Nimejisikia uchungu sana nyimbo za taifa zilipopigwa wakati mechi kati Kili Stars vs Zanz Heroes inaanza

Nimejisikia uchungu sana nyimbo za taifa zilipopigwa wakati mechi kati Kili Stars vs Zanz Heroes inaanza

Maswali yafuatayo ndiyo yamenitoa machozi.

Nimejiuliza kwamba:

1. Kumbe haya ni mataifa 2 tofauti? Kila moja lina katiba yake, wimbo wake, jeshi lake na rais wake?

2. Kwahiyo hivi Sasa Tanganyika inaongozwa na raia wa kigeni??

Hilo swali la 2 ndiyo limeniumiza zaidi.
Nenda kajifunguwe tatizo lenu watanganyika ni vichwa maji siku zote kwenye michezo ya CECAFA tukikutana na machogo huwa hivyo ndio kwanza wewe Leo ushuhudie Wacha ushambaaa
 
Sema Nyerere aliwaza nini...kwa Karume it was very clear alitaka muungano wa federation huku kila nchi ikibaki na utawala wake wa ndani....

On the contrary, Nyerere aliwaza kuimeza Zanzibar iwe mkoa kama vile katavi au Geita ya leo...ili kuhalalisha hilo akaua tanganyika kwanza on the hope ingekuwa rahisi kuiua Zanzibar later on....

Infortunately for him, mambo yakaenda kombo and here are...almost miaka 60 ya muungano wenye manung'uniko kibao!

Wazanzibar wanaupenda huu mfumo wa muungano kwa vile unawafaidisha wao zaidi ......!!
 
Maswali yafuatayo ndiyo yamenitoa machozi.

Nimejiuliza kwamba:

1. Kumbe haya ni mataifa 2 tofauti? Kila moja lina katiba yake, wimbo wake, jeshi lake na rais wake?

2. Kwahiyo hivi Sasa Tanganyika inaongozwa na raia wa kigeni??

Hilo swali la 2 ndiyo limeniumiza zaidi.
Tanganyika iko wapi?
 
Maswali yafuatayo ndiyo yamenitoa machozi.

Nimejiuliza kwamba:

1. Kumbe haya ni mataifa 2 tofauti? Kila moja lina katiba yake, wimbo wake, jeshi lake na rais wake?

2. Kwahiyo hivi Sasa Tanganyika inaongozwa na raia wa kigeni??

Hilo swali la 2 ndiyo limeniumiza zaidi.
una hoja nzito na chungu sana
 
Tatizo kubwa ni watanganyika wengi ni wavivu wakuhoji mambo ya msingi. Watanganyika ni wapole sana. Hivi Kuna mtu aliwahi kuwaza kwanini, tupokezane uongozi kati ya Zanzibar na Tanganyika, kwanini Rais wa Tanganyika ni Rais wa Muungano, kwanini wazanzibar wanapewa uwaziri bara wakati mtanganyika hapati hata udiwani Zanzibar. Kwanini ukinunua bidhaa Zanzibar unakatwa Kodi ya Zanzibar ukija bara unalipa Tena, mzanzibari akinunua bidhaa Dar akilipa Kodi akifika Zanzibar haikatwi Tena. Kimsingi huu Muungano unatunyonya sana watu wabara.
 
Maswali yafuatayo ndiyo yamenitoa machozi.

Nimejiuliza kwamba:

1. Kumbe haya ni mataifa 2 tofauti? Kila moja lina katiba yake, wimbo wake, jeshi lake na rais wake?

2. Kwahiyo hivi Sasa Tanganyika inaongozwa na raia wa kigeni??

Hilo swali la 2 ndiyo limeniumiza zaidi.
Daaaa! Nimesikitika pia
 
Ukipenda boga penda na ua lake, huu muungano ni tunu na una faida zake kibwe a ila sasa tatizo tumelea ushubwada mwingi ambao unaleta ukakasi kwenye mbivu tuliyonayo
 
Maswali yafuatayo ndiyo yamenitoa machozi.

Nimejiuliza kwamba:

1. Kumbe haya ni mataifa 2 tofauti? Kila moja lina katiba yake, wimbo wake, jeshi lake na rais wake?

2. Kwahiyo hivi Sasa Tanganyika inaongozwa na raia wa kigeni??

Hilo swali la 2 ndiyo limeniumiza zaidi.
Siku nyingine beba hata tenga la nyanya Nenda nalo Zanzibar ndio utajua hii nchi Moja au nchi 2
 
Maswali yafuatayo ndiyo yamenitoa machozi.

