Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Kuna watu watawah kuondoka !! Kuliko hata bro folk kwa hiyo tukumbuke kutubu !! Hapa ulimwenguni tunapita wakuu .. Mi naanza mimi kutubu naamini wengi watanifuata .. Akiwemo jiwe !!
 
kama una imani Mungu yupo jaribu Maombi nenda Tanga majestic hall kuna ministry inaitwa shiloh utarudi ukiwa mzima watu wenye HIV wanapona sembuse ww Mungu atakukuponya
Uponyaji unafanywa bure au mnataka kumpiga kirungu tu huyo kijana?
 
Nimejisikia uchungu sana ndugu yangu nakuombea kwa mungu atende miujiza kwa kuwa yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuponya
 
Hata mi nashangaa huyu daktari mbona kamtamkia mgonjwa straight to the point akijua kabisa Maneno huumba hatakama Hana uhakika
 
Nilishaumwa sana kaka. Maisha yangu yamekuwa ya mateso mno hapa Duniani, Nikapumzike tu.


Pole mkuu!
 
Pole sana Mkuu, hakika Mungu ni mwema na ana makusudi mema na wewe. Kwakua dawa na matibabu zimewekwa na yeye, na hivyo vyote havijafanya kazi, basi ni wakati wa kuomba huruma ya Mungu, ufanye toba ya dhambi zako, uungame zambi kama ni mkatoliki na upakwe mafuta ya wagonjwa. Weka roho yako tayari kumuona Mungu. Siyo kusudi la Mungu tuishi hapa duniani milele, hivyo mshukuru kwa zawadi ya maisha na ujiandae kuonana naye.
 
Hebu mara uisomapo hii comment, haraka sana nipe namba yako inbox nina machache ya kuzungumza na wewe
 
Option uliyobaki nayo ni moja Tu KATAA ROHO YA UMAUTI, Hivyo basi kwa Imani Yako nenda kaombewe na uombe sana kila kilicho negative kiwe positive kuanzia leo.

Amen
 
Kwani dr. Ni mungu ??
Ondoa hayo mawazo ya dr. Jua mungu ndio alie na hatma yako na ndo anajua kakuumbia nn kushinda huyo dr

Usije kufa kwa mawazo bure wakat hauna ttzo lolote dr. Is just human being hawapaswi ku act like gods

Shame on them
 
[emoji23] [emoji1] maaaan...!!
Kwanza pole kwa huo ugonjwa then ulichokosea ni kuuruhusu moyo na akili kukiri kuwa unakufa baada ya miezi 4, watu wapo wana magonjwa ya ajabu lakini wameishi mpaka Leo hii kwa tumaini na Neema za Mungu.

Kuanzia sasa kataa kuwa hutakufa miezi 4, bali utaishi zaidi kuwa na imani kuwa na Amani ni Mungu pekee ndiye anajua na kupanga kuwa umati utakukuta muda gani na wala siyo maneno ya daktari. [emoji4]
 
Dah!
Pole sana ila Mungu yuko nawe.

Swali la kizushi: Kwa wewe mwenye bahati kujua hilo, umejiandaaje?
folk.
 
Pole sana ila nnachoweza kukwambia sisi sote njia yote ni moja.hakuna kati yetu ajuae saa au siku ya ajali yake!wakati we umepewa miezi 4 kuna wanaokusoma humu lakini kesho yake wasiione!.hakuna cha kupigania humu duniani.hatujui nani atatangulia kabla yako
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…