Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Unahakika gani ulichokiona wewe kua ni msingi sio mawenge yako yaliyochangiwa na ufinyu wa maarifa kufikiria hicho kitu ndio msingi?
Unarudia swali ambalo nimeshakujibu.
 
Uhalisia.
Uhalisia ni nini?

Unathibitishika kwa ithibati?

Kwasababu uhalisia wa kusema viumbe vinakula na ndio sababu inayowafanya waishi, uhalisia huo upo na unakubalika na kila mtu na hakuna anayebisha kwasababu unathibitishika na ndo uhalisia

Uhalisia wa kusema allah yupo, unakubalika na kuthibitishika na nani?

Kwanini hakuna mjadala kwamba viumbe hai wanakula ili waishi kwasababu ndio uhalisia ila kuwe na mjadala wa uwepo wa allah kuwa ni uhalisia?
 
Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Reheema na mwenye kureemu akuna kiumbe yoyote aliwai kuonaona nae face to face na afananishwi na kitu chochote

Nenda kalime ukimaliza kuliza vuna mazao ukimaliza kuvuna yale mabua yanayobaki si utayateketeza kwa Moto kwakuwa ni uchafu kwako

Pia sisi Mwenyezi Mungu ni mazao kwake yatakayokuwa mema atayabeba na yatakayokuwa mabaya atayapeleka motoni

Kumbuka maisha ya dunia ni mafupi mno usidanganyike Leo ukasahau kesho yako

Yani wewe umeubwa kwa manii umewekwa tumboni mwa mama ako miezi 9 bila atabkujitambua Leo umezaliwa umekuwa unasema. Mungu ayupo na unapumua kwa pumzi yake tena bure kabisa

Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi
 
Muungu YUPO. Na uthibitisho UPO, ila sio unaoutaka wewe. Upeo wa Mungu ni wa juu sana, kuliko unavyoweza fikiria. Binafsi, BIBILIA inanisaidia kupata fununu ya Upeo huo kwa imani (naamiini ndio moja ya malengo yake).

Tuanze hapo, nitajitihidi kujushirikisha uthibitisho wa uwepo wa Mungu kadri nitakapo weza, kama utahitaji.
hiyo biblia unaiongelea hvyo kwasababu umezaliwa kwe familia ya kikristu ila km ungezaliwa saudi arabia leo hii ungekuwa muislamu na wala usingeichukulia biblia km unavyoichukulia sasa, lkn pia km ungezaliwa north korea ungekuwa unaamin iman nyngne kabisa kwa ile miungu yao ile na si hizi habari za mungu wa mbinguni, kimsingi km wazungu na waarabu wasingefika huku tungeendelea kuwa na tamaduni zetu na imani zetu za kiloko za mizimu n.k dini
 
Na kila kiumbe chenye kutumia akili yake kwa usahihi na kutafakari.
hapa unafanya kosa lingine

Unaanza kwa kusema kiumbe chake wakati bado hujakamilisha the whole process ya kuthibitisha, huoni kwamba hapo unafanya utapeli?

Hoja yako ilikuwa ya msingi zaidi endapo ulitanguliza uthibitisho ambao unaonesha dhahiri kua huyo mwenye hivyo viunbe ni kweli yupo
 
Unaanza kwa kusema kiumbe chake wakati bado hujakamilisha the whole process ya kuthibitisha, huoni kwamba hapo unafanya utapeli?
Wapi nimendika chake ? Uwe unasoma ibara kwa umakini kabla ya kujibu.

Pili,hakuna kinachobadilisha ya kuwa sisi sote ni wake na kwake tutarejea. Hii naiweka akiba tutaijadili kielimu penye haja.
 
Nimesoma hiyo post ambayo uneiita kuwa ndio jibu la kile nilicho kuuliza ninegundua mambo kadhaa

Swali lilikuwa lina hoji uhalali wa hicho chanzo

Baadaye ulipoonesha kwamba umejua kua huo msingi ndio chanzo kwasababu hakiruhusu msingi mwingine

Hapa niliuliza swali linalolenga kuhusu kupata uhakika wa akili yako uliyotumia kujua hilo jambo

Nikiwa na maana kwamba vipi kama akili yako ilitafsiri vibaya?