Nimejiuliza kwamba:

1. Kumbe haya ni mataifa 2 tofauti? Kila moja lina katiba yake, wimbo wake, jeshi lake na rais wake?

2. Kwahiyo hivi Sasa Tanganyika inaongozwa na raia wa kigeni??

Hilo swali la 2 ndiyo limeniumiza zaidi.
Huwa najiuliza pia,Cjui Zanzibar huwa wanafanya hvyo kuwakumbusha watanganyika wao ni nchi huru na hawajamezwa,sababu hakukua na ulazima wa hzo nyimbo mbili kupigwa kama tuna nyimbo moja ya Taifa.
 
Mtsnganyika huruhusiwi
1. Kugombea cheo chochote kule visiwani, hata uenyekiti wa mtaa. Wao rukhusa kugombea Tanganyika mpk urais.

2. Kumiliki ardhi hata ya kujenga FREMU.
Lkn wao rukhusa mpk kumiliki mamilioni ya ekari.
Dah watanganyika tuamke. This is day light robbery kwa taifa letu.
 
Wimbo wa taifa wa huko upoje. Mwenye mashairi yake aweke hapa tuuimbe kidogo.

Na kama wameimba wimbo mmoja basi labda waliimba kwaajili ya ufunguzi tu.
 
Tatizo kubwa ni watanganyika wengi ni wavivu wakuhoji mambo ya msingi.
Hii ni hoja muhimu sana ndiyo maana wapo wanaohoji kwanini tunaonyesha matundu ya Muungano.
Hakuna Mtanganyika anayehoji kuhusu uwepo wa Taasisi mbadala kila upande na kwamba kwanini iwe hivyo.

Majuzi tu Katibu wa CCM wa Zanzibar kaweka mambo hadharani, kwamba, Rais SSH alipoingia ameongeza pesa kutoka asilimia 4.5% iliyokuwepo hadi 9% ya Bajeti ya JMT. Ikumbukwe kwamba Zanzibar inapata mgao wake iwe Mikopo au misaada, na kwamba Zanzibar haichangii mapato ya JMT kwa njia yoyote ile.
Hivyo 9% ya Bajeti ya JMT ni kodi za Watanganyika na mapato ya rasilimali za Tanganyika.

Kwa Bajeti ya JMT kama sikosei ni 49T. Ukiwapa Zanzibar 10% ni sawa na 4.9T. Bajeti ya Zanzibar ni 2.8T.
Kwa maneno mengine Bajeti ya SMZ ni karibia nusu ya Pato kutoka Tanganyika.

Ni kwa msingi huo, utaona SMZ inafanya makubwa kuliko Bajeti yake ikiwemo kulipa pensheni Wazee

Bajeti ya SMZ haIna mahali mradi wa uwanja umetajwa. Kiasi cha takribani 50B ni kikubwa kutoonekana katika Bajeti.

SMZ wanaojenga Viwanja hawana uwezo wa kulipa TANESCO! Real!! wakasamehewa 60B deni lililokuwepo tangu Kikwete hadi Magufuli, halafu tunalaumu Tanesco kwa utendaji hafifu.

Bilioni 60 zilizosamehewa ni pesa ambazo ima ni hasara kwa shirika au kama zitalipwa ni kwa kodi za Watanganyika.


Watanganyika ni wapole sana.
Hapana ni kutokuelewa, na sijui kama wana uchungu na nchi yao.
Hivi Kuna mtu aliwahi kuwaza kwanini, tupokezane uongozi kati ya Zanzibar na Tanganyika, kwanini Rais wa Tanganyika ni Rais wa Muungano, kwanini wazanzibar wanapewa uwaziri bara wakati mtanganyika hapati hata udiwani Zanzibar. Kwanini ukinunua bidhaa Zanzibar unakatwa Kodi ya Zanzibar ukija bara unalipa Tena, mzanzibari akinunua bidhaa Dar akilipa Kodi akifika Zanzibar haikatwi Tena. Kimsingi huu Muungano unatunyonya sana watu wabara.
Ndiyo maana Tanganyika inatakiwaili ijisimamie, isimamie shughuli na rasilimali zake kama ilivyo Zanzibar.

