Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Asante

Pia uwepo wa Mungu hauna athari hasi kwa maisha ya mwanadamu.Sijaona faida ya upagani.Dini huwafanya wanadamu waishi kwa pamoja kwa amani kwa kusaidiana.Upagani shabaha yake ni watu wasiishi kama jumuiya.Katika maisha ya mwanadamu hakuna kitu chema kama kuishi katika jumuiya.

Uliza wapagani huwa wanakutana kujadili kutokuwepo mungu na kushirikiana kijamii? Utaambiwa sisi hatuna makanisa ila huwa tunakutana mitandaoni kumpinga Mungu🙂

Kwa uelewa wangu mdogo ni bora ya FREEMASON kuliko upagani.Yaani upagani ni TAKATAKA
Mtu yeyote anaweza kuwa mpagani katika jicho la dini tofauti na yake

Ni kama ishu ya Mungu na miungu, Mungu wako anaweza kuwekwa kundi la miungu kwenye dini nyingine tofauti na yako kama ambavyo wewe ulivyowaita miungu

Mimi kuniita mpagani haina maana kwamba wewe umesalimika na jina hilo, ni kama ambavyo muislamu anavyo kuita wewe kaffir japokuwa anajua una amini MUngu
 
wote hao walisoma seminary wakatimuliwa fatilia historia zao utagundua kwanini walikuja kukataa mambo ya Mungu,na baadae wakamrudia
Kutimuliwa seminari haimaanishi waliachana na mambo ya Mungu.
 
Kwa mamlaka ya Yesu natamka nguvu ikushikie.Na utakuwa MTU wa kwanza Ulipo kuona Ukuu wa Mungu.Tubu Leo mambo yako yote yatakuwa sawa futa kauli chafu
Acha vitisho ww , unamtisha ili iweje? Fikra za kijinga sana hizi
 
Nilipata kusimuliwa kisa kimoja,

Kuna bwana mmoja alikua akitembea ufukweni huku akitafakari juu imani ya kikristo ya utatu mtakatifu yaani Mungu baba,Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu,huyu bwana aliona kwamba anapigwa haiwezikani Mungu mmoja nafsi tatu.

Ghafla akakutana na katoto kadogo pake yake kakiwa kanafukua mchanga wa ufukweni akavutwa kuongea nacho kwani kalikuwa peke yake pasipo wazazi.

Huyu bwana akakauliza kanafanya nini pale kakiwa peke yake?

Kale katoto kakamjibu kanachimba shimo ili kahamishe maji yote ya bahari kwenye kishimo anachochimba na bahari itakauka kabisa.

Yule bwana akakaambia kale katoto karudi nyumbani kwani haiwezekani kuhamisha maji ya bahari yaenee kwenye kale kashimo.

Kale katoto kakamjibu kwamba uwezo wa kichwa chake ni mdogo Sana kulielewa fumbo la imani la utatu mtakatifu linalo msumbua kulitafakari,vivyo hivyo ataendelea kuona haiwezekani maji ya bahari kuyahamishia kwenye kale kashimo kwani uwezo wa kichwa chake ni mdogo.

Yule bwana akaingiwa hofu dogo amejuaje kwamba yeye anatafakari juu ya utatu mtakatifu.

Kwa bahati mbaya kale katoto kalitoweka kwenye mazingira yakutatanisha.

Kwa mafano huu ni dhahiri uwezo wa vichwa vyetu ni mdogo Sana kutafakari na kuelewa habari za uwepo wa Mungu.

Samahani kwakujibu kwa hadithi ndefu chief.
 
Bora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Hata ukiamini Mungu yupo mbona haikuzuii kufanya mambo yoyote unayotaka!???
Binadam aliyekamilika anapaswa kuishi kwa ustaarab flan na utaratibu hata kama haamini Mungu.

Haya sasa umeamua kutoamin, inakusaidia nini??au inakuongezea nini ambacho hukua na fursa kuki parsue...Ulipokua ukiamin, ni kitu gan ulikua unapungukiwa??

