Nimekwazwa na bandiko la Robert Mtibeli linalosema eti 'Wanaume na Wanawake wako sawa kiakili', - Siyo kweli

Aisee mjadala umekuwa mzuri sana. Naona watu wanapepetana Ile kinoma nima moja saa nane usiku aisee.
 
Abee umeniita ndugu.

Umeibua kitu ambacho ni cha kitaaluma, mimi kama sio wa taaluma husika ni ngumu kukielewa. Hiyo sio generally knowledge inahitaji diving.

Kesho ukipata muda unaweza kufafanua zaidi?
Sio mzuri sana kumuelewesha mtu ila ina a layman language ni kwamba biology(anatomy) inatuambia Seli hai za Utendaji kazi za Ubongo(neurons) zipo kwa kiasi kikubwa kwa ME ukilinganisha na KE in general population.

Pia brain volume ipo hivyo hivyo.

Na wingi wa Seli hai za Ubongo na ujazo wake vinahusishwa Moja kwa Moja na Akili(intelligence). Na hii anatomy(biology) haibadiliki vizazi na vizazi.
Para mbili za mwisho nina cha kucomment nitafanya hivyo kesho .
Nitashukulu, napenda kusoma , humu Kuna watu wananondo aisee Hadi una appreciate.

Lakini Kuna kitu nataka pia uje unifafanulie... Huwa Kuna utetezi kuhusu historical gap lililopo Kati ya ME na KE hasa Kwenye mambo ya science na gunduzi na vumbuzi nk.

Ila Mimi nataka kujua how that gap arise from the first place.!!!!
Mimi namuona Mwanamke wa kwanza kabisa na mwanaume wa kwanza kabisa wote walikuwa na equal chance ya kuinstall superiority but kwanini patriarch ika-rise na sio matriarch??

Nakusudia those earlier times hakuna social constructs hakuna mifumo kandamizi hakuna chochote binadamu ndo anaanza civilization yake.

Why Patriarch overtake matriarch at that time???

And for this overtake can't we for whatever the reasons recognize this as a natural Gender superiority???

Mwisho tujaribu kutrace au kufikili tuu jee kulitokea Upinzani wowote au kutukukubali?? Nazungumzia haya from the first place yaani kule mwanzo kabisa sio baada yake.

Ahsante
 
( Kuna comments nitazipunguza, watu wakijakusoma huu mjadala watakutana na mashambulizi binafsi kati yangu na wewe na hayana msingi, like we could have focus with the topic on the table)
I get that.
Nimecheka sana🤣.. Why do you have to care about peoples judgements?

This is a discussion my friend opened up to criticism na majibizano, you can't run away from thaat. Ukifuta haina maana watu watatrace kupitia quotes za wengine pia.

Rafiki we all have flaws that ignoring them is a disservice both to us and those who look upon us.

I wanna crack you open, mpk ego ijidharau yenyewe.. (joking) 😀 anyways I'll get to your other comments baadae
 

Upo sawa, zamani ulimwengu ulihitaji masculinity for survival, mwanamke asingeweza kwenda porini kuwinda swala ama kufukuza wanyama wakali wakiwavamia kwenye mapango walimoishi. Kwa hiyo kuwa provider wa ulinzi na mahitaji ya ndani lilikuwa jukumu la mwanaume..
Hii umeita nature ni sawa kabisa

Ila teknolojia inazidi kubadilisha kila kitu, leo hii mtu yupo ndani anaongea instagram na anaingizia pesa.

Jambo lililo wazi Teknolojia inazidi kufanya demand ya masculinity kuwa ndogo sana kiasi kwamba wanawake nao wanaweza kufanya mambo ambayo wasingeweeza kufanya zamani.
Pia wanaume kutokana na kuondoka yale mazingira magumu yaliypwaforce kutumia masculinity yao nao wanaanza kuwa feminine. Mfano angalia miili ya mwanaume wa leo na wa zamani ni tofauti hivyo, wanaume kushindwa kutimiza majukumu ya wanaume wa zamani ikiwemo security inayohitaji physical muscles. Angalia tu Dar, kibaka mdogo anaukalisha mtaa mzima. Hili linawezekana kwenye mikoa inayotumia masculinity kama Mara. No way ila ndio tunapoelekea kiujumla

Yani Imefikia hatua masculinity ya wanaume ni pesa ambayo wanawake wanazidi kuitafuta. Unadhani ni nini kitatokea

Kiuhalisia dunia inazidi kuwa feminine, wanawake wanazidi kupata access na fursa. Hili gap unaloliona kama natural occurance litaondoka naturally kwa teknolojia. Japo haliwezi kuondoka completely ila litazidi kupungua siku hadi siku
 
Kuna vitu ambayo huwezi kuviondoa. Vipo ndani yetu kijinsia,

Mwanaume ana testosterone zaidi, mwanamke ana estrogen. Na zina kazi yake

Mwanamke kiasili na kimaumbile ni nurturer, na mwanaume ni perseverer

Lakini pia influence yake inatokana na jamii inavyomkuza mwanamke kama mtu anaetakiwa kubeba mzigo wa malezi na mwanaume atabeba provision..

