Nimempiga mke wangu milioni 2 kizembe sana

Sema Nini umetisha Ila siku INGINE mwambie mbona umeficha pesa na unaona tuna changamoto moja mbili Tatu ..kwanini usitoe tu solve mambo yakae sawa ..au mke wako ndio wale wa privacy Sana Yani ukimuliza ata mind. Ila wanawake bana. Akili zao wanazijua wenyewe banaa ..Mimi ndio maana napiga nasepa ..Kama watoto nabeba nalea mwenyewe kwani Shi ngapi..??!
 
Ni ujinga mkuu baba familia unakua jizi af anafanya justification zisio kua na mantiki, sijui tunaelekea wapi kwa kweli
Binafsi Huwa ninafanyaga baadhi ya arguments na Mzee wangu, ambaye namshukuru Mungu kwa kumweka hai mpaka sasa. Huwa ananiambiaga kama kijana wake, mwanaume ni lazima uwe na high bar kwenye maswala ya kimaadili na hekima kama baba, mwanaume ni lazima awe na busara kwelikweli na uongozi usio na hitilafu na mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yenye mantiki pasipo mabavu maana yeye ndo symbol ya familia nzima, Ili pale familia inapopata changamoto nzito na ngumu aweze kuwa kimbilio na source of wisdom, solution, and stability.

Mwanaume akishakosa moral authority kwa kujihusisha na mambo ya hovyo atatengeneza instability ndani ya familia kupitia chaos either baina yake na mke wake au watoto, atadharaulika kutokana na uovyo wake na hakuna atayemsikiliza Wala kumheshimu Ikiwemo mbwa wake mwenyewe. Mwanaume akiwa mdokozi na mwenye makandokando ya kijinga Hana tofauti na kibaka wa mtaani. Baba ni lazima achape kazi kwelikweli Ili amtunze mke wake, wazazi wake,jamii inayomzunguka na watoto wake kwa juhudi na maarifa.
 
Up sio uwizi ..wewe hujapata changamoto bado ..au