Una unaishi kwa kukariri??
Wew sas ndio mwenye uzi kuliko Yule aliyefuta biblia kisa ajaona uku wa mung ktk kutokomeza njaa na Vita
 
Hivi mbona huwa watu mnashindwa ku reason? Kwanini umwambie mtu aamini jambo ambalo halipo kisa hofu tu?

Eti ukifika huko ukakuta hayupo it's okay? Ukifika wapi? Nani alikuambieni kuwa ukifa kuna mahali utaenda?

Mkuu mleta mada mimi nakupongeza kwa kujitambua.

Welcome to the Enlightened Club.
Sawa,
 
View attachment 2099557
Sasa nimeamini kuwa dini ni kwaajili ya maskini na waoga tu.

Mpaka leo hakuna mwanadamu au kitu chochote ikiwemo Mungu alitethibitisha kuwa Mungu yupo.

Kila mtu atakuthibitishia kwa maandiko ambayo yameandikwa kwa mkono wa mtu.

Ukiondoa maandiko hakuna mtu wa dini kukuthibitishia uwepo halisi wa Mungu.

Waislamu kwa kitabu chao watakuthibutishia uwepo wake, Wahindu, Wabudha, Waktisto n.k watakuthibutishia uwepo wa Mungu kwa maandiko na hadithi tu ila hawataweza kukuthibitishia kwa njia nyingine ya reality.

Kwa taabu wanazopata watu duniani ni kama nature ndio inatawala.

Haiwezekani Mungu ambaye wanasema aliupenda ulimwengu aruhusu vita, ubakaji, kuchinjana, kudhulumiana, ufukara, njaa n.k huku hivyo vitu ni vidogo kwake angevikomesha ndani ya sekunde.

Je, Mungu kazidiwa utu na upendo na mwanadamu?

Hii amani na hali ya maendeleo tunayoiona ni fikra na utu wa binadamu kwa ulimwengu.

Binadamu anaunda mabaraza ya kitaifa kupambana na majanga mbalimbali, pasipo na haya mabaraza Dunia isingekalika kabisa kwa idadi hii ya watu ilivyo kwa sasa.

Illusion ndizo zinatawala watu ndio maana kila dini na dhehebu wanajiona kuwa wako sahihi na wana ushahidi kuwa dhehebu lao ndilo sahihi mbele za Mungu na wao tu ndio wataingia mbinguni au peponi.
View attachment 2099556
Km huamini kuwa MUNGU yupo, basi tupe Sababu za msingi zinazokufanya uone kuwa MUNGU hayupo.
 
Mtu yeyote anaweza kuwa mpagani katika jicho la dini tofauti na yake

Ni kama ishu ya Mungu na miungu, Mungu wako anaweza kuwekwa kundi la miungu kwenye dini nyingine tofauti na yako kama ambavyo wewe ulivyowaita miungu

Mimi kuniita mpagani haina maana kwamba wewe umesalimika na jina hilo, ni kama ambavyo muislamu anavyo kuita wewe kaffir japokuwa anajua una amini MUngu
Mpagani ni mpwgani ata ukilemba vipi.Tupo waislamu wenye hofu ya allah lakini hatufanyi ibada ya kutosha kwa sababu ya udhaifu wetu lakini hatujawahi kubisha uwepo wa Allah.
Mpagani ni mpagani tuu
 
View attachment 2099557
Sasa nimeamini kuwa dini ni kwaajili ya maskini na waoga tu.

Mpaka leo hakuna mwanadamu au kitu chochote ikiwemo Mungu alitethibitisha kuwa Mungu yupo.

Kila mtu atakuthibitishia kwa maandiko ambayo yameandikwa kwa mkono wa mtu.

Ukiondoa maandiko hakuna mtu wa dini kukuthibitishia uwepo halisi wa Mungu.

Waislamu kwa kitabu chao watakuthibutishia uwepo wake, Wahindu, Wabudha, Waktisto n.k watakuthibutishia uwepo wa Mungu kwa maandiko na hadithi tu ila hawataweza kukuthibitishia kwa njia nyingine ya reality.

Kwa taabu wanazopata watu duniani ni kama nature ndio inatawala.

Haiwezekani Mungu ambaye wanasema aliupenda ulimwengu aruhusu vita, ubakaji, kuchinjana, kudhulumiana, ufukara, njaa n.k huku hivyo vitu ni vidogo kwake angevikomesha ndani ya sekunde.

