love life live life
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 2,584
- 3,051
Tunachohitaji is the cause of every cause.Kwa hiyo unaamini simu imetengenezwa na mtu na yupo, unaamini gari kuna wajapani wameitengeneza ila hayupo aliyekutengeneza wewe na babu zako wote? Mzee kuna eneo lingine tofauti na hili ambapo una ukilaza wa hiyari?
Yaani simu haukumuona mtengenezaji ila kwa confidence kabisa unaamini yupo. Grai unaamini yupo aliyelitengenza japo hujawahi hata kuongea naye. Ila Aliyekutengeneza wewe umeamua kuamini hayupo? Dah, kweli kuna ujinga wa hiyari!
Vipi kama wewe ndio umesinzia and you need to wake up?Shetani ndio husema hivyo ili afiche ukweli. Anyway Yehova hahitaji wewe mimi au mtu mwingine amwamini ili awepo. Yaani Yupo halafu ndio Mungu sasa. Alikuumba na huna cha kufanya. Na kuna siku utakutana naye uso kwa uso. By then hata ujasiri wa kumwita Mungu let alone shetani utakuwa huna.
Angalau utaikumbuka hii post! Hello, wake-up before it's too little late!
Hayo yote yana prove vipi ndio Mungu unayemwamini na si Alla kwa waislamu,Mpumbavu husema moyoni mwake hakuna Mungu, bible.
Usitazame nje ili uone uwepo wa Mungu
Anzia kwako wewe hapo
Ulipokua haupo, shahawa ya baba yako na yai la mama yako vilivyokutana ukaanza kutengenezwa,
Kwanza ukiwa bonge zito la damu
Baadae ukajishika kwenye mji wa mama yako
Ukakulia humo huku viungo vyako vikijitengeneza ukianza na moyo, then mishipa ya damu, ubongo, na viungo vingine , mifupa yako inayokufanya uweze kuwa na hiyo fremu , sikio, jicho na kila kitu
Ukakua hadi muda ukafika ukaanza uchungu, ukapita kwenye uke wa mama yako!
Umbilical cord ikakatwa ukaanza kunyonya huku hujui unachokifanya!
Kwa sababu hakuna ambaye ana kumbukumbu ya hayo hadi pale wakati unapofika kumbukumbu unapozaliwa na ufahamu kuwepo, Mambo yote haya yakitokea kwa mpangilio wa aina yake!
Ufahamu kuwa wewe siyo hizo hisia ulizoziandika hapo! Ubongo wako ukipewa chakula na moyo wako ukawa hai ndivyo vilivyokufanya uandike hayo!
Pamoja na uhuru uliopewa ukatype bila obvious consequences as of now!
Njoo Nje yako sasa
Tazama hapo ulipo angani wakati wa mchana...
Jua
Je unajua kwamba dunia na ardhi yake ipo angani inaelea!
Unayo hii perception? Kwamba unaweza kwenda Around hii ardhi/ dunia— ile circumnavigation?
Kwamba Gimba hili liitwalo dunia linaelea angani na hawa watu wengi wasioona?!
Je mpangilio huu umejiweka wenyewe!
Je vitu alivyovifanya mwanadamu vimejiweka tu vuu vikawa?
Kama ni ndege ulaya ina design yake, kama ni gari/ pikipiki vilevile.
Hakuna chombo chochote kilichozuka!
Lazima kila chombo kina design yake na designer wake!
Vyombo artificial vina design yake na designer wake ambae ni Mtu
So kupanga ni kuchagua lakini unapowaza kuhusu Mungu ukafikiri hayupo jitazame wewe kwanza—look through you you siyo unamtazama mtu kwa ngozi yake tuu!
Mtazame as a whole and as made of Parts.
Mtazame kwa hilo jicho la kitabibu kama kitu kamili kilicho na parts na Umuone akiwa hai lakini akiwa wa kufa pia.
“See now that I, even I, am he, and there is no god with me: I kill, and I make alive; I wound, and I heal: neither is there any that can deliver out of my hand.” Bible
Lets say kama umemuamini Mungu AllahHuyo huyo unaye amua ww kumu amin ..
Shida ukiamini haya Mambo unakuwa chizi sadaka zinaliwa tu na wajanjaBora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Hata ukiamini Mungu yupo mbona haikuzuii kufanya mambo yoyote unayotaka!???
Binadam aliyekamilika anapaswa kuishi kwa ustaarab flan na utaratibu hata kama haamini Mungu.
Haya sasa umeamua kutoamin, inakusaidia nini??au inakuongezea nini ambacho hukua na fursa kuki parsue...Ulipokua ukiamin, ni kitu gan ulikua unapungukiwa??
Una unaishi kwa kukariri??
😅😅😅 Too slow. Nimempa iyo movie ili nikimuelekeza baadhi ya mambo tofauti tofauti aweze kuhandle.Umeanza kuamini katika movie[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Statement hii haipo specific katika ulimwengu wenye dini zaidi ya 5,000 ambazo kila mmoja ana abudu Mungu tofauti na mwingineAmini tu kuwa Mungu yupo, haitakugharimu chochote.
Ukifika huko ukakuta hayupo it's okay.
I hope ukikuta mtu amelala huwa unatumia same reasoning kuwa may be wewe ndiye uliyelala!Vipi kama wewe ndio umesinzia and you need to wake up?
Kusema wake hata kwenye ndoto unaweza kusema.
Hiyo haina shaka.I hope ukikuta mtu amelala huwa unatumia same reasoning kuwa may be wewe ndiye uliyelala!
Aliyekwambia kila kitu kina chanzo nani? Umeitoa wapi hii?Tunachohitaji is the cause of every cause.
