Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Mtu yeyote anaweza kuwa mpagani katika jicho la dini tofauti na yake

Ni kama ishu ya Mungu na miungu, Mungu wako anaweza kuwekwa kundi la miungu kwenye dini nyingine tofauti na yako kama ambavyo wewe ulivyowaita miungu

Mimi kuniita mpagani haina maana kwamba wewe umesalimika na jina hilo, ni kama ambavyo muislamu anavyo kuita wewe kaffir japokuwa anajua una amini MUngu
Jibu la kisomi
Mtu yeyote huweza kuitwa mpagani na mtu wa dini nyingine bila yeye kujua
 
hao uliowataja Wana uspesho gani kwani Hadi uwaone hivyo unavyowachukulia.
wao na umaarufu wao walikataa uwepo wa Mungu ila baadae walikiri Mungu yupo na kujenga makanisa sasa wewe ni nani ukatae Mungu hayupo?
 
Mleta mada bhana nacheeeeeeka, nilitegemea ufanye yako kwa sababu huna hofu wala umaskini na wala wewe sio sehemu ya hizi dini. Kitendo cha kuleta hii thread hapa yaani umekiri nn kilicho moyoni mwako ambacho umekikana hapa huna hofu, umaskini wala sio sehemu ya hizi dini.
Waacheni wenye Mungu wao ninyi ambao hampo huko wala hamsadiki hayo msijihusishe na huko, kitendo cha kuhoji inadhihirisha kutokujiamini km ulipo ni sahihi au siyo sahihi
 
Bora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Hata ukiamini Mungu yupo mbona haikuzuii kufanya mambo yoyote unayotaka!???
Binadam aliyekamilika anapaswa kuishi kwa ustaarab flan na utaratibu hata kama haamini Mungu.

Haya sasa umeamua kutoamin, inakusaidia nini??au inakuongezea nini ambacho hukua na fursa kuki parsue...Ulipokua ukiamin, ni kitu gan ulikua unapungukiwa??

Una unaishi kwa kukariri??
Huyo ndio binadamu mbwembwe nyingi lakini hadi leo ameshindwa kuongeza hata urefu/miaka mingi ya kuishi duniani.
 
ZABURI 14

Uovu wa watu
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)
1 Wapumbavu hujisemea moyoni:
“Hakuna Mungu.”
Wote wamepotoka kabisa,
wametenda mambo ya kuchukiza;
hakuna hata mmoja atendaye jema!
2Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni,
aone kama kuna yeyote mwenye busara,
kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu.
3Lakini wote wamekosa,
wote wamepotoka pamoja;
hakuna atendaye mema,
hakuna hata mmoja.
4“Je, hao watendao maovu hawana akili?
Wanawatafuna watu wangu kama mikate;
wala hawanijali mimi Mwenyezi-Mungu.”
5Hapo watashikwa na hofu kubwa,
maana Mungu yu pamoja na waadilifu.
Mbinguni ni wapi
 
Pole mkuu unaonekana biblia hujui na sio ww asilimia 90 ya watu wengi hawapendi kuijua tulia kama unanyolewa nikupe elimu
Wewe unayeijua umeshindwa kuweka hata mstari mmoja kuthibitisha madai yako kuwa Biblia inasema kuwa ukoma chanzo chake ni laana?
Lete mstari acha porojo. Vinginevyo kubali tu umesema uongo Shetani mdogo!
 
Wewe umemuona?
Usiseme kuwa umemuona kwenye ndoa yako, elimu yako na kazi yako.
Kumbuka hiyo simu unayotumia kabuni mtu mwenye akili na wewe usiye na akili ndio unaitumia ukisema umemuona Mungu.
Unanunua gari used ambayo Japan wameipiga marufuku kuwa inachafua mazingira kisha unaenda kanisani kushuhudia matendo makuu ya Mungu kuwa kakupa gari huku umedokoa pesa za kampuni .
Kwa hiyo unaamini simu imetengenezwa na mtu na yupo, unaamini gari kuna wajapani wameitengeneza ila hayupo aliyekutengeneza wewe na babu zako wote? Mzee kuna eneo lingine tofauti na hili ambapo una ukilaza wa hiyari?

