Nimedokezwa: MOU 30 alizosaini Rais Dubai zikiwekwa hadharani, waTanganyika wote tutalala uchi barabarani

hata ufiche wee kuna siku litafichuka tu. Mungu yupo.
 
Nini tofauti ya Agreement na mkataba?
Agreement ni makubaliano kwa kiswahili. Pia limetumika neno 'azimio' la makubaliano wakati suala la DP World linakwenda bungeni. Makubaliano yaliyofikiwa bungeni ndio yanayokwenda kutengeneza mikataba ya kibiashara.

Mkataba ni kile kinachozaliwa kutokana na makubaliano mara nyingi huwa ya mdomo. Katika kutunza kumbukumbu ndio pande mbili huandikiana yale wanayotaka yaongoze ufanyaji biashara yao.
 
Mkuu @paschalmayala una andiko lolote kuhusu hizi hekaheka za DP World?Naomba link kama umeandika
 
Endeleeni kusubiri hayo majibu
 
Mi nadhani napia sinauzoefu sana kuhusu hiyo mikataba kwa mna Dhani tatizo lilitokea wapi mpaka kufikika makubaliano ya kukabidhiana hizo lasilimali za in inchi pengine watu walijisahau wakaupiga mwingi wakamsahau mwenyewe jamani mina pitatu
 
Sijauliza ‘tafsiri’ ya neno ‘agreement’ , bali nimeomba tofauti ya maana ya neno ‘agreement’ na neno ‘mkataba’ , tofauti za hayo maneno mawili ni nini?

Kwamba mkataba huzaliwa baada ya makubaliano, na makubaliano huzaliwa baada ya nini? Yaani onyesha tofauti kwa criteria moja kwa maneno yote mawili
 
Sgr , tanesco ,ttcl
 
Hizo ni picha tuuu , uhalisia inakuwa zero
 
Agreement ni kile kilichokwenda bungeni na ni summary ya lengo zima la mikataba inayokwenda kusainiwa kati ya wazalendo na hao DPW.

Makubaliano ya DPW kati ya wanasheria wao na hawa wa kwetu yamechukua mwaka mzima kuweza kuandikwa.

Huwezi kuweka kila kitu kwenye makubaliano unachofanya ni kufupisha lengo zima la uwekezaji na huko kwenye mikataba ndio unakwenda kuweka kila kitu na mjadala wa kuandika mkataba unakuwa mrefu kuliko huo wa kupitisha azimio ndani ya bunge kwani huko ndio inakuwepo hatima nzima ya uchumi wa nchi kwa miaka mingi ijayo.

Huko ndiko kwenye ukomo, wanaosema mkataba hauna ukomo wanamaanisha makubaliano bila ya kujua, wanachokilenga ni hiyo mikataba ya kibiashara yenye ukomo kutegemea aina ya biashara zinazokwenda kufanyika.
 
Kipi hasa kinafanya kilichopelekwa bungeni kiwe ‘Makubaliano’ , na hicho kinachokuja kuwa ‘mkataba’? What are the distinctive criteria between the two?

- Kwamba mkataba ukiandikwa kwa kifupi unabadilika na kuwa makubaliano?

- Kwamba mkataba ukichukua mwaka mzima kuandikwa unabadilika na kuwa makubaliano?

- Kwamba mkataba ukiwa haujawekwa kila kitu unabadilika na kuwa makubaliano?

- Kwamba mkataba wa pili ukiandikwa baada ya wa kwanza, ale wa kwanza unabadilika na kiwa makubaliano?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…