Huyo "mungu" anayeumbwa ni feki. Kwanza una assumption zisizo za kweli kwamba kila kitu kina mwanzo. Hii nadharia umeitoa wapi?Mungu ametuumba kama ni hivyo yeye ameumbwa na nani?
Kwa sababu tuna mwanzo. Hahitaji kuumbwa kwa sababu hana mwanzo. Ulitaka aumbwe lini sana?Na kama hajaumbwa kwa nini sisi iwe lazima tumeumbwa!?
Basi una tatizo! Ina maana huna uhakika wa kitu chochote na hivyo huna haja ya kujadiliana na watu.Hiyo haina shaka.
So interested, but it has nothing to do with existence of GodNilipata kusimuliwa kisa kimoja,
Kuna bwana mmoja alikua akitembea ufukweni huku akitafakari juu imani ya kikristo ya utatu mtakatifu yaani Mungu baba,Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu,huyu bwana aliona kwamba anapigwa haiwezikani Mungu mmoja nafsi tatu.
Ghafla akakutana na katoto kadogo pake yake kakiwa kanafukua mchanga wa ufukweni akavutwa kuongea nacho kwani kalikuwa peke yake pasipo wazazi.
Huyu bwana akakauliza kanafanya nini pale kakiwa peke yake?
Kale katoto kakamjibu kanachimba shimo ili kahamishe maji yote ya bahari kwenye kishimo anachochimba na bahari itakauka kabisa.
Yule bwana akakaambia kale katoto karudi nyumbani kwani haiwezekani kuhamisha maji ya bahari yaenee kwenye kale kashimo.
Kale katoto kakamjibu kwamba uwezo wa kichwa chake ni mdogo Sana kulielewa fumbo la imani la utatu mtakatifu linalo msumbua kulitafakari,vivyo hivyo ataendelea kuona haiwezekani maji ya bahari kuyahamishia kwenye kale kashimo kwani uwezo wa kichwa chake ni mdogo.
Yule bwana akaingiwa hofu dogo amejuaje kwamba yeye anatafakari juu ya utatu mtakatifu.
Kwa bahati mbaya kale katoto kalitoweka kwenye mazingira yakutatanisha.
Kwa mafano huu ni dhahiri uwezo wa vichwa vyetu ni mdogo Sana kutafakari na kuelewa habari za uwepo wa Mungu.
Samahani kwakujibu kwa hadithi ndefu chief.
Kama kuna baadhi ya vitu havina mwanzo.Aliyekwambia kila kitu kina chanzo nani? Umeitoa wapi hii?
Huyo "mungu" anayeumbwa ni feki. Kwanza una assumption zisizo za kweli kwamba kila kitu kina mwanzo. Hii nadharia umeitoa wapi?
Kisayansi na kifalsafa ni kitu chenye mwanzo pekee ndio kina sababu ya chanzo. Sasa Mungu hana mwanzo wala mwisho unataka chanzo kianzie wapi?
Kwa sababu tuna mwanzo. Hahitaji kuumbwa kwa sababu hana mwanzo. Ulitaka aumbwe lini sana?
Haya mambo ni yapi? Biblia imesema kuwa nyakati hizi za mwisho kutakuwa na matapeli wengi na watakuja kwa jina la Yesu. Na kwamba wazipime kila roho, ili kuona kama zimetoka kwa Mungu. Na ya kuwa watawajua kwa matendo yao.Shida ukiamini haya Mambo unakuwa chizi sadaka zinaliwa tu na wajanja
Hahaha!!! Nyakati za mwisho zimeimbwa sana na hazifiki..Haya mambo ni yapi? Biblia imesema kuwa nyakati hizi za mwisho kutakuwa na matapeli wengi na watakuja kwa jina la Yesu. Na kwamba wazipime kila roho, ili kuona kama zimetoka kwa Mungu. Na ya kuwa watawajua kwa matendo yao.
Huwezi kuiamini na kuifuata Biblia na bado ukatapeliwa na hao wahuni. Unless "haya mambo" unamaanisha kitu kingine!
Khaa! How absurd is your question. Kwa hiyo birthday yako kwa mfano ina maana gani?Kama kuna baadhi ya vitu havina mwanzo.
Kwa nini unalazimisha binadamu anamwanzo?
Yani siku biblia ikisema hakuna moto wafia dini hawataimba tena hizi nyimbo za kumpenda Mungu,Haya mambo ni yapi? Biblia imesema kuwa nyakati hizi za mwisho kutakuwa na matapeli wengi na watakuja kwa jina la Yesu. Na kwamba wazipime kila roho, ili kuona kama zimetoka kwa Mungu. Na ya kuwa watawajua kwa matendo yao.
Huwezi kuiamini na kuifuata Biblia na bado ukatapeliwa na hao wahuni. Unless "haya mambo" unamaanisha kitu kingine!
Unaelewa hata ya maana ya nyakati za mwisho?Hahaha!!! Nyakati za mwisho zimeimbwa sana na hazifiki..
Nilijua tu hujui. Biblia imeandikwa na Vatican lini?Biblia imeandikwa vatican, unaitumiaje kama reliable source yako?
Unahaki ya kusema walio kinyume na imani yako ni wapagani na kwa ulivyo jinasibu kua wewe ni muislamu wala sishangaiMpagani ni mpwgani ata ukilemba vipi.Tupo waislamu wenye hofu ya allah lakini hatufanyi ibada ya kutosha kwa sababu ya udhaifu wetu lakini hatujawahi kubisha uwepo wa Allah.
Mpagani ni mpagani tuu