Je, Mungu kazidiwa utu na upendo na mwanadamu?

Hii amani na hali ya maendeleo tunayoiona ni fikra na utu wa binadamu kwa ulimwengu.

Binadamu anaunda mabaraza ya kitaifa kupambana na majanga mbalimbali, pasipo na haya mabaraza Dunia isingekalika kabisa kwa idadi hii ya watu ilivyo kwa sasa.

Illusion ndizo zinatawala watu ndio maana kila dini na dhehebu wanajiona kuwa wako sahihi na wana ushahidi kuwa dhehebu lao ndilo sahihi mbele za Mungu na wao tu ndio wataingia mbinguni au peponi.
View attachment 2099556
Mkuu, kwanza nikutake ukaitubu hii dhambi mara moja; kwasababu iko hatari kubwa inakunyemelea siku za usoni kwako mwenyewe au kwa uzao wako. Hakuna mtu au Taifa lolote lile lililomkufuru Mungu likabaki salama.

Biblia Takatifu (kwa mani yangu ya Kikristo) iko dhahiri kabisa kuwa Mungu yupo. Tofautisha ukinzani wa imani mbalimbali juu ya uwepo wa Mungu na uhalisia.

Siko sehemu rafiki sana ya kukupa uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa sasa ila NAKUHAKIKISHIA kwamba MUNGU YUPO. GOD IS REAL.

Nitarudi baadaye kidogo.
 
Hizo ni blabla tu haya nikuulize na wewe ni nani aliyetengeneza huyo Mungu na kumpa uwezo wa kutengeneza hivyo unavyodai ni Kazi yake Yaani Ulimwengu vitu vyote?
Maana kama unaamini binadamu aliumbwa lazima muumbaji ana muumbaji wake pia maana hiyo ndio kanuni ya maisha katika ulimwwngu wetu!
Embu twende polepole Unasema kama "binadamu aliumbwa lazima muumbaji ana muumbaji wake pia maana hiyo ndio kanuni ya maisha katika ulimwwngu wetu!" Kupitia hiyo kauli yako embu tuambie binadamu aliumba/ameumba nini ili tuone kama kweli kila muumbaji anamuumbaji wake
 
Pole kushtuka leo ila hongera kwa kuanza kujitambua haiwezekani mungu awe na jina la Jehovah asili yake kiibrania au aitwe Allah asili yake kiarabu kwanini mji mtakatifu uwe Jerusalem au makka na kwanini biblia itaje makabila 12 ya israel au quran itaje kabila la quraish ukijuliza hayo maswali utakuja kugundua hizi ni tamaduni za watu nasi tulivamia tu mimi niliacha mambo ya dini mwaka 2014 nikiwa na miaka 22 tu niliona ujinga kuamini mauzauza eti katika biblia kuna watu wanageuka chumvi wengine walizaliwa bila ya baba huku Quran watu wanongea na sisimizi yaan vituko vitupu mtu anakaa kuamini vituko hivi
 
Imani Yako nguvu Yako, ukitaka kujua Mungu yupo amini halafu omba lolote likitokea umethibitisha Imani Yako. Biblia inakusaidia tu kujua sheria za Mungu na taratibu
 
Waje hapa wathibitishe tuamini
Hapo ndio huwa mnakosea sana. Yaani maisha baada ya kifo na ukweli uliopo kule ni jukumu lako. Ukikosea hasara si ya Mungu wala si ya hao unaowataka wathibitishe. Hasara ni yako. Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe.

Kama una akili timamu hakuna mtu ulisubiri akutafutie kazi ili uthibitishe kama kuna kazi. Ulihangaika mwenyewe. Sasa mbona kwenye mambo ya msingi unajilegeza na kusubiri waje "wakuthibitishie"?

Nimalizie na ushauri huu. Mwizi akitaka kukamatwa anajua pa kwenda. Vivyo hivyo anayetaka kuhakikisha uwepo wa Mungu anajua pa kwenda. Endelea kusubiri waje wakuthibitishie...!
 
