habari za asubuhi Jf people?
Mimi ni Dalali wa Viwanja Magari Nyumba & Co. Kuna pesa huwa naipata gjafla kutokana na shughuli zangu za u middle Nimeamua kuanza kukopesha.
watu ninaoanza nao ni waaminifu sana nawafahamu.
Kwa kuanza tu nimeamua kuwapa mkopo wa masharti haya
Kwa kila shilingi elfu 10, irejeshe Sh 500 kila siku.
Mkopo utakaa siku 14.
Jana nimetoa elfu 40, after two weeks ilete Riba ya Tshs 28,000
Je nipo sahihi au najiumiza kwa kiwango nilichoweka?
Je nikipandisha kwa kila elfu 10 izae buku kila siku nitakosea?
Note: mteja wangu ni mama ntilie
Habari
Unawazo zuri la biashara, ila kama mtaalamu wa haya mambo inaonekana hii biashara sio endelevu na haitachukua mda utuifunga kwasababu ya kuishiwa au kupoteza Mtaji au gawio.
"Unatakiwa kuachana na hii biashara kwanza kama ukiweza paka utapo pata majibu ya haya maswali"
1. Nakopesa watu waaminifu. Je, nitatumia kipimo gani kujua nani ni mwaminifu?
Suggestions:-
Hapa unaweza tengeneza form ambayo wahusika watajaza majina ya watu ambao watakuwa "
Wadhamana wa tabia njema" au unaweza sema "
Character referee".
Hakikisha referee wote sio ndugu wa waombaji. Hii ni kwasababu kama ni ndugu wanaweza kusema uwongo ili tu kusaidia ndugu yake kupata pesa.
Pili unatakiwa kujiuliza, Kwa nini huyu mtu ameandikwa kama referee? Je kuna faida yeyote ya referee atapata kupitia mwombaji kupata mkopo? Kwa nini amendikwa kuwa referee?
2. Ninakopesa pesa bila dhamana. Je, ikatokea mtu akashindwa kulipa au akaamua kutokulipa, nini nitafanya kupata pesa yangu?
Suggestions:-
a/Hapa unaweza kwenda polisi, lakini inaweza kuwa mda utao poteza na gharama nyingine za mahakamani zinaweza kuwa kubwa kuliko mkopo. Hii inaweza kuwa sio option nzuri
b/ Unaweza tumia Insurance. Ila kwa sababu unafanya vitu "casual" au sio rasmi sidhani kama watakubali kukupa insurance. Hii inaweza kuwa sio option. Ila unaweza kufuatilia kwa uzaidi.
Jaribu kujibu hayo maswali hapo Juu.
Je biashara inatija?
Kama unatoa Tshs40,000/= na unategemea kupata Tshs 28,000 baada ya wiki mbili. Hii inamaana utapata faida 70%(Tshs 28k/Tshs 4k). Lakini, upande wa pili una risk ya kupoteza 100% au Tshs 40,000.
Watu wa Bank, wanatoza riba ya 6% paka 15% kwa mwaka. Hii unaweza kusema ni kati ya 0.0023% paka 0.0057% kwa week mbili.
Wakati wenzako wanatoza riba ya chini ya 1% kwa mda wa wiki mbili, wewe unatengeneza asiliamia 70.Kwa haraka unaweza kuona
"red flag"
Utapata faida Kubwa, kwasababu umekubali au upo tayari kupata
hasara kubwa. Hii ni tabia mbaya kwenye maswala ya fedha.
Hii inamaana leo unaweza kupata faida, na kesho ukapoteza pesa yote.
Asante.