Kama Muungano unahitaji, waulizwe Wazanzibar! Watanganyika hawana cha kupata zaidi ya kupoteza.

Yes tunapoteza kwasababu tunatumia rasilimali nyingi kwenda eneo lisilo na mchango au msaada woeote.

Zanzibar wana serikali na uwezo wa kukusanya kodi , mapato ya rasilimali zao n.k., wanaweza kusimama wenyewe.
Tuelekeze rasilimali zetu kunakohitajika ambako kutatusaidia kuchangia pato la Taifa.

Tuna mikoa michanga kama Simuyu, Njombe n.k. yenye watu wengi na maeneo makubwa kuliko Zanzibar, hii inahitaji kuangaliwa kwa rasilimali za Tanganyika. Hilo litawezekana tukiwa na uongozi wa Tanganyika, utakaosimamia rasilimali za Tanganyika kwa wivu na uchungu.
 
Kuna mambo yanayostaajabisha katika Muungano kwa bahati nzuri au mbaya Watanganyika hawayajui.

Kwa muda mrefu Wazanzibar waliaminisha Umma Tanganyika imevaa koti la Muungano na kuwanyonya.
Hoja imedadavuliwa na kuonekana ni ya kijinga na kipuuzi ikienezwa na watu wasio na Elimu, hata wenye elimu.

Kuvaa koti la Muungano ni hasara kwa Tanganyika. Rasilimali kila pato la Tanganyika limefanywa la Muungano.

AFCON Pamoja Bid ni kazi ya TFF wakishirikisha Kenya na Uganda. Waliokwenda Cairo ni Waziri wa Tanganyika na viongozi wa TFF. Gharama zote za maandalizi ya ' Pamoja Bid' zilibebwa na Walipa kodi wa Tanganyika

Ni haki AFCON kuchezwa viwanja vya walipa kodi wa Tanganyika katika miji yenye Viwanja kama Arusha na Mwanza
Ujanja umetumiwa , kwamba AFCON ni Bid ya Tanzania na hilo jina linatoa uhalali wa Zanzibar kuwa mshiriki.

Chama cha Mpira Zanzibar ni cha nchi jirani. Mchezaji kutoka Tanganyika anapewa hadhi sawa na yule wa kutoka Cameroun, India au Moldova. Katika mazingira hayo ushirika wa Tanganyika na Zanzibar AFCON unatoka wapi?

Ni utamaduni ule ule wa Wazanzibar kuzuia hata ndizi kwa kudai zinatoka Tanganyika. Katika mazingira ya kustaajabisha ni Wazanzibar hao hao wanaosema ikiwa sisi ni Tanzania kwanini wao wasiingize bidhaa bila kodi Tanganika! Wameruhusiwa sasa hivi uchochoro wa bidhaa kutoka nje ni kupitia Zanzibar! hatupati kodi za kutosha

Ni utamaduni ule ule wa kudai Uhamiaji ni chombo cha pamoja, lakini maduhuli na kila pato linalotokana na huduma kule Zanzibar linabaki Zanzibar. Malipo ya mishahara ya Wafanyakazi wa Uhamiaji Zanzibar yanatoka Tanganyika. Kwamba, tunalipa Wazanzibar wakusanye kodi !

Ni uhuni ule ule wa kuchukua fedha za kodi za Tanganyika kwenda kwenye kinachoitwa mfuko wa Jimbo.
Huko Zanzibar kuna Wwawakilishi na serikali yao, kwanini mfuko wa jimbo utoke Tanganyika?

Uhuni ule ule wa kodi zetu za simu kwenda Zanzibar kwasababu wanatumia 255. Kwanini wasipewe 259 yao!
Tanganyika haipotezi chochote kwa Zanzibar kuwa na country code yao, wapewe. Kuchukua kodi zetu si sahihi

Kuna mambo mengi sana ya kushangaza, akina Mwigulu na Mpango wanajua, ni washiriki
Wabunge wanajua lakini ni mwiko kuitetea Tanganyika! wanaruhusiwa kusema Mbowe akitoa kauli tu.

Ipo siku watu wote wanaoihujumu Tanganyika tutawauliza. Kazi moja tu tunayo, Kuirejesha Tanganyika.

Kama Muungano utahitajika si suala la Tanganyika, Waulizwe Wazanzibari.
 
Back
Top Bottom