Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Wewe umezowea filamu za van Damme,utapendaje filamu za wanyama!?..hawajatengeneza kukulenga wewe
JokaKuu amezingua sana. Royal tour ingekuwa Kwa ajili ya wabongo si ingezinduliwa hapahapa Tanzania? Ililenga kutangaza vivutio vya nchi yetu nje ya mipaka ya Tanzania, na huko nje hivo vitu kwenye hiyo filamu ni vigeni kwao. MATAGA waache kudandia vitu visivyowahusu
 
Reactions: Tui
Tangu nizaliwe ninaishi pwani ya bahari na ziwa sijawahi kuona mwanamke anavua samaki kwenye mtumbwi au ndoano labda akina mama wanaovua vidagaa kando ya ziwa au bahari kwa kutumia kanga, tuwe wakweli tusilete siasa za vyama kwani filamu hiyo si kwa wanaccm au wasio wanaccm japo wamaccm tayari wanadalili ya kuidandia.
 
Hiyo 7b ilitumika kuandaa hiyo filamu, baada ya hapo huu uzinduzi wa rais kukaa ughaibuni na akina magulu ya chemba, tabasamu & co nk nk, itagharimu kiasi gani maana Hadi Sasa wanakula Bata la uzinduzi huko US.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Washarudi hawa jamaa au wameamua kubaki huko huko.
 

Umenikumbusha kitabu cha An enemy of the people ambapo ilikua inafikia wananchi wanaambiwa kiongozi anaenda kuwapigania ulaya kumbe kaenda kuhudhuria sherehe za wapenzi wake
 
Sasa kama ni hivyo mkuu mbona kwenda kuizindua USA hawajatumia gharama zao kusafirisha msafara wa Rais badala yake zinatumika kodi za watanzania?
 
Mkuu kwa hiyo filamu ku base tu Kaskazini ni sawa?

Dah!! Hivi unajua tuna Mbuga nyingine kubwa mbili kuizidi Serengeti?
Hii filamu imeonesha mbuga zote na kila kivutio kilichopo nchini. Sema tu kama ilivyo ada vijana wa kitanzania mara nyingi huwa tayari kutumiwa na maadui dhidi ya nchi yao wenyewe kupitia kigezo cha utofauti wa kisiasa. Nchi kama Israel, New Zealand, Rwanda nk zimesharekodi filamu hizi za Royal Tour kwa mtindo huu huu. Lakini kwa vile vijana wao wana mioyo ya utaifa, uzalendo, elimu na akili, basi ilikuwa ngumu maadui wa nchi hizo kuwatumia vijana wa mataifa hayo kuandika propaganda za ushuzi kama hizi tunazoshuhudia kwa vijana wetu. Nimeamini ni kwann mwl Nyerere alikataa siasa ya vyama vingi, maana aliwaelewa tosha vijana wa kitanzania walivyo mbumbumbu katika kuchanganua mambo, na kwamba ni rahisi sana wao kuhadaika na pengine kupelekea kuiingiza nchi yao wenyew machafukoni kwa faida ya walio/wanaowatuma. Maadui wa taifa mara nyingi wamekuwa wakipitisha ajenda zao kimya kimya kupitia huu unaoitwa uhuru wa kutoa maoni, wanasiasa uchwara nk.
 
mkuu, kwani watalii wanaoitembelea kenya hawaruhusiwi kuja Tanzania? hao watalii kutoka kenya wakifika tz, watalipia kuangalia vivutio vyetu, by the way... wametafutwa na wakenya kwa juhudi zao, na bado na sisi tumefaidika nao...hata kenya nao wana vivutio vya utalii kama mbuga ya tsavo e.t.c.. sasa kama mtalii kashamaliza kutalii kenya..anataka kupanda mlima kilimanjaro kuna kosa? ( na akipanda atalipia) tunawalaumu tu wakenya bure, hata wakisema mlima kilimanjaro uko kenya...bado huyo mtalii hawezi kupandia kenya hakuna njia...atakuja tu tanzania na kulipia $ na nchi itafaidika.
 
Mkuu sikupingi ila nakuomba fanya kautafiti kadogo, ongea na wadau hasa wa utalii as tour guide, tour operators nk, waulize kuhusu hii sinema nje ya matokeo.

NOTE: Uliza kuhusu hiyo sinema na siyo matokeo ya sinema please. Alafu njoo tujadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…