Kwa hiyo hii inaathiri hata mwanamke anavyokua na choices zake kulinganisha na mwanaume.

Lakini siku zinazidi kubadilika na nini kinaingiza faida zaidi vinazidi kubadilika.

Kuwa mkulima wa jembe la mkono au fundi mwashi haina faida kubwa kama kuwa digital marketer.

Kwa hiyo dunia inazidi kuwa feminine na teknolojia inazidi kubadili maana ya masculinity haswa kuanza kupimwa kwenye mizani ya finances ambao nao wanawake wanazidi kuingia katika utafutaji hivyo, gap linazidi kupungua..

Binafsi yangu naamini tupo katika transition inayoongozwa na teknolojia so sijui , hizi roles za mwanamke na mwanaume zitakuwaje. Au masculinity vs Femininity vitazidi kuathirika kwa kiasi gani
 
Mifumo ya kijamii na kiserikali ndio inamuwezesha mwanamke kupunguza hiyo gap. Kuna favouritism mwanamke anaipata. Tukimwondolea mwanamke upendelelo tukamwacha ashindane na mwanaume kwenye fair playing ground yaani kila mmoja atumie akili yake kui-exploit nature ili atoboe bila shaka mwanamke hawezi ku-compete na mwanaume.

Mfano mwanaume na mwanamke wanaotokea katika familia masikini ukawapa challenge ya miaka 10 kila mmoja abadilishe maisha yake from scratch. Mwanamke kuweza kushindana na mwanaume ni lazima apigwe tafu hapo katikati. Yeye mwenyewe singlehandedly hawezi.

Unamjua McKenzie Scott? moja ya wanawake matajiri duniani. Utajiri wake aliupata kupitia talaka. Aliolewa na Bezos(mmiliki wa amazon), wakatalakiana akapata mgao wa mali, akawa mwanamke tajiri zaidi duniani bila kuinua hata kidole kimoja kusaidia kuitengeneza Amazon. Hapa kwetu Jaqline Ntuyabaliwe maarufu kama klyn alikaribia kuwa mwanamke tajiri zaidi Tanzania kabla ya janja janja zake kujimilikisha mali za hayati Reginald Mengi kugonga mwamba.

Tukiondoa hii mifumo inayompa upendeleo mwanamke. Tunabakiwa na wanawake wachache sana wenye uwezo wa kuyatafsiri mazingira na kuja na majibu ya changamoto zinazowazunguka bila kuhitaji kubebwa
 
Umegusa kitu ambacho nikijaribu kumuelezea ndugu yangu mmoja kwenye comment za nyuma. Niliomba anitajie nyanja yoyote ambayo kiwastani wanawake wamewa-out perfom wanaume. Akaja na utetezi kwamba historia inaonyesha wanawake hawakuruhusiwa ku-compete. Ndipo nikamfafanulia hili suala lako hapa ulilohotaji ufafanuzi.

Hakuna mwanaume aliibuka aka-install patriarch kwenye fikra za watu na jamii kwa ujumla, isipokua natural pattern ndio iliwezesha patriarch kushika hatamu. From ancient eras mwanaume ali-solve matatizo, ali-step up kwenye kila changamoto inayoikabiri jamii, alimlinda mwanamke n.k ndio maana akamiliki hiyo nafasi ya kuwa main character.
 
Kuwa na amani bestie.Sijaudhika.Najua huwezi kuleta mada hapa ipokelewe na watu wote bila kutokea watu wakui challange na watu wanapochallange ndipo milango ya kujifunza zaidi inafunguka.

