Nimekata tamaa, nimepigika, nimeteswa, nimedharauliwa, nimeumizwa, sasa basi!

Nakubaliana na mleta mada follow your heart, sometimes inner peace inakuja kwa kufanya kile nafsi inataka. Ingawa ni bora zaidi angeangalia ni vitu gani vya kufanya ambavyo havitakua na madhara kwake pamoja na wapendwa wake
 
Pole Sana..kukata tamaa si suluhu..mshirikishe Mungu kwa kila gumu upitialo na linalokukatisha tamaa..Anza upya.
 
Kamba sili ila natafuta furaha na mimi nimechoka.
Raha jipe mwenyewe ndugu yangu.

Pia ukisaidia ndugu au hata rafiki usisubiri shukrani, sema tu yatosha na songa mbele na maisha yako, jihudumie kula vizuri, vaa vizuri ikibidi kuwa selfish kidogo usisubirie sijui mke au Mama au ndugu aone au athamini umuhimu wako!!
Kazini unaweza stepdown kwenye hicho cheo ikawa mtumishi wa kawaida ili kuirudisha furaha yako maana umesema kazi yako Ina mshahara mzuri.
Kumbuka furaha yako haitoki kwa mtu mwingine zaidi yako!
Almsiki.
 
Siku utakayoanza kuamini kuwa wewe ndiye mtu pekee anayeweza kukupa furaha ndiyo siku ambapo tatizo litaanza kutatuka, asante.
 
Ni kama vile umesoma mawazo yangu!! Ushauri wangu ni kama wako kwa 90%!
 
Sasa wewe unawasomesha wadogo zako, wazazi wako wanafanya shughulo gani?
 
Pole sana mkuu, ila huko unakotaka kukimbilia ndo kutakumaliza kabisa..Kujipa furaha sio kunywa pombe, kuvuta sigara wala kulala kwenye madanguro. Unaongeza matatizo juu ya matatizo. Ishi maisha yako sasa, wakupende wasikupende sawa..Endelea kutenda wema ila wema usizidi sana.
 
Vita iko ndani ya familia yako kabla ya kutoka nje, ndugu zako uliowapa msaada walikuwa wanakupa heshima kwa sababu walikuwa hawana kitu..ila sasa wanakitu, kwa hiyo vita iliyopo ni wao kutaka kuonekana wananguvu zaidi kuliko wewe....wanatafuta nguvu ya kutambulika ndani ya boma (hii ni asili ya binadamu). Si ajabu walishaenda kuongea kwenye mavibuyu ndio maana mambo yako yote yanaenda kinyume; na hii changamoto inawakuta watu wengi....chunguza baadhi ya familia utajifunza kitu. Cha kukushauri, fanya maombezi kama wewe ni wa maombezi n.k
 
Jiarbu kufany research utaona kabsaa ww unanafuu kuna wat wana huzin kila siku ila awakati tamaa kama ww
Kumbuka
 
πŸ‘
 
Kwenye introductio n nimeelesa hilo. Hata hivyo siwezi kueleza yote. Machache nimesema kwa sababu ya stress tu.
Sasa wewe unawasomesha wadogo zako, wazazi wako wanafanya shughulo gani?
 
Well
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…