Nimefanikisha kutimiza ndoto za binti wangu wa kazi

Jifikirie una matatizo gani mpaka ukimbiwe na madada wa kazi?
 

Wema hulipwa kwa wema.
 

Polee Sanaa mkuu,Mana umeongea kwa uchungu kweli...huyu mtafutie mwenzake jeuri itapungua Kama sio kuishaa.

Embu funguka kidogo vigezo gani vilipelekea adi ukamchagua yeye Ili na sisi ambao bado kuoa tusije tukanasa Kwenye huo mtego.
 
Mahouse girls wengi ni wanawake wazuri sana hasa upande wa kuwaoa...wanajituma,wanatabia nzur ndani adi nje,wanajua kumuhudumia mme Kama mtoto vile japo wengi wanakuwa sio attractive (romantic) kutokana na matunzo yao but wakipata matunzo mazur wanavutia kwakweli adi mama mwenye nyumba anakuwa na wivu.

Ila hawa wadada wanapitia changamoto nyingi sana,kuna mdada nafahamiana nae kafanya hizo kazi takribani nyumba tatu na nyumba zote hzo kanusurka kubakwa na baba wenye nyumba....yani adi sasa yupo hopeless kabsa...nimempa nafasi ya kuwa mke wangu apo mbelen coz kakizi baadh vigezo vyangu,nimemwambia ajifikirie akiridhika tufate taratibu tufunge ndoa.
 
Safi sana mkuu
 
nakupongeza mkuu kwa Jambo hili. na Mimi umenifundisha Jambo nikipata nafasi nitafanya Kama wewe.

Asante Sana.

Kuna mashetani huwa yanawageuza watoto wa watu Kama watumwa, kazi kibao huku mshahara mdogo Sana mengine yanawabaka kabisa walaaniwe kwa kweli
 
Hongera sanaaa mkuu kwa moyo huo
 
Pole sana mkuu, wanawake sampuli hii ni wengi sana kwenye jamii yetu
 
Mimi mwenyewe beki3 mkuu! Kama itakupendeza naomba 300,000/ - nimnunulie mama kiwanja!
Ukishindwa naomba 30000/-
Hongera kwako pia.
Kama haya mawazo ni ya beki3 ina maana hata wewe bosi wako anakutunza vizuri na anastahili pongezi lol!!

..Wasaidizi wa ndani wanatumikishwa kitumwa kiasi kwamba hata wao wenyewe wanajidharau na kutokukua kiakili.
Wengi wao ni ndani tu muda wote, hawapewi nafasi ya kujua dunia inaendaje.
Hata kuangalia tv ni mpaka bosi wake aondoke na hapo wanaishia kuangalia bongo muvi na tamthilia nyinginezo.
Kwa asilimia kubwa Ubeki3 ni utumwa ndani ya jamii huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…