Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Mwenzio kapewa tapishi hili na mabwanyenye ya nchi jirani, ambayo yalitaka dunia iendelee kuamini kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya na ziwa Nyasa ni la Malawi. Hii film inakwenda kuwaumbua na kuwalaza njaa mabwanyenye wote. Maana dunia itaelewa ukweli kuhusu mmiliki halisi wa mlima Kilimanjaro, ziwa Nyasa nk. Hongera raisi wetu Samia.
Umemjibu vizuri.Na sisi wananchi wakawaida,unatufahamisha,na tunafahamu vizuri sasa.
 
Hivi Kuna rais yeyote duniani aliyeko madarakani anafanya kama anayofanya Samia ya kuacha shughuli za kitaifa na kuwa busy na filamu?
Bora muda huu tungepata kiongozi mwingine tuu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Ila kumbuka mtalii mmoja akija atapanda tax atalala hotel atanunua vinyago na dada yako atapata bwana.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , hii filamu ni yao, walituomba watutengenezee, tukakubali, wametumia gharama zao, na sasa baada ya uzinduzi, wataendelea na biashara yao kurudisha gharama zao, huku sisi tukifaidika kutangaziwa utalii wetu bure bure.

Tena mbele ya safari, in future, mnaweza kuja kuwa surprised kukuta hata the main character, alilipwa tuu kama ma starring wengine wote wa movies nyingine zote!, the only difference, zile nyingine ni fiction movies, this is non fiction.

P
Nani atakuwa anafanya analysis ya kile walichokipata dhidi ya kile tulichokipata au tunaamini tu kuwa sisi ndio tutakao faidika zaidi!!? Haka kamchezo natamani CAG Akachambue unataka kutwambia jamaa wamelipia na gharama ya bi mkubwa kwenda kuifungua kwa wiki mbili USA na cost ya muda na rasilimali za taifa kushoot kama helicopter ya jeshi na muda wa mtumishi namba moja wa umma

Naona tumecopy kwa Kagame na kufanya modification za kutosha... Very disappointing
 
Na wao pia nasikia wanatoa filamu yao inayoonyesha Mlima Kilimanjaro na serengeti zipo kwao...Filamu inaitwa the Tour Guide
Siku zote aliekutangulia ndio mkubwa. Wao wakitoa mlima Kilimanjaro baada ya sisi dunia itatambua kuwa wame copy kwetu.
 
Huyo bi mkubwa namshangaa sana, vitu vimepanda Bei na Wala hana hata mpango navyo, mambo aliyotakiwa kufanya waziri wa utalii anafanya yeye, nchi za nje Kuna mabalozi Kila nchi ambapo wanaweza kufanya kazi izo anazokwenda yy lkn bado anaend mwenyew nazn tunachekwa Sana uko nje, wazungu washenzi Sana wanampa mama kichwa huku wanampoteza mwishowe wanatamuacha peke yake pakiwa pameshaharibika, ndo watanzania tulivyo.
Fanyakazi acha uvivu.Duniani vitu kupanda ni jambo la kawaida.Babu zetu wakinunua kilo ya nyama sent tano miaka ya 1847, ulipozaliwa wewe ukakuta ni 5000, ikawa inapanda inapanda,kulingana na wakati.Hata dala dala enzi za miaka ya 70,ilikuwa shilingi 5,mpaka unazaliwa wewe umekuta ni 200 na sasa 400.Bei hazibaki hizo hizo,miaka,bei zinabadikika.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Umemjibu vizuri.Na sisi wananchi wakawaida,unatufahamisha,na tunafahamu vizuri sasa.
Jamaa alijua kila mtu anaweza kushikiwa akili kama alivyoshikiwa yeye na mabwanyenye wake. Tunajua fika kuwa maadui zetu wanatumia nguvu kubwa, na pesa nyingi kuwarubuni hawa vijana ili waje waharibu sifa za filam na nchi kwa ujumla kwa lengo la kuwavunja nguvu wengine. Lakini sisi wenye uchungu na taifa hili kamwe hatuwezi kuwaacha hawa chawa watambe au wachafue chochote.
 
