Nimedokezwa: MOU 30 alizosaini Rais Dubai zikiwekwa hadharani, waTanganyika wote tutalala uchi barabarani

Nimedokezwa: MOU 30 alizosaini Rais Dubai zikiwekwa hadharani, waTanganyika wote tutalala uchi barabarani

Kunataarifa zindai kwamba kuna hati za maelewano zipatazo 30 zilisainiwa na Rais katika ziara yake ya Dubai.

Pia inadaiwa, huu mkataba wa Bandari ni moja tu kati ya vilivyomo kwenye maelewano hayo. Pia kuna sekta zingine kama posta nk.

Inasemekana kwamba, MOU hizo zote zikiwekwa wazi, basi waTanganyika wote mtalala uchi barabarani mkigalagala na kulia.

Ombi, MOU hizo zote 30 alizosaini, ziwekwe wazi.
Jamaa waliweka picha ya Rais na bendera ya Tanzania kwenye lile li mnara.....rukashangiliaaaa
 
Ni nchi moja imejaa washenzi wa kila aina. Kuna hawa wanaomfanyia fitina Rais SSH wakisahau kuwa malipo ya dhambi ya ubaguzi yapo hapa hapa chini ya jua, hausubiriwi ufe ndio ukutane na adhabu.
Subiri hayo "malipo" yanamhusu nani!
Sasa umekuwa mtu wa kujiandikia tu lolote linalopita akilini mwako?
 
Kilichobaki ni kumuibia Muarabu mpaka awaambie CCM nimekoma kuwekeza, Hivi hajui tukienda Sumbawanga kwa wazee tunaweza kuiba mpaka Meli? Hawatujui hawa ngoja wakutane na Vibaka wazoefu waone kama watafikia hata lengo moja.
Kwa dhahabu na almasi wanazovushiwa na wazalendo naona itakuchukua miaka 100 kuwafilisi

Kila ukiiba wanapiga x1000
Huo wizi wenu wa diesel na mifuko ya cement unaona ni wizi mkubwa sana eti

Watu wanapata mgao 2b kwa dili
Yaani huwa nasema mwisho wa Dunia ufike tu au hayo mabomu ya nuclear walipue tu waanze Alif
 
EEeeenHeeeee Heeee!
Ni wewe kweli au huyu ni 'Steven Joel Ntamusana' mwingine, na siyo yule aliyekuwa akijigamba na wanasheria wa maPhD!

Kule kupotosha ulikokuwa unajitahidi sana kukufanya humu jamvini hukukumbuki tena?

sasa umegeuka na kuwa mtu wa kulilia pembeni kama yatima?
Muda sio mrefu utaona mikataba ya kibiashara ikisainiwa na suala hili kumalizika kabisa. Hakuna kitu serikali itataka kufanya halafu ikashindwa kufanikisha nia yake.

Samia kaamua kutumia njia ya demokrasia njia ya kistaarabu vinginevyo angekuwa JPM suala hili kitambo keshalimaliza, usingemsikia Mwabukusi au kima mwingine yoyote akifungua mdomo wake.

Nasikitikia madhara ya nguvu kubwa wanayotumia wapinzani wa awamu ya sita katika kujaribu kuja kufanikisha malengo yao ya baadae, inaweza ikavunja nchi yenye miaka karibu 60 kwa sababu ya siasa zao za chuki badala ya kujikita kwenye mantiki nzima ya hoja.
 
Daah, hatari, ila..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

Tanganyika wazanzibar wanachukua Mali yetu kisa Cha muwekezaji jamani.
WHY WHY BANDARI ZA ZANZIBAR No. KUWA FAIDA WACHUKUE WAO TU YOTE HATA TANGANYIKA ISIPATE FAIDA YA 0TZS. HUKU MASIKINI WAKIUMIZWA NA KODI YA MIAMALA NA KILA SEHEMU IMEJAA KODI WHY HUYO ASEMEHEWE KODI HAMUONI KUWA HAO JAMAA WANAJILIPA KWENYE BANDARI KAMA WENGINE WALIVYOKWISHAJILIPA KWENYE UMEME, GESI NA MAFUTA WAO TU NDIO MADILA BASI PAMOJA NA SUKARI.

WATU MMELALA SIJUI MTAJUJA KUWAAMBIAJE WAJUKUU ZENU WATAKAPOKUWA HAWANA PA KWENDA NA KUTUMIKISHWA KAMA PUNDA NA HUKU WEWE UMESHIBA LEO PEKEE.