Au nije na mfano mwingine

Akatokea mtu mwingine hapa akaleta masimulizi ya dini nyingine kinyume na yako akasema mungu wake yeye ni chanzo kwasababu yeye ndio msingi na hakuna msingi mwingine unaoweza kuingia pale, utakubali?

Kumbuka ukikubali tafsiri yake mungu wako sio kitu, na ukikataa maana yake kumbe hata mtu akisema kilicho msingi hakuna msingi mwingine sio hoja thabiti ya kufanya kile kitu kiwe kama yeye anavyosema

Sasa vipi kama na wewe ni miongoni mwa watu wa namna hiyo?
 
Akili ya Mungu ipo juu sana.Kujaribu kumfikiria Mungu kwa akili iliyokata tamaa,ni sawa na mtoto mchanga kumfikiria baba kama mtu katili kwa vile hamnyonyeshi maziwa.

Mungu akurehemu sana,huenda ukakutana naye kwa urahisi kuliko sisi wengine ambao hatujafuta biblia kwenye simu zetu.Kwani sifa kuu ya Mungu ni Mungu mwenye REHEMA.
wote tunaishi dunia hiihii acha kuongea as if umewahi ishi sayari nyngine ukaona vitu vinginme ambavyo watu wa dunian hp hawajaviona, ww umehadithiwa au kusoma kwe biblia kuhusu habari za mungu lkn nje ya hapo hauna info zozote kuhusu mungu wala huwez kuprove chochote kuhusu yy, kimsingi km ungezaliwa kwe jamii ya kipagan nawe ungekuwa mpagan na usingejua au kuamin kuhusu mungu, ni vile tu wakolon na wafny biashara wa kiarabu walileta hizi dini ndio maana tunaongea hbr za mungu kinyume na hapo tungekua busy na imani za matambiko za babu zetu
 
Wapi nimendika chake ? Uwe unasoma ibara kwa umakini kabla ya kujibu.

Pili,hakuna kinachobadilisha ya kuwa sisi sote ni wake na kwake tutarejea. Hii naiweka akiba tutaijadili kielimu penye haja.
Tuseme "Kila kiumbe chenye kutumia akili" iwe ndo kauli mbiu ya dini zote kuelezea miungu yao

Ikiwa kila mmoja kwa nafasi yake anadai kila kiumbe chenye kutumia akili kitaweza kukubali uwepo wa mungu wake

Je hapo kigezo kitakuwa nini ili kupata ukweli wa kujua mungu wa kweli?
 
Nimesoma hiyo post ambayo uneiita kuwa ndio jibu la kile nilicho kuuliza ninegundua mambo kadhaa

Swali lilikuwa lina hoji uhalali wa hicho chanzo

Baadaye ulipoonesha kwamba umejua kua huo msingi ndio chanzo kwasababu hakiruhusu msingi mwingine

Hapa niliuliza swali linalolenga kuhusu kupata uhakika wa akili yako uliyotumia kujua hilo jambo

Nikiwa na maana kwamba vipi kama akili yako ilitafsiri vibaya?

Au nije na mfano mwingine

Akatokea mtu mwingine hapa akaleta masimulizi ya dini nyingine kinyume na yako akasema mungu wake yeye ni chanzo kwasababu yeye ndio msingi na hakuna msingi mwingine unaoweza kuingia pale, utakubali?

Kumbuka ukikubali tafsiri yake mungu wako sio kitu, na ukikataa maana yake kumbe hata mtu akisema kilicho msingi hakuna msingi mwingine sio hoja thabiti ya kufanya kile kitu kiwe kama yeye anavyosema

Sasa vipi kama na wewe ni miongoni mwa watu wa namna hiyo?
Kwani jibu halionyeshi uhalali wa hicho chanzo.

Hivi unajua hata hilo tamko "Msingi potofu" umekosea kulitumia ? Huwa nakwambia karibu kila mara,ukiwa unajadiliana na mimi hakikisha unajua matumizi sahihi ya maneno, sisi waswahili hatuna "msingi potofu" bali tuna "msingi mbovu" na tuna "imani potofu" huu ndiyo usahihi. Sasa tuachane na hilo.

