Nimechoka na matusi ya huyu kaka yangu mwenyewe Miaka zaidi ya 40

Watu washapeleka kesi sana serikali za mtaa kaitwa na wajumbe mpk siku ya jana anamtukana mama mbele ya wajumbe ana mdhalilisha wajumbe wakasema mama achukue hatua huyo alipofikia sio wa kusikiliza ushaurii tena
 
Hana mke?
Watoto je?
Maana angekua na kazi ya maana sinzani kama angekua na huo muda wa kushika ayo mapanga
Nishayaeleza hayo

Unafkiri mtu mwenye tabia kama zake anaweza kuishi na familia
 
Muache kwanza Hadi amjerui mama Yako na panga ndio Muta pata maamuzi ya kiume. Kwenye tatizo Akili inaongezeka
 
Watu washapeleka kesi sana serikali za mtaa kaitwa na wajumbe mpk siku ya jana anamtukana mama mbele ya wajumbe ana mdhalilisha wajumbe wakasema mama achukue hatua huyo alipofikia sio wa kusikiliza ushaurii tena
Haya nendeni polisi mkafungue faili
 
Nishayaeleza hayo

Unafkiri mtu mwenye tabia kama zake anaweza kuishi na familia
Nenda polisi ukamshtaki atawekwa lockup ataonywa akiendelea anafungwa akapumzike jela kidogo hio ndio step ya mwisho ukizembea ukasema hatujakuelekeza basi endeleeni na matatizo yenu, nenda polisi waje wamchukue alale selo kidogo hata miezi 6 akirudi akili itakua imemkaa sawa
 
Nishayaeleza hayo

Unafkiri mtu mwenye tabia kama zake anaweza kuishi na familia
Wahi polisi sasa hivi vituo vipo wazi waje wamchukue atawaua kweli km mpaka mjumbe anamvimbia huyo hafai akalale selo na wakorofi wenzie huko wakampasulie mayai
 
Yule kaka aliyemdunda akapoa anahitajika. Mpeni kandarasi ya kumdunda huyo mkandarasi maradufu tena ikiwezekana kila baada ya miezi miwili kwa sababu mmeshajaribu kila kitu kimeshindikana kasaoro kipondo
 
Daah ndio hivyo mkuu… jana kakamatwa tunasubiri maelekezo
 
Asee kibao kimegeuka eti malezi ya mama! Natamani niingie kwny ubongo zenu nijue unavyofanya kazi
 
Asee kibao kimegeuka eti malezi ya mama! Natamani niingie kwny ubongo zenu nijue unavyofanya kazi
Ukiamua kuelewa ni jambo zuri ila ubongo wako ukigoma ni vizuri pia

Hivi unajua upendo wa baba uliozidi kwa mtoto wake wa kiume ndio huwa unatengeneza uadui kati yao?
 
Aisee ndio hivyo mtusamehe tuna mioyo ya huruma tu
Cheza kwa akili unaposhughulika na huyo bro ili usijekosana na mama hata kama lengo lako ni zuri. Hata ukisema apelekwe sober house bado mama anaweza kataa. Ni mpaka hali iwe mbaya sana.

Na mkisema aondoke nyumbani mama yenu atawalaumu mnamtenga kaka yenu kwa kuwa hapo sio kwao. Cheza na mama ndio awe anatoa suluhu ya kushughulika na mtoto wewe msaidie mawazo na njia za kuweka mambo sawa
 
Kwa hiyo we dogo unajikuta mjanja kuja kuniandikia huku au sio ? Ngoja nirudi nyumbani utanitambua .
 
Nipe hits mkuu maana huyu wa kwetu amelala stakshari hapa tunasikilizia mama atafanya kweli au anatuchora tu… maana yeye ndio anakuwa mshtaki
poleni sana ,....
 
Tatizo ni mama. Miaka 62 mbona bado sana. Kama mama hamtaki, anaweza kumuondoa vizuri tu. Lakini inaonekana ni kipenzi cha maza. Wazazi wanaharibu sana watoto​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…