Binafsi naamini niko sahihi kabisa niliposema hata mwanamke asome vipi bado mwanaume kutoka huko maporini asojua kusoma wala kuandika atamzidi akili kwa sababu;
1)Siongelei akili zinazopatikana shuleni ila hata kama kama ningekua namaanisha akili za darasani bado ningekua sahihi kuwa mwanaume wa maporini atakua bora kiakili kwa sababu ni MWANAUME ndiye aliyeanzisha kitu inaitwa elimu.Mwanaume alitumia akili yake kugundua vitu kisha akaona iwepo shule ili watu wengi zaidi wajifunze vile alivyovigundua.Kwa hiyo mwanaume wa maporini ni mwanaume na kama sio mwanaume mimi Prida nisingeenda kusomea Education na kuitwa teacher/madam Pridah leo hii wala wewe usingekua Surgeon/injinia binti kiziwi leo hii.Point yangu ni kwamba wewe kumiliki gari haikufanyi ulijue gari kumzidi alolitengeneza.Yawezekana leo hii wewe ni injinia mahiri Tz nzima wewe ndo unayeaminika kuwa ukijenga jengo hata lipige tetemeko gani la ardhi majengo yote yatadondoka lako linabaki limesimama na mim nikachukua tuzo ya teacher bora Tz nzima ila utaona vifaa zana zoote tunazotumia kwenye fani zetu ni mwanaume katengeneza.Mwanaume asingetengeneza kobelo na pima maji huo umahiri wa kunyoosha kuta ungeutoa wapi?Ungepima na mwiko au kisu cha kukatia vitunguu?Huo mwiko wenyewe na kisu si ni mwanaume kavumbua?Hata huko jikoni tunakotambia kama sio mwanaume leo hii tungekua tunakata vitunguu kwa vijiti?Kuna mwanamke anaweza kutengeneza kibao cha nazi anzia ile chuma/kisu kinqchokuna?HAKUNA.

Usije ukasema hatukupewa fursa sawa.Kwamba tulikandamizwa,kwamba tulifungiwa jikoni tusubiri kuolewa na kuzaa.Ni kweli tulifungiwa jikoni hata shuleni tulikataliwa kwenda ila kama sisi tuna akili sawa/kuwazidi wanaume kwanini isiwe sisi ndio tuwanyime wanaume fursa,tuwafungie jikoni kisha tujipakulie minyama yote ya fursa.?

🎵🎵Kwani wao waweze (kutufungia) wana nini hata sisi tushindwe(kuwafungia) tuna nini?🎵🎵.

Kitendo cha mwanaume kutunyima fursa na hakuna kitu tuliweza fanya inadhibitisha mwanaume katuzidi nguvu na akili.Na hata pale mwanamke alipopata fursa ya kuingia darasani ni mwanaume kwa utashi wake aliona ziko faida mwanamke akisoma.

Wanawake wa zamani,wale walioshuhudia process ya mwanaume kuubadili ustaarabu wa dunia waliheshimu hata mtoto mchanga wa kiume na walijua kabisa mwanaume akili yake ni kubwa zaidi na ndio ukweli sababu sayansi imedhibitisha kuwa ubongo wa mwanaume ni bora zaidi ya wa mwanamke.Hiyo device yenyewe unayotumia kupinga kuwa mwanaume wa porini hakuzidi akili nina hakika elements zote zilizotumika
kuiunda waliozitengeneza majina yao Me ni 98.9% zilizobakia ndo ke au yawezekana zote zimetengenezwa na Me.

Hebu jitizame hapo ulipo,vyote ulivyovaa kuanzia wigi hadi pichu,mapambo,perfume,makeup then jiulize nani wa kwanza kukutengezea,namaanisha kuanzia kugeuza pamba hadi iwe pichu au hiyo jeki hapo kifuani.Ni mwanaume.

2)Akili ninayoongelea ktk bandiko langu ni akili ya maisha kwa ujumla.Mambo yote makubwa duniani yamefanywa na wanaume na wote tunajua.Hapo mtaani kwako unapoishi,chunguza,majina ya wanayomiliki hizo nyumba yapi mengi kati ya wamiliki ke na wamiliki me?

Pia naomba nieleweke kuwa wapo ke wamewazidi me akili ila kwa idadi wanawake wenye akili kuwazidi wanaume ni wachache.

Mfano wewe udugu wangu binti kiziwi kwa muda mrefu nakuheshimu kama mwanamke mwenye uwezo kiakili.

Hongera sana maana hata kwenye hii mada kunipinga kwako kumefanya nijifunze mengi zaidi.Binafsi naona ktk wanawake waliopinga hii mada wewe umeonyesha uwezo mkubwa kama mwanamke na ingekua unaenda head to head na wanawake wenzio ungewatoa jasho tena ukiweka na hivyo viingereza vyako vya havard ila uongo dhambi mibaba ya JF inajiwezaIko vizur upstair.Unaweza usikiri ila naamini kuna vitu vingi umejifunza kupitia hoja za hii midume ulokua ukijadiliana nayo.Tukubali tu mianaume iko vizuri kichwani.Ndo ilivyoumbwa.
 
 
Sisi tunajua yuko kwako.Tunamuomba haraka😃
 
Asante🙏
 
 
Nashukuru kwa kunielewa na kufafanua zaidi🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…