Umesema kweli,sisi wananchi,sasa tumeelewa kwa nini,wanaumia kuhusu hii filam,kumbe walikuwa wanajitangazia vivutio vya Tanzania ni vya nchi nyingine.
Ndio mkuu, hii filam imeenda kuifanya dunia ielewe kila kitu kuhusu Tanzania na watanzania. So maadui wana wasi wasi wa kupoteza watalii.
 
Filamu nyingi kuhusu Tanzania ukiziangalia hakuna jipya utaona, ila mambo unayoona ya kawaida kuna watu wengi watashangaa sana tu.

Kwa kifupi, you are not the target.
 
Hii filamu imeonesha mbuga zote na kila kivutio kilichopo nchini. Sema tu kama ilivyo ada vijana wa kitanzania mara nyingi huwa tayari kutumiwa na maadui dhidi ya nchi yao wenyewe kupitia kigezo cha utofauti wa kisiasa. Nchi kama Israel, New Zealand, Rwanda nk zimesharekodi filamu hizi za Royal Tour kwa mtindo huu huu. Lakini kwa vile vijana wao wana mioyo ya utaifa, uzalendo, elimu na akili, basi ilikuwa ngumu maadui wa nchi hizo kuwatumia vijana wa mataifa hayo kuandika propaganda za ushuzi kama hizi tunazoshuhudia kwa vijana wetu. Nimeamini ni kwann mwl Nyerere alikataa siasa ya vyama vingi, maana aliwaelewa tosha vijana wa kitanzania walivyo mbumbumbu katika kuchanganua mambo, na kwamba ni rahisi sana wao kuhadaika na pengine kupelekea kuiingiza nchi yao wenyew machafukoni kwa faida ya walio/wanaowatuma. Maadui wa taifa mara nyingi wamekuwa wakipitisha ajenda zao kimya kimya kupitia huu unaoitwa uhuru wa kutoa maoni, wanasiasa uchwara nk.
Acha utani bwana wewe! Yaani rais wa Israeli alikaa marekani zaidi ya nusu mwezi! Hata wa Rwanda hakukaa hivyo.
 
nafikiri Tusubiri muda Ndio utaleta jibu sahihi kuliko kutoa maamuzi sasahivi
 
Hivi Kuna rais yeyote duniani aliyeko madarakani anafanya kama anayofanya Samia ya kuacha shughuli za kitaifa na kuwa busy na filamu?
Bora muda huu tungepata kiongozi mwingine tuu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Kwa vile unaishi mwanalumango mambo kama haya ya maraisi au viongozi wa serikali kuacha shughuli zao kwa ajili ya filamu hauwezi kuyajua. Wewe umeshazoea mtu aje akushike masikio akwambie andika hivi na ww uandike bila hata kutumia japo robo tu ya akili yako uliyojaaliwa na mola wako. Hao chini ni baadhi tu ya hao walioacha shughuli zao kwa ajili ya filamu. Na kwa vile nchi hizo hazina vilaza wa aina hii ya baadhi ya watanzania basi hakuna raia wao waliowalaumu au kuwaattack kwa walichokifanya. Maana waliamini kuwa filamu hizo ni moja kati ya shughuli za nchi ambazo raisi au kiongozi anapaswa kuzifanya kwa taifa lake. We endelea kuaminishwa na kuamini kwamba hakuna raisi alieacha shughuli za kitaifa na kuwa busy na film. Najua akili haichanganui, lkn sidhani kuwa hata macho yako nayo hayaoni.

images (65).jpeg


images (64).jpeg


39876622880_75ab92ae28_b.jpg
 
Tuangalie gharama za hiyo tour, na uhalisia...
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , hii filamu ni yao, walituomba watutengenezee, tukakubali, wametumia gharama zao, na sasa baada ya uzinduzi, wataendelea na biashara yao kurudisha gharama zao, huku sisi tukifaidika kutangaziwa utalii wetu bure bure.

Tena mbele ya safari, in future, mnaweza kuja kuwa surprised kukuta hata the main character, alilipwa tuu kama ma starring wengine wote wa movies nyingine zote!, the only difference, zile nyingine ni fiction movies, this is non fiction.

P
Kila nikijaribu kutype maoni yangu mkono unakuwa mzitoooooooo! Acha ibaki Ivo.
 
Back
Top Bottom