Uwekaji wa jiwe kubwa au dogo, hautengui maamuzi ya mwendazake. Ni vena kufuata maamuzi yake ili kuepusha maafa kwa wale wanaobatilisha maamuzi yake.
Jiwe huwekwa jirani na sanduku baada ya sanduku kupakiwa ndani ya gari, na huondolewa baada ya sanduku kushushwa toka garini. Kazi ya jiwe hili sio kuzuia ajali, bali ni kuiondoa nuksi au mkosi unaofuatana na mwili wa mfu.
Baada ya sanduku kushuswa ndipo jiwe huondolewa toka garini na kudondoshwa chini . Kwa kufanya hivyo, nuksi iliyofuatana na sanduku huondoka ndani gari pamoja na jiwe. Hivyo, gari litakuwa salama.
Hujawahi ona gari lililotoka kusafirisha maiti linapata ajali wakati linarudi toka safari?.
" Kalaga bahho."