JAMANI ACHENI UOGA KIZAZI CHA AKINA NYERERE WALITESEKA SIE TUWE HURU WHY SIE TUNAKUWA WAOGA NA ASKARI ANAGANYA KAZI KAMA ROBOTI ANAUA MTU ANAYETETEA TAIFA KISA CHA AJIRA YAKE AMBAYO KWANZA INAMFANYA AWE MASIKINI.
ANGALIENI NCHI YETU IMESHAUZWA IMEISHA PORI TENGEFU, MADINI YAMEISHA YOTE WANAWAPA WATU KWA GAWIO LA SIRI KIVYAO NA SIO LA SERIKALI.

BAADAYE UNAKAMULIWA KODI MPAKA VIMA YAISHE.

YAANI HUJIULIZI UNALIPWA SALARY KODI, UKITOA HELA BANK KODI, UKIITUMA KODI, UKIITOA ULIYOTUMIWA KODI, UKINUNUA KITU KODI , YAANI KUNA KODI NYINGI MNO UNALIWA MPAKA UNAKUJA KUIPATA HELA YAKO.
HUKU WATU WAKIWAPA MA EX WAO GARI ZA 500M.
Hayo yote uliyohoji hayawezi kuandikwa kwenye makubalino yaliyopitishwa bungeni. Kule Dodoma ilipitishwa framework ya biashara itakayovyukiwa au kwa lugha nyingine ilipitishwa SKELETON tu ya namna mtu atakavyokuwa.

Huku kwenye kupitisha mikataba ya kibiashara ndio yote hayo uliyohoji yanakwenda kupitishwa baada ya mijadala ya kina kati ya mwekezaji na mzalendo.
 
Fitna kajifanyia yeye mwenyewe kwa kukubali kuvaa kiatu ambacho kwake ni over-size...watanzania hawako tayari kuuzwa kwa waarabu...
Mimi mtanzania kama wewe na siuzwi kwa mwarabu yoyote na sitokuja kuuzwa kwa mtu yoyote.

Huu uanaharakati hauna tija iwapo mwisho wa siku bandari inaingiza pato dogo kuliko uwezo wake halisi.

Kagame alitucheka enzi za JK namna tunavyoshindwa kuitumia rasilimali ya bahari yenye bandari iliyo katika nchi yenye bahati ya kijiografia.

Hata huko kaburini Nyerere anatucheka tukiwa tumejaaliwa rasilimali za kila aina na mpaka leo miaka 24 baada ya kifo chake tumenasa kwenye mijadala na siasa za maongezi za JF.
 
Subiri hayo "malipo" yanamhusu nani!
Sasa umekuwa mtu wa kujiandikia tu lolote linalopita akilini mwako?
Malipo yanawahusu wote tunao ibua hoja za uzanzibari kwa nia ya kumnyanyapaa Rais na mawaziri wanaotoka huko Unguja na Pemba.

Maneno ya Mwalimu Nyerere bado yana uhai kwamba ubaguzi ni dhambi itakayokuja kulitafuna taifa.
 
Kunataarifa zindai kwamba kuna hati za maelewano zipatazo 30 zilisainiwa na Rais katika ziara yake ya Dubai.

Pia inadaiwa, huu mkataba wa Bandari ni moja tu kati ya vilivyomo kwenye maelewano hayo. Pia kuna sekta zingine kama posta nk.

Inasemekana kwamba, MOU hizo zote zikiwekwa wazi, basi waTanganyika wote mtalala uchi barabarani mkigalagala na kulia.

Ombi, MOU hizo zote 30 alizosaini, ziwekwe wazi.
huu uongo kuna siku mtaamka msene wake zenu au waume zenu wameuzwa
 
Ombi, MOU hizo zote 30 alizosaini, ziwekwe wazi.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni suala la muda tu. Nasikia kuna mpaka ya mwarabu wa jangwani kuja kutusaidia kutunza misitu yetu! Pia Dr Slaa amesema kuna kitu kingine kipya kinakuja siku si nyingi. Kwenye hiyo hiyo inner circle ya Maushungi kuna watanganyika wengi wamechukizwa. Unakumbuka Ndugai alivyosema nchi inauzwa? Alikwishanusa kitu. BTW mazingira aliyolelewa na kukulia huyu mama yanamasisha watu hasa wanawake kuwa tegemezi kwa waarabu. Nadhani wajanja waliojua huu udhaifu wakautumia kumshawishi kuwa akiwapa wajomba nchi wataitengeneza kama walivyofanya kwao.
 
