DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,256
- 4,647
Habari zenu
Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu
Shughuli ilianzia alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofissini na kuniagiza vitumbiua vya mia tisa
Kwakweli kulingana na nilivyokua mi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri na nimechomekea
Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa nimechomekea, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana
Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kua sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize
mi nina mke na watoto uniagize vitumbua?
Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi
Hivi hii ni sawa kweli?
Sasa kama pamoja na kuvaa vizuri na kuchomekea ulishindwa kuelewa kwamba kuagizwa vitumbua ni sehemu ya kazi yako?
Ungetambua kwamba kwa kuagizwa vitumbua, mkeo na watoto wanaweka foleni ya kwenda msalani ungekimbia kununua fasta.
Unaona ulivaa vizuri kwasababu unalipwa mshahara na huyo uliyemtunishia misuli. Kodi ya ofisi ulimokaa yeye ndo analipa, kimsingi wewe ni ndezi kama ndezi wengine tu.