Tatizo kubwa ni watanganyika wengi ni wavivu wakuhoji mambo ya msingi.
Hii ni hoja muhimu sana ndiyo maana wapo wanaohoji kwanini tunaonyesha matundu ya Muungano.
Hakuna Mtanganyika anayehoji kuhusu uwepo wa Taasisi mbadala kila upande na kwamba kwanini iwe hivyo.
Majuzi tu Katibu wa CCM wa Zanzibar kaweka mambo hadharani, kwamba, Rais SSH alipoingia ameongeza pesa kutoka asilimia 4.5% iliyokuwepo hadi 9% ya Bajeti ya JMT. Ikumbukwe kwamba Zanzibar inapata mgao wake iwe Mikopo au misaada, na kwamba Zanzibar haichangii mapato ya JMT kwa njia yoyote ile.
Hivyo 9% ya Bajeti ya JMT ni kodi za Watanganyika na mapato ya rasilimali za Tanganyika.
Kwa Bajeti ya JMT kama sikosei ni 49T. Ukiwapa Zanzibar 10% ni sawa na 4.9T. Bajeti ya Zanzibar ni 2.8T.
Kwa maneno mengine Bajeti ya SMZ ni karibia nusu ya Pato kutoka Tanganyika.
Ni kwa msingi huo, utaona SMZ inafanya makubwa kuliko Bajeti yake ikiwemo kulipa pensheni Wazee
Bajeti ya SMZ haIna mahali mradi wa uwanja umetajwa. Kiasi cha takribani 50B ni kikubwa kutoonekana katika Bajeti.
SMZ wanaojenga Viwanja hawana uwezo wa kulipa TANESCO! Real!! wakasamehewa 60B deni lililokuwepo tangu Kikwete hadi Magufuli, halafu tunalaumu Tanesco kwa utendaji hafifu.
Bilioni 60 zilizosamehewa ni pesa ambazo ima ni hasara kwa shirika au kama zitalipwa ni kwa kodi za Watanganyika.
Watanganyika ni wapole sana.
Hapana ni kutokuelewa, na sijui kama wana uchungu na nchi yao.
Hivi Kuna mtu aliwahi kuwaza kwanini, tupokezane uongozi kati ya Zanzibar na Tanganyika, kwanini Rais wa Tanganyika ni Rais wa Muungano, kwanini wazanzibar wanapewa uwaziri bara wakati mtanganyika hapati hata udiwani Zanzibar. Kwanini ukinunua bidhaa Zanzibar unakatwa Kodi ya Zanzibar ukija bara unalipa Tena, mzanzibari akinunua bidhaa Dar akilipa Kodi akifika Zanzibar haikatwi Tena. Kimsingi huu Muungano unatunyonya sana watu wabara.
Ndiyo maana Tanganyika inatakiwaili ijisimamie, isimamie shughuli na rasilimali zake kama ilivyo Zanzibar.
Kama Muungano unahitaji, waulizwe Wazanzibar! Watanganyika hawana cha kupata zaidi ya kupoteza.
Yes tunapoteza kwasababu tunatumia rasilimali nyingi kwenda eneo lisilo na mchango au msaada woeote.
Zanzibar wana serikali na uwezo wa kukusanya kodi , mapato ya rasilimali zao n.k., wanaweza kusimama wenyewe.
Tuelekeze rasilimali zetu kunakohitajika ambako kutatusaidia kuchangia pato la Taifa.
Tuna mikoa michanga kama Simuyu, Njombe n.k. yenye watu wengi na maeneo makubwa kuliko Zanzibar, hii inahitaji kuangaliwa kwa rasilimali za Tanganyika. Hilo litawezekana tukiwa na uongozi wa Tanganyika, utakaosimamia rasilimali za Tanganyika kwa wivu na uchungu.