Kunataarifa zindai kwamba kuna hati za maelewano zipatazo 30 zilisainiwa na Rais katika ziara yake ya Dubai.

Pia inadaiwa, huu mkataba wa Bandari ni moja tu kati ya vilivyomo kwenye maelewano hayo. Pia kuna sekta zingine kama posta nk.

Inasemekana kwamba, MOU hizo zote zikiwekwa wazi, basi waTanganyika wote mtalala uchi barabarani mkigalagala na kulia.

Ombi, MOU hizo zote 30 alizosaini, ziwekwe wazi.
Kwa uvivu wa huyo mama atakuwa hakuzisoma hizo agreements yeye aliwaachia wasaidizi wake wasome nao wakaacha kuzisoma pia.
 
Mimi mtanzania kama wewe na siuzwi kwa mwarabu yoyote na sitokuja kuuzwa kwa mtu yoyote.

Huu uanaharakati hauna tija iwapo mwisho wa siku bandari inaingiza pato dogo kuliko uwezo wake halisi.

Kagame alitucheka enzi za JK namna tunavyoshindwa kuitumia rasilimali ya bahari yenye bandari iliyo katika nchi yenye bahati ya kijiografia.

Hata huko kaburini Nyerere anatucheka tukiwa tumejaaliwa rasilimali za kila aina na mpaka leo miaka 24 baada ya kifo chake tumenasa kwenye mijadala na siasa za maongezi za JF.
Ninyi ndio wale sifia sifia hata ktk mambo ya kijinga yaliolitesa taifa hili kwa miongo mingi hata sasa...sitaki kuamini kama hauna ufahamu wa kile kinacholalamikiwa na watanzania ktk sakata hili...unataka kutuaminisha kuwa wote walioukosoa mkataba huu ni wanaharakati na watu wasiopenda wawekezaji...!
 
Vipi waki-sign kimya kimya...?
Mara ngapi tena? Walishafanya hivyo na wamekurupushwa tu...
20141018_MAP004_0.jpg

Hayo juu ndiyo yanayoendelea.
 
Mnatenda dhambi mbaya sana ya kupotosha taifa lenu. Mnatenda dhambi mbaya sana ya kumchonganisha Samia na watu anaowaongoza kwa nia tu za kuutaka urais wa JMT 2015.

Dhambi mbaya mnayoifanya mtakuja kuilipia siku moja isiyokuwa na jina wala isiyojulikana tarehe yake.
Chawa wa mama
 
WANASHERIA WAANDIKE BARUA KWA DP WORLD WAKIMTAADHALISHA KUWA YALIYOFANYWA NA SAMIA WATANGANYIKA HATUKUMTUMA. HIVYO HAWATAPOKELEWA HAPA
Lbda waje watanzania wapya, lakini kama ni sisi wa siku zote watapokelewa tu na tubakia kulalama huku mitandaoni na vijiweni.
 
Muda sio mrefu utaona mikataba ya kibiashara ikisainiwa na suala hili kumalizika kabisa. Hakuna kitu serikali itataka kufanya halafu ikashindwa kufanikisha nia yake.

Samia kaamua kutumia njia ya demokrasia njia ya kistaarabu vinginevyo angekuwa JPM suala hili kitambo keshalimaliza, usingemsikia Mwabukusi au kima mwingine yoyote akifungua mdomo wake.

Nasikitikia madhara ya nguvu kubwa wanayotumia wapinzani wa awamu ya sita katika kujaribu kuja kufanikisha malengo yao ya baadae, inaweza ikavunja nchi yenye miaka karibu 60 kwa sababu ya siasa zao za chuki badala ya kujikita kwenye mantiki nzima ya hoja.
Hivi kwanini hamtaki kujibu hoja husika?
 
Hayo yote uliyohoji hayawezi kuandikwa kwenye makubalino yaliyopitishwa bungeni. Kule Dodoma ilipitishwa framework ya biashara itakayovyukiwa au kwa lugha nyingine ilipitishwa SKELETON tu ya namna mtu atakavyokuwa.

Huku kwenye kupitisha mikataba ya kibiashara ndio yote hayo uliyohoji yanakwenda kupitishwa baada ya mijadala ya kina kati ya mwekezaji na mzalendo.
Ipo tofauti ya makubaliano na mkataba?
 
Back
Top Bottom