Na ukimlazimisha mrudiane jiandae kwa maumivu makali zaidi ya hayo uyapatayo sasa. Kwanza shukuru Mungu wako upo salama, ujue mke mzinzi ni rahisi sana kukuambukiza magonjwa.
Rafiki yangu mmoja nimpe jina Robert alikuwa na mke mzuri tu kwa mtazamo wake, baada ya kuishi naye kwa miaka kadhaa wakapata mtoto wa kike maisha yakaendelea, walipopata mtoto wa pili Robert akaanza kuhisi mkewe anamsaliti kwa kutOmbw@ na baba mwenye nyumba walipokuwa wamepanga, akamdadusi mkewe kwa kina sana akakiri ni kweli.
Robert akaamua kutengana na mkewe kwa muda, miongoni mwa watu aliowaomba ushauri ni mimi, akaenda kucheck afya yake kakutwa yupo salama, baada ya miezi mitatu kacheck tena yupo vizuri.
Nilimshauri sana Robert asikunali kurudiana na mkewe hadi ahakikishe naye amecheck afya yake akakubali. Siku moja Robert akaniambia ameongea na mkewe wakutane wazungumze ikiwezekana wayasuluhishe yaishe nikamwambia ni jambo jema sana kutafuta suluhu ila asisahau afya ni ya muhimu.
Siku hiyo nilimtafuta sana kwa simu zake zote kutwa nzima sikumpata. Nikamtumia ujumbe mfupi wa sms uliosomeka hivi "rafiki yangu kama hujazingatia suala la afya omba Mungu akuokoe", jioni akanipigia akanieleza kuwa alikuwa na mkewe wameyajenga yameisha lakini hakuzungumza lolote kuhusu sms niliyomtumia hapo kabla. Kiukweli moyo wangu ulikosa amani sana juu yake na sikujua ni kwanini maana nilikuwa napata hisia mbaya sana.
Baada ya miezi kadhaa kupita Robert alitokwa na kijiupele kidogo dogo sehemu ya joint ya mkono wake wa kushoto, kikawa kinakua kadiri siku zilivgosonga anajikuna kinazidi kusambaa, alijaribu kutibu kwa kila njia ilishindikana. Siku moja tukaenda hospital fulani kumsalimia daktar ni rafiki yetu, doctor alipoona kile kidonda akamshauri Robert kucheck afya yake kabla hajachelewa na mambo kuwa mabaya zaidi.
Alikuwa ameshaambukizwa ukimwi, alilia sana na kujilaumu mno kwanini hakuweka msimamo siku ile alipokutana na mkewe maana tangu pale hakuwahi kukutana kingono na mwanamke mwingine yeyote. Tulifanya kazi ya ziada kumshauri maana alitamani ajimalize.
Mbeleni ilikuja kugundulika hata wale watoto sio wa kwake ni wa yule mzee mwenye nyumba wote wawili. Waliachana kila mmoja akashika njia yake. Robert alijilaumu sana kwasababu kukosa kwake msimamo kulimponza.