya yote, umkubali na kumwamini. Anaponya pia.
 
Good news! Nenda katubu vizuri, gawa mali zako kwa masikini na zingatia ibada. Tenda mema siku zote na ukipokee kifo kwa uchaji! God be with u!
 
Ndugu Folk kama una taka maisha yarudi na magonjwa yaishe uwe huru naomba nitafute kwa namba hizi 0753570709 sihitaji hata mia yako ndugu yangu nia yangu upone ufurahie tena makusudi ya Mungu juu yako,thanks kama uta ridhia ndugu...
 
Pole sana ila be strong endelea kumtumai Mungu ye ndo anayejua hatima ya maisha yako.
 
Kama maisha ya mateso ni bora kufa Tuu

Kuliko kupoteza gharama hospital wkt kufa kuko palepale..

Mkuu hii miez mnne ndio ya kula hata, kuiaga DUNIA haswaa hakika ukifika huko hujutiii,kama revenge Fanya sasa,yan umepewa muda wa kumaliza na kufanya kile rohoo inapenda

Mimi binafsi nikiwa na huzun au matatizo watu wanao nipa pole ,huwa wananiongezeaga huzuni Tuu


Mkuu hii miez minne Fanya kitu moyo unaenda

Have a good time
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…