Daah, hatari, ila..
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Tanganyika wazanzibar wanachukua Mali yetu kisa Cha muwekezaji jamani.
WHY WHY BANDARI ZA ZANZIBAR No. KUWA FAIDA WACHUKUE WAO TU YOTE HATA TANGANYIKA ISIPATE FAIDA YA 0TZS. HUKU MASIKINI WAKIUMIZWA NA KODI YA MIAMALA NA KILA SEHEMU IMEJAA KODI WHY HUYO ASEMEHEWE KODI HAMUONI KUWA HAO JAMAA WANAJILIPA KWENYE BANDARI KAMA WENGINE WALIVYOKWISHAJILIPA KWENYE UMEME, GESI NA MAFUTA WAO TU NDIO MADILA BASI PAMOJA NA SUKARI.
WATU MMELALA SIJUI MTAJUJA KUWAAMBIAJE WAJUKUU ZENU WATAKAPOKUWA HAWANA PA KWENDA NA KUTUMIKISHWA KAMA PUNDA NA HUKU WEWE UMESHIBA LEO PEKEE.
JAMANI ACHENI UOGA KIZAZI CHA AKINA NYERERE WALITESEKA SIE TUWE HURU WHY SIE TUNAKUWA WAOGA NA ASKARI ANAGANYA KAZI KAMA ROBOTI ANAUA MTU ANAYETETEA TAIFA KISA CHA AJIRA YAKE AMBAYO KWANZA INAMFANYA AWE MASIKINI.
ANGALIENI NCHI YETU IMESHAUZWA IMEISHA PORI TENGEFU, MADINI YAMEISHA YOTE WANAWAPA WATU KWA GAWIO LA SIRI KIVYAO NA SIO LA SERIKALI.
BAADAYE UNAKAMULIWA KODI MPAKA VIMA YAISHE.
YAANI HUJIULIZI UNALIPWA SALARY KODI, UKITOA HELA BANK KODI, UKIITUMA KODI, UKIITOA ULIYOTUMIWA KODI, UKINUNUA KITU KODI , YAANI KUNA KODI NYINGI MNO UNALIWA MPAKA UNAKUJA KUIPATA HELA YAKO.
HUKU WATU WAKIWAPA MA EX WAO GARI ZA 500M.