Yaani simu haukumuona mtengenezaji ila kwa confidence kabisa unaamini yupo. Grai unaamini yupo aliyelitengenza japo hujawahi hata kuongea naye. Ila Aliyekutengeneza wewe umeamua kuamini hayupo? Dah, kweli kuna ujinga wa hiyari!
 
The one who asked where in the mind, !! For him/her faith is greater than reason, when you don't understand don't believe for the sake of believing
 
Ukiwa na akili mbona unajua tuu Yupo.

Hata wanyama wanajua sembuse Binadamu!!!

Uwepo wako na kutokuwepo kwako ni ushahidi tosha kuwa Yupo
Katika maelfu ya Miungu ni Mungu gani kati ya hao akili itajua tu yupo?

Kusema wanyama wanajua pasipo kuthibitisha we umejuaje kua wanajua?

Uwepo wangu na kutokuwepo kwangu kunathibitisha vipi Mungu yupo?

Unafanya ule ulaghai tuliokubaliana mwishoni mwa mwaka 2021 kua usiurudie tena 2022?
 
Mkuu Mungu yupo ila binadamu ndo wanavuruga mambo.

Mungu anahitaji medium/chombo ili kujidhihirisha, tatizo vyombo vingi ni vichafu kama sio vyote, nazungumzia wanaojiita watumishi wa Mungu.

Hata Mimi kuna wakati nawaza huenda hakuna Mungu lakini badae nasema Mungu yupo lakini hafanyi kazi na kwakujiuliza maswali kama yako...

Bado akili inanirudisha kuamini mediums ni chafu...
Case closed[emoji122]
 
Katika maelfu ya Miungu ni Mungu gani kati ya hao akili itajua tu yupo?

Kusema wanyama wanajua pasipo kuthibitisha we umejuaje kua wanajua?

Uwepo wangu na kutokuwepo kwangu kunathibitisha vipi Mungu yupo?

Unafanya ule ulaghai tuliokubaliana mwishoni mwa mwaka 2021 kua usiurudie tena 2022?
Scars kwa uelewa wako Mungu maanake nini?
 
Kitu cha ajabu yule ambae anasali saana unakuta anayo roho mbaya tu wala hawezi kukusaidia (sio wote lakini), na yule ambae hana time na Mungu au anasali lakini sio kivileee anakua na roho nzuri.
Dini sio kigezo cha watu kua wema au wabaya cha muhimu katika maisha ni kutenda mema tu kwa nafasi yako, kuepuka makuu na kwasaidia wahitaji.

Nimeona watoto Wa wachungaji wengi wakiwa na matendo mabaya tu pia nimeona watu wasiokua na Mungu wakifanya mambo makubwa tu ya maendeleo na wakiwa na matendo mazuri tu.

MUHIMU
bora uamini Mungu yupo ukifika mbinguni ukimkuta fresh tu kuliko kutokuamini alafu ufike umkute katulia aisee believe me utapigwa fire unaambiwa ujazo wake ni Mara 1000 ya moto Wa duniani just imagine, na moto wake hauzimiki yani daily ni maumivu tu dadeki...........
[emoji38][emoji38]
 
Bora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Kwa kauli yako hii ni uthibitisho kuwa imani yako kwa Mungu sio suala la BAYANA bali ni KUBAHATISHA. Iweje aliyeumba ulimwengu huu kwa kanuni thabit kabisa, ashindwe kujidhihilisha hadi watu wafanye kubahatisha juu ya uwepo wake?
 
Kwa kauli yako hii ni uthibitisho kuwa imani yako kwa Mungu sio suala la BAYANA bali ni KUBAHATISHA. Iweje aliyeumba ulimwengu huu kwa kanuni thabit kabisa, ashindwe kujidhihilisha hadi watu wafanye kubahatisha juu ya uwepo wake?
Vyovyote vile ila naamin Mungu yupo.Hata kama kwa papasa papasa na kubahatisha..i believe there is God
 
Vyovyote vile ila naamin Mungu yupo.Hata kama kwa papasa papasa na kubahatisha..i believe there is God
Vyema. Hoja yangu, uthibitisho wa Mungu mkuu, muumba wa ulimwengu huu na vyote vilivyomo, haupaswi kuwa wa KUBAHATISHA.
 
Back
Top Bottom