Nimeibiwa milioni 5 Stendi ya Mabasi ya Magufuli

Ujinga mtupu, sasa unalia nini wakati obviously hauko serious na maisha. Au ulitaka tujue unamiliki Toyota crown
 
Millioni 5 unaweka kwenye briefcase kweli? Huoni kama brifcase liliamua kukataa udhalilishaji uliolifanyia? Hii nchi uhuru umesidi sana.
 
Chai hii
 
Kwa iyo ulisahau Ile kauli ya abiria chunga mzigo yako kweli wafwa
 
Daaah hakuna hata zawadi nono kwa atakae kuletea.
 
Pole .Hukiwa na kiasi kikubwa Cha pesa husijiamini kuwa nacho na kusafiri nacho Ni kosa kubwa kwani dunia Ina Mambo mengi Sana jitaidi uwe na pesa soft siyo cash maana hizo Zina usalama.Pole sana
 
Ndo ukubwa
 
Ila wee jamaa unajua kutupanga sana. Au kuna mashindano ya nyuzi humu JF tuambizane fasta.
 
Pole sana, next time usitembee na maburungutu(cash).
 
Nimepoteza dakika zangu 5 kumuonea huruma, kumbe ni choko tu! Pambavu.....
 
Kwanini unahisi ni karma? Kuna Jambo gani baya ulishawahi kufanya?
NOTE: Karma is real
 
Huo ni uzembe.. kiwango cha pesa chochote kikizidi elfu 50 hutakiwi kitembea nacho.. wewe 5M unatembea nayo are you serious?

Nawapomgea waizi kwa ujanja waliotumia...mungu awajalie huko walipo wafanye vitu vya maendeleo
 
huku ni JF kwa magreat thinkers.
watu wameshamshtukia huyu jamaa ni mwongo. mara aanzishe thread ameacha kazi, mara aseme anatafuta mume, tisa kumi kwenye hii thread yake anasema alikuwa na mkewe halafu kaibiwa pesa za kazini.

yote kwa yote, tunaburudika.
 
Pole sana mkuu. Siku nyingine uwr unakumbuka kufunga vizuri milango ya gari, sio wakati wa kupaki tu, hata wakati ukiwa unaendesha barabarani, ni vizuri kwa usalama wako na mali zako zilizo ndani ya gari.

Kwakuwa hiyo gari ni ya kwako, uza hiyo gari, hela utakazopata, toa hapo hiyo 5m ukalipe ofisini halafu chenji utakayobaki nayo nunua gari nyingine ndogo kama vitz au corolla, ikusaidie kwa usafiri.

Kila la kheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…