Turudi katika jibu langu,nilikwambia ya kuwa "Hairuhusu kuingia kisicho msingo" hapa nimeonyesha uhalali wa kuingia kinacho husu msingi na uharamu wa kutoingia kisicho husu msingi. Kijana ongeza umakini.

Shukrani.
 
Tuseme "Kila kiumbe chenye kutumia akili" iwe ndo kauli mbiu ya dini zote kuelezea miungu yao
Sasa usiseme hivyo au usiwasemee hivyo sababu wengine matumizi ya akili si himizo katika dini zao.

Usiwe unajenga hoja kwa dhana unajipa uwanja mdogo sana wa kujadili mada husika.
Ikiwa kila mmoja kwa nafasi yake anadai kila kiumbe chenye kutumia akili kitaweza kukubali uwepo wa mungu wake
Rudi kwenye uhalisia kijana, wakina nani wengine wanasema haya ?s
Je hapo kigezo kitakuwa nini ili kupata ukweli wa kujua mungu wa kweli?

Swali lako la uongo sababu limejikita kwenye dhana.
 
Kwani jibu halionyeshi uhalali wa hicho chanzo.

Hivi unajua hata hilo tamko "Msingi potofu" umekosea kulitumia ? Huwa nakwambia karibu kila mara,ukiwa unajadiliana na mimi hakikisha unajua matumizi sahihi ya maneno, sisi waswahili hatuna "msingi potofu" bali tuna "msingi mbovu" na tuna "imani potofu" huu ndiyo usahihi. Sasa tuachane na hilo.

Turudi katika jibu langu,nilikwambia ya kuwa "Hairuhusu kuingia kisicho msingo" hapa nimeonyesha uhalali wa kuingia kinacho husu msingi na uharamu wa kutoingia kisicho husu msingi. Kijana ongeza umakini.

Shukrani.
Umetumia maelezo mengi kunikosoa kiswahili changu, ila maelezo mengi niliyoyaandika kuelezea hoja yangu umeyapa majibu ya shorcut

Point yangu ni hiyo aware uliyopata na kusema hairuhusu kisicho misingi, una hakika gani kama upo sahihi na sio kwamba umepotoka?

Na ndio maana nimekuwekea mfano hapo

Kwamba akija mwingine akaweka madai yake na kusema kwamba madai hayo ni ya kweli na ni sahihi kwakua kitu hicho alichokidai hakiruhusu kuingia kisicho msingi, utakubali kua ni kweli?

Ukikubali kua ni kweli tafsiri yake ni kwamba mungu wako ni wa uongo

Na ukikataa tafsiri yake ni kwamba ishu ya kusema "hairuhusu kisicho misingi" kumbe sio kigezo cha kufanya jambo hilo au madai hayo yawe ya kweli
 
Unakumbuka huko nyuma nilikuuliza kama unajua maana ya tamko msingi ? Ila hili swali hukulijibu, aisee uwe unajitahidi kujibu maswali kuepuka kukosea kama unavyokosea.

Unajua maana ya tamko msingi ?
 
Sasa usiseme hivyo au usiwasemee hivyo sababu wengine matumizi ya akili si himizo katika dini zao.

Usiwe unajenga hoja kwa dhana unajipa uwanja mdogo sana wa kujadili mada husika.

Rudi kwenye uhalisia kijana, wakina nani wengine wanasema haya ?s

Swali lako la uongo sababu limejikita kwenye dhana.
Kwamba una maanisha watu wenye matumizi sahihi ya akili ni wale wanaokubaliana na mungu wako?

Kuna dini gani ambayo unaona inajinasibu kwamba inahitaji wasiokuwa na akili ili kumjua mungu wao?
 
Unakumbuka huko nyuma nilikuuliza kama unajua maana ya tamko msingi ? Ila hili swali hukulijibu, aisee uwe unajitahidi kujibu maswali kuepuka kukosea kama unavyokosea.

Unajua maana ya tamko msingi ?
Nijuze
 
Back
Top Bottom