Nimeguswa na wale wananchi waliookoa watu ajali ya ndege

Uwanja wa ndege upo ziwani kabisa hivyo kukosekana hata boti moja ya dharura
Na mkoa umezungukwa na nchi jirani, ina maana hakuna Police Boat ya ku patrol
Usalama wa wakazi wa Kagera upoje? Kuna bandari pale hakuna Boat?
Je tunapswa kuamini kuwa pale uwanjani hakuna kikosi cha zimamoto na uokoaji?
Ningependa kumsikia mkuu wa kitengo cha maafa, Mh Waziri Mkuu.
Ajali ya MV Bukoba hadi ajali ya hii ndege kwenye ziwa hilo hilo, serikali ya CCM haijajifunza wala kuwa tayari kubadilika kwenye sekta ya uokozi na dharura.
Kuna ajali ya MV Nyerere miaka michache na kila siku zinatokea! hatujifunzi tunaadhimisha siku ya May 21 kwa kumbu kumbu , mapambio. Hatuna cha kujifunza.
Kimsingi tumewekeza kununua mitambo imara kuiwezesha TCRA kuwafuatilia wananchi wanaoikosoa serikali kuliko kuweka mazingira na miundombinu wezeshi kwenye matukio kama haya.
Yes, kwasababu neno ' priority na public interest' hayapatiwa misamiati ya kiswahili
Tumeaibika sana jana kama nchi endapo hiyo video ya ajali na maelezo yake vikisambazwa duniani.


Kwa hili Mh Waziri Mkuu ajitathmini! kuna kushindwa kwingine ni kuboronga! PM Jitathmini
 
Haya yote uliyo yaongea hayana nafasi kwa nchi hii labda kama unaongelea nchi nyingine,

Nchi hii majanga mengi huwa yanatatuliwa na wananchi wenyewe wala sio hao wataalamu wako unao wasema na isingine kuwa jitihada za wananchi hata maafa ya MV bukoba yangekuwa mara 1000 ya yalivyo tokea

Na hata hilo la ndege ukisubiri hao waokoaji wako unao sema wana ujuzi wakati mimi nawaona hawana lolote maafa yangekuwa zaidi ya mara 100

We angalia hata majanga ya moto mara nyingi msaada mkubwa hutoka kwa wananchi acheni kujifanya kama mnaishi nchi za Scandinavia wakati mpo kwa wala mihongo huku kwa mtogole
 
Ulaya gani wewe..tumia akili bwana, hivi kusubiri polisi wafike kwenye tukio ni mambo ya ulaya..
Sidhani kama uko serious ..au la una addiction ya kuangalia movie..kwa tukio la jana unasubiriaje vifaa vya uokozi mkuu? Unajua maji within few sec you are finished?hebu tupumzishe
 
Sikuombei ila natafakari utajisikia vp ukipata ajali au watu wako wa karibu wakipata ajali utajiskia vipi ukikuta Raia wamesimama pembeni na smartphone zao wana chart wakiwa wanasubiria Wataalam wenye ujuzi wa kuokoa ambao nao muda huo wapo kwny maofisi wabakimbizana wapate posho za safari kabla ya kuanza safari
 
Nchi no one cares...sisi wakazi wa Bukoba tushajichokea na serikali zetu hiz...

Mfano mji wa Bukoba una matatizo kibao...mfano barabara kuu inaoingia mjini ina njia mbili na ina miteremko mkali sana...na ajali zinatokea mara kwa mara...serikali toka miaka ya 90 inasema itaipanua na kuwa njia nne hadi leo wako upembuzi yakinifu[emoji2]..
Mji wa bukoba barabara zake ni finyu, mji haunaga stendi toka uhuru...
Uwanja wa bukoba haunaga taa, ni mfupi na uko karibu na makazi ya watu..no one cares...
 
Wala usiwe na shaka, tunapendana sana. Aliyetaka na aliyepanda mbegu kutugawa na kutufarakanisha keshatangulia.

JokaKuu Pascal Mayalla
Bado yupo mkuu. mkubwa wao ni utandawazi bora kidogo hata siasa maana unawezashitka kwamba unatumiaka kukamilisha mission za watu wengine.

Utandawazi umefanya watu tuwe wachoyo. Na ukiwa mchoyo huwezi kusaidia mtu mwingine. Eti leo hii huwezi kumtembelea ndugu mpaka umpe taarifa akuwekee bajeti, haya ni mambo ya kuiga kutoka kwa washenzi wanaoiharibu dunia. Huo ni mfano tu. Kuna mengi sana ya kutisha yatokanayo na utandawazi ambayo yamefanya wanadamu tuwe makatili wa kutisha na tusipendane.
 
Yaani wewe kolo, unasema wawasubiri wataalam?. Watoke wapi hao wataalam?, Dar au wapi!, Hao wataalam unaosema wanachojua wao ni kubwa simu zao za Smart phone, alafu kuelezea maelezo meengi waliojifunza darasani wakati watu wanaendelea kufa. Lakini wavuvi au wananchi hawana hizo hadithi, wao ni kuokoa kinachowezekana kuokolewa. Shukuru wavuvi kuwatoa hao 26, tungewasubiri hao wataalam, tungeokoa 0. Waache watanzania wajilee na kusaidiana, Suala la utaalam waachie Marekani.
 
Serikali iwape hata medali za heshima.
 
Yaani huyu jamaa sijamuelewa, yaani amejitia sana ujuaji
 
Ushauri wa kiboya sana, kwa hiyo wavuvi wangesubiri uokozi kwa kusubiria wataalam na vifaa toka GGM na kagera sugar?

Kuna mtu angenusurika?

Je tuna team gani ya uokozi?

Tanzania ni yatima wenyewe wanahudumiana wazazi na viongozi ni wafu kiutendaji
Akikujibu nitagg mkuu
 
Huyo jamaaa ni empty kichwani
 
Na bado wakifika wanaweza fika mikono mitupu.
Yaani nimepata ajali Muda wowote chombo chaweza zama ati unaona watu wapo pembeni wanawashangaeni wakisubiri waokozi wafike.πŸ˜‚
 
Huo uwanja uitwe airstrip tu, maana hata zimamoto zingeweza saidia vuta kuliko kutumia binadamu...

Kiufupi tumeaibika kama taifa
 
Hii ndege ingedondoka kati kati ya hilo ziwa hao watu tungesubiri msaada wa marekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…