Nimechoka na matusi ya huyu kaka yangu mwenyewe Miaka zaidi ya 40

Nimechoka na matusi ya huyu kaka yangu mwenyewe Miaka zaidi ya 40

Jamani mpk naandika huu uzi hatujalala tunakesha kila siku

Kimsingi huyu ni kaka yangu mkubwa kabisaa wa mwaka 84 tumeshare mama.. Yeye ni mkandarasi.sijajua tatizo ni bangi ama amerogwa.. maana bangi ni chakula kwake na mapombe

Huyu ndugu yangu atakuja kumuua mama yangu na presha kama sio kumchoma kisu.. tumeshaongea nae sana mpk polisi kupelekana lakini Hakuna alichobadilika

Yupo nyumbani tangu mwaka 2023 na hataki kuondoka tena.. alirudi home akiwa hoi kwa kupigwa huko nnje kwa ujeuri wake,, sura imejaa alama za kutosha

Wakuu majirani wapangaji wetu hawana amani, amekuwa akiwatishia kuwakata mapanga na kuwatukana matusi ya nguoni.. anafanya fujo mtaani anatukana kila mtu. Anaweza kuvuta bangi hata ndani na Hakuna wa kumfanya kitu

Kinachoniuma zaidii anamtukana sana mama yaani matusi kabisaa ya nguoni tena akiwa nnje mpk majirani wanasikia
Hii hali namuona kabisaa mama anaumia
Mama yetu mwenyewe umri umeenda yuko na 62

Sasa nauliza tu kama nitaenda kumfungulia mashtaka polisi awekwe hata jera nitakuwa nafanya vibaya???
Huyu mtu anatembea na mapanga barabarani naogopa kuna siku anaweza kutuchinja

Na Kama Kuna mtu ameshawahi kukumbana na janga Kama hili kwenye familia au majirani walitumia njia gani kupambana na mtu kama huyu
Ni mkandarasi au fundi ujenzi?
 
Nakubaliana na wewe poti nimeshuhudia kesi nyingi za aina hii akina mama wanawabeba hao watoto wao wasumbufu.

Na hii bond ni ya tangu utotoni. Akikosea anaadhibiwa na baba lakini mama anamvuta jikoni kumlambisha mchuzi na kipolo cha wali. Ubaya mara nyingi baba anatangulia kufa mtoto anarudi kumsumbua mama yake aliyemtengeneza kuwa wa hovyo. Akibaki na baba anafukwa kwa neno moja tu.
Aisee ndio hivyo mtusamehe tuna mioyo ya huruma tu
 
Ni mkandarasi au fundi ujenzi?
Sio fundi ujenzi…. Anaendesha yale magari ya kujenga barabarani sijui yanaitwaje ila ndio kazi yake now wanajenga hizi barabarani za mwendokasi
 
Mpeleleni hospitali au rehab. Kuna hospitali nzuri sana iko Mbulu, Hydom. Mkiweza kumpeleka huko, itamsaidia sana. Bangi hizo zimeshamuharibu akili. Na bangi nyingi siku hizi wanachanganya vitu including unga, inakuwa balaa.
 
Usikute huyo alisharogwa na wenzake, binadamu tuna wivu wa kijinga sana haswa kwa wasio na elimu
Inawezekana maana ni mtu mwenye ana sijui akili sijui uelewe mzuri… maana Hakuna sehemu anaomba kazi akakosa kwaiyo fani yake Tatizo lake ni mkorofi wanamchoka wanamuachisha na anapata sehemu nyinginee

Ila hela zake zinaishia kwenye Mapombe na mabangi
Imagine siku ya jana alikuwa na 1m lakini kabebwa na polisi anatoa laki 2 tumuhifadhie kaenda kununua mavitu hayana maaana

Ana kazi nzuri mshahara mzuri ila hana maendeleo yoyote kaishiaga kununua kiwanja tu Miaka na miaka
 
Mama ni mtu anaesita ni kama anataka mara hataki… mimi nilichotaka kufanya kama hili linawezekana atolewe nyumbani yaani apewe onyo kukanyaga nyumbni sasa sijui kama hiyo kazi polisi wanaifanya
Hawataifanya. Zaidi ya hospitali hakuna tiba nyingine. Vijana wakifika hapo huwa ni kasheshe kubwa kwenye familia.
 
Mpeleleni hospitali au rehab. Kuna hospitali nzuri sana iko Mbulu, Hydom. Mkiweza kumpeleka huko, itamsaidia sana. Bangi hizo zimeshamuharibu akili. Na bangi nyingi siku hizi wanachanganya vitu including unga, inakuwa balaa.
Ngoja tuone kwanza kama watafikishana mahakamani
 
Hospital tunampelekaje mkuu.. unavyoona hapa tumetoka polisi na sungusungu ila ameachiwa wanasema hawawezi kulaza vichaa maana mara ya mwisho alitaka kujinyonga huko lockup
Mnatumia polisi au watu at least wawili wenye nguvu, wanampeleka. Akiwa kule, watamchoma sindano za kumtuliza, huku anapewa drips za kutoa sumu. Hapo pia nyinyi mtakuwa na amani nyumbani, kujua yuko sehemu salama na anapata tiba.
 
Mnatumia polisi au watu at least wawili wenye nguvu, wanampeleka. Akiwa kule, watamchoma sindano za kumtuliza, huku anapewa drips za kutoa sumu. Hapo pia nyinyi mtakuwa na amani nyumbani, kujua yuko sehemu salama na anapata tiba.
Si nimesikia wanalipia hivo vituo
 
Ninachoweza kusema huyo ni mtoto wa mama na huenda mpaka anafika hapo mama amechangia.

Ukifuatilia watoto wa kiume wengi wasumbufu ni wale mama's boys. Na pindi baba alipokuwa anachukua hatua dhidi yake ili kuweka sawa anapokosea mama alimkumbatia. Na kama sivyo alilelewa bila baba.

Ukimfungulia mashtaka atakayeumia ni mama yako. Akitupwa rumande kwa onyo mama ataenda kumtoa. Kaa na mama uone hilo kama litamfurahisha usijegeuka adui wa wote.
Huu ni ukweli mtupu
 
Huyo atakua hiyo tabia ni ya kurithi itakua kwenye ukoo wao lazima kuna tabia kama hiyo, utakuta Baba akizaa watoto kuna mmoja hiyo tabia itamkamata tu sasa kwenye ukoo wao itakua yeye ili pepo limemshika yeye.
Sijajua kwa upande wa kwao mkuu
 
Sasa kwanini msifukuze aende kwao kwasababu hapo siyo kwao.
Unafikiri ni rahisi hivyo anakwambia hatoki pale labda mama ake afe ila hatoki… kwanza anasema akitoka wataenda kumuua mtaani si anajua Watu wanamjua kupitia mama sasa akienda kupanga huko watamuua
 
Poleni Kwa tatizo..Kuna mama alikuwa Na kijana Wa pekee aliyekuwa naishi naye ..mama alikuwa Dr PHD alikuwa anaishi sinza mwaka 2022 kijana wake alikuwa Na tabia kama za kaka yako

Kutokana Na Upendo Wa mama Kwa mtoto akawa anamkingia kifua

Huwezi Amini hiyo kijana alimuua mama yake

Mwingine alikuwa Ni bangi bangi...alikuwa anaishi Pugu kajiungeni alimuua mke wake aliyekuwa anafanya kazi NMB naye alikuwa bangi bangi..kisa hicho kimetokea mwaka Jana 2024

Chukueni hatua au mjiandae kitu kibaya ndani YA familia
Ndio tumempeleka polisi
 
Back
Top Bottom