Nilisomaga mtandaoni kuna ajali ya ndege ilitokeaga kama sio 2014! Kwa mujibu wa taarifa za kisanduku cheusi ndege ilidondoshwa kwa makusudi kwa sababu dakika chache sana kabla ya kudondoka ilisikika sauti ya mtu anayegonga kwa nguvu mlango kama mtu anayetaka kufunguliwa katika mlango wa chumba cha marubani.
Hii inaonesha aliyeiangusha ndege kwa makusudi ni rubani msaidizi na aliyekuwa anagonga ni rubani kwa sababu kuna sauti ilinaswa kabla ya hapo ilisikika rubani mkuu akimuaga msaidizi kwamba anaenda kujisaidia, hivyo msaidizi akaitumia hiyo fursa kujifungia na kuilazimisha ndege ishuke chini kwa nguvu na kusabisha ajali.
Ripoti zinasema kabla ya pale huyo jamaa alikuwa kama ana msongo wa mawazo na alikuwa anajitapa kuwa siku moja atakumbukwa kwa sababu atafanya tukio la kukumbukwa.
Alikuwa analalamika kuwa anatumikishwa na rubani kufanya kazi ambazo hakusomea.
Kuna siku alipigana makonde na rubani kisa aliambiwa ahesabu abiria akasema sio kazi yake, yeye amesomea kurusha ndege.
Nadhani upo kwenye kundi