Pole kushtuka leo ila hongera kwa kuanza kujitambua haiwezekani mungu awe na jina la Jehovah asili yake kiibrania au aitwe Allah asili yake kiarabu kwanini mji mtakatifu uwe Jerusalem au makka na kwanini biblia itaje makabila 12 ya israel au quran itaje kabila la quraish ukijuliza hayo maswali utakuja kugundua hizi ni tamaduni za watu nasi tulivamia tu mimi niliacha mambo ya dini mwaka 2014 nikiwa na miaka 22 tu niliona ujinga kuamini mauzauza eti katika biblia kuna watu wanageuka chumvi wengine walizaliwa bila ya baba huku Quran watu wanongea na sisimizi yaan vituko vitupu mtu anakaa kuamini vituko hivi
Pole sana. Inaonekana unatamani sana ku justify uamuzi wako. Unajua kuwa ulifanya uamuzi feki ndio maana unatumia nguvu nyingi sana kujaribu kuonyesha kwa nini uko rational.

Umeandika ujinga mtupu jambo linaloonyesha haukuacha kuamini kwa sababu ya ushahidi fulani ila uliamua na hivi ni visingizio vya kujiridhisha nafsi.

Kiufupi Jehovah sio Allah na kwa hiyo kila ulichoandika baada ya hapo ni ujinga kama ujinga mwingine!
 
View attachment 2099557
Sasa nimeamini kuwa dini ni kwaajili ya maskini na waoga tu.

Mpaka leo hakuna mwanadamu au kitu chochote ikiwemo Mungu alitethibitisha kuwa Mungu yupo.

Kila mtu atakuthibitishia kwa maandiko ambayo yameandikwa kwa mkono wa mtu.

Ukiondoa maandiko hakuna mtu wa dini kukuthibitishia uwepo halisi wa Mungu.

Waislamu kwa kitabu chao watakuthibutishia uwepo wake, Wahindu, Wabudha, Waktisto n.k watakuthibutishia uwepo wa Mungu kwa maandiko na hadithi tu ila hawataweza kukuthibitishia kwa njia nyingine ya reality.

Kwa taabu wanazopata watu duniani ni kama nature ndio inatawala.

Haiwezekani Mungu ambaye wanasema aliupenda ulimwengu aruhusu vita, ubakaji, kuchinjana, kudhulumiana, ufukara, njaa n.k huku hivyo vitu ni vidogo kwake angevikomesha ndani ya sekunde.

Je, Mungu kazidiwa utu na upendo na mwanadamu?

Hii amani na hali ya maendeleo tunayoiona ni fikra na utu wa binadamu kwa ulimwengu.

Binadamu anaunda mabaraza ya kitaifa kupambana na majanga mbalimbali, pasipo na haya mabaraza Dunia isingekalika kabisa kwa idadi hii ya watu ilivyo kwa sasa.

Illusion ndizo zinatawala watu ndio maana kila dini na dhehebu wanajiona kuwa wako sahihi na wana ushahidi kuwa dhehebu lao ndilo sahihi mbele za Mungu na wao tu ndio wataingia mbinguni au peponi.
View attachment 2099556
Kuhani Musa ni bonge la msanii
 
Imani Yako nguvu Yako, ukitaka kujua Mungu yupo amini halafu omba lolote likitokea umethibitisha Imani Yako. Biblia inakusaidia tu kujua sheria za Mungu na taratibu
Biblia haikusaidii tu kujia sheria za Mungu bali ni muongozo kamili wa namna ya kuishi, yaliyopita, yaliyopo, yanayokuja na maisha baada ya duniani.

Mungu sio ATM kwamba ukibonyeza correct PIN inatoa hela. Mungu ukimtafuta ili uthibitishe hayupo huwezi kumwona. Ni yule amtafutaye kwa bidii, intentionally, ndiye anayemwona!
 
Kwa mamlaka ya Yesu natamka nguvu ikushikie.Na utakuwa MTU wa kwanza Ulipo kuona Ukuu wa Mungu.Tubu Leo mambo yako yote yatakuwa sawa futa kauli chafu
Acha ushamba boss! Mungu sio madaso kuyarusha unavyotaka. Haya ni matumizi mabaya ya vidole!
 
Back
Top Bottom