matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Mambo yanaenda kasi sana.
Ujuzi ndio kila kitu.
1: Dogo wa kwanza anatengemeza Website, Apps, Systems, na projects zake kama akipata connections ninza mamillioni. Kama haitoshi huwa anawafanyia projects wanafunzi wa mwaka wa mwisgo wa chuo. Huyu anajituma sana, huwa anaingia maktaba ya taifa kujisomea siku nzima vitabu vya ujuzi kwa PC yake.
2: Dogo mwingine, fundi umeme tu lakini yuko updated sana. Nilipomuona nikajua ni kajizi. Mdogomdogo lakini nilipompa connection ya kuweka umeme nyumba flani kubwa. Peke yake na kibarua wake walifanya kazi kubwa kwa ubora usio wa kawaida.
3: Huyu mwingine ndio balaa. Ni muimba kwaya tu, ukimuona kwa bodi la nje ni mdogo unaweza kumpuuza. Ila ni fundi gwiji wa masuala ya vioo. Nyumba bora na kubwa mtaani yeye ndio kaipiga finishing vioo na balcon. Mwanzoni nilijua ni kampuni maana hiyo nyumba mtaani tulidhani ni ya waziri kwa jinsi ilivyo kubwa nzuri na ya kisasa (ghorofa). Nilipombishia akanionyesha miamara ya mpesa ya kazi zake anatumiws pesa nyingi ndogo ni 3M na mabosi wake mikoani kote.
Kwa haraka nimewaona wengi sana wenye degree na wasio na degree. Mwingine nimemuona kwenye kampuni kubwa ya kimataifa mdogo kuliko wote ila ni meneja mkuu wa idara ya fedha (ni msomi). Anakalisha wazee na watu wa makamo wote wanamtetemekea.
Nilichojifunza
1: Wote hawa watu wanyenyekevu sana, hawanamajivuno wala makuu.
2: Ni watu waaminifu sana. Unaweza kuwatumia hata 10M ukasubiri kazi na kwa wakati ukafanyiwa kila kitu.
3: Ni wepesi sio wazito wala hawajivutivuti.
4: Nimeona hawa ni kama sisi tu ila sisi wazazi walitupiga marufuku kujihusisha na biashara na ubunifu na michezo kwa kigezo tutakuwa wajinga darasani. Elimu ilitakiwa ibaki yenyewe bila kubughuziwa na chochote.
Kimsingi hawa madogo nimewakubali sana. Taifa likijielekeza kwenye kuwajengea uwezo wa kiujuzi zaidi kuliko makaratasi.