Nimekutana na Basi "Made in Tanzania", hongera Rais Samia Suluhu

Gari inatengenezwa kwa siku 70?

Acha utoto wewe. Toa sifa kwa rais anaestahili. Heko Hayati JPM.
 
Acha kujipendekeza. Samia kaingia juzi tu anahusikaje na utengenezaji wa hilo basi? Badala ya kupongeza wabunifu na watengenezaji unapongeza wanasiasa wasiojua A wala Z

Sent from my TECNO P701 using JamiiForums mobile app
 
fala sana,Kwa hiyo Samia kaunda hilo basi?! halafu hapo wametengeneza basi au bodi?kama ni bodi mbona hata Katavi wanaunda?
 
Unapata shida kuelewa nini wakati wewe ni mkongwe hapa nchini?

Hujui Rais akisema Tanzania ya Viwanda ndo inatokea? Akisema Tanzania ya Bata inatokea pia?
hivi huwa mnajipa muda wa kutumia akili kabla hamjaandika humu?
 
Viwanda vyote vya magari duniani huwa ni assemblers tu. Wanasource vifaa mbalimbali vya magari kutoka kwa watengenezaji mbalimbali. Injini kutoka kwa huyu na suspension system kutoka kwa mwingine.
Tusipende kujipa sifa za kitoto! Tz HATUNA kiwanda cha magari. Tuna viwanda vya kuunda bodi za mabasi na malori. Huwa tunaagiza magari toka kwa WATENGENEZAJI WA MAGARI yakiwa chassis ( chassis= frame and engine), halafu sisi tunayaundia bodi ya lori/basi. Hatujawa na uwezo wa kutengeneza chassis ambayo ndio gari yenyewe.
Halafu huu ujinga wa kila jambo linalofanyika anapewa rais sifa tunapaswa kuondokana nao. Tusiwe kama watoto ambao wanaamini baba au mama yao anaweza kufanya chochote hata kuhamisha mlima.
Huu ujinga ulianzia kwa aliyejobatiza jina 'jiwe'. Tuliaminishwa kila kitu anafanya yeye. Miundombinu tunajenga kila siku tangu tupate uhuru, lakini media zikaminywa na kulazimishwa kutoa sifa za uwongo mpaka wakataka kumuongezea muda. Eti akistaafu hakuna atakayeweza kuvaa viatu vyake. Sasa Mungu amefanya yake, na kila kitu kinaendelea.
 
Duh.....
 
Praise&Worship Team.
 
Gari inatengenezwa kwa siku 70?

Acha utoto wewe. Toa sifa kwa rais anaestahili. Heko Hayati JPM.
Huyo nyumbu anadhani akimsifia Samia atakuwa amemkomoa Magufuli wakati Tanzania ya viwanda wameanza kuiimba wote tangu 2015
 
Kwahio mkuu NIT wameunda hadi engine?
 
Mbona kuunda basi ni kitu simple sana kujifunia ni kutaka kuchekwa na wenzetu.
Ukiwa na grenda, welding machine unashindwa vipi kuunda.
 
Hizi zipo advanced kuliko hizo za moshi, ndo maana wapo NIT kutafuta roadworthy certificates, ni kama jamaa wanataka kufanya vitu kwa umakini zaidi
Waweke bei reasonable Ili tusipeleke pesa China kununua body za miaka 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…