Tulichoambiwa na Waziri Mahiga ni kwamba Tanzania ilishaamua haitasaini huo mkataba. Na sababu zikaainishwa. Kwahiyo mama hapa unatuambia kuwa, tulikuwa tumekurupuka, tumetulizwa na wenzetu, tujitafakari mpaka January ndo tuje na uamuzi mwingine.
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?
Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?
Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
kama Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wamesaini basi huo mkataba utakuwa uko vizuri tu make hao wawili ndo marais wenye bongo safi na zinazochemka ukanda huu
Ingawa wamesaini kabla raisi Magufuli hajaingia Ikulu.
haibadirishi mkataba, mkataba ni uleule
Mkuu, kumbuka mikataba yote ambayo ilikuwa ikisainiwa huko nyuma na hatukusikia mawaziri wetu wakisema wanataka muda ili kuipitia.
Unaweka kukumbuka mkataba hata mmoja ikianzia Buzwagi?
Ni kweli, Tanzania itajengwa na Rwandawewe nishakuambia ukiona kagame kasaini jua huo na mkataba swafi, we ushaona kwa kagame kuna mikataba ya kibuzwagibuzwagi.
Hii ni zaidi ya hivyo mkuu.Hatuna cha kuuza Ulaya. Kenya wanauza sana maua na mboga sasa sisi tusaini tuuze nini? Uliza ile ya USA inaitwa AGO kama kuna tunacho uza
Kwani EPA ni mkataba wa kibiashara unaohusisha ukanda na ukanda? Au race na race?Lakini hao wanaouza huko Ulaya ni wazungu wakenya wenye connections.
Mwafrika hapati kitu hapo.
Inferiority complex ya kiwango cha lamikama Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wamesaini basi huo mkataba utakuwa uko vizuri tu make hao wawili ndo marais wenye bongo safi na zinazochemka ukanda huu
Wanarudia kuutizama? Au wanawasubiri wasiosaini kwa vile ni mkataba kati ya union na union na sio single countries?Ulukolokwitanga: Huna la kujadili ila hoja ya kupinga pasipo na ushahidi kwamba suala la EPA halijafanyiwa utafiti! Du, wewe utafiti umejifunzia wapi!
Kwa kifupi utafiti wowote ni lazima ukubaliwe na watafiti wengine, na wakati mwingine, matokeo ya utafiti mmoja huweza kubatilishwa na tafiti zingine. Kwa hili la EPA mbali na kufanyiwa utafiti lazima likubalike na nchi zote husika. Kwa taarifa ya mtoa mada, Mama Anna, tayari Uganda na Rwanda walikuwa wametia saini. Hivyo kuwaaminisha hadi wakerejea kuutizama upya ni hatua kubwa.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Vizuri Mama wa HeshimaLeo wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.
Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.
Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.
Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.
Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara.
Nz vipi kuhusu mikataba mibovu na ya siri ambayo serikali imekwisha sign kwa mfano ya madini na Richmond?Anna Mghwira,
Ni kweli kwa hili namuunga mkono Magufuli japo sikubaliani na mambo yake mengi. Sasa kwenye hili inabidi atumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha anapitia mikataba mingine nchi iliyoingia huko nyuma ili kuona kama ina faida kwa nchi au ilisainiwa na 10%.
Kwa mara ya kwanza nimeona nchi yetu ikisimama kidete dhidi ya mikataba inayotengenezwa ulaya huku ikivalishwa vazi la nia njema.
Sasa tuhakikishe tunapinga mikataba hii lakini tuhakikishe tunajitahidi kujikwamua na hali hii ya kutegemea bidhaa toka nje kwani ninavyojua kuna uwezekano wa nchi hizi za Ulaya kuanza kutupa wakati mgumu.
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?
Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?
Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
Kamwe hatutasaini..LOL!!
..lakini sisi tulisema HATUTASAINI na mkataba huo UTATUUMIZA KIUCHUMI.
..and it took us a long time to arrive at that decision.
..tukibadili uamuzi huu basi Tz itakuwa " imeonyeshwa njia."
..zaidi tutakuwa tumekubali KUONGOZWA NA KUSALIMU AMRI KWA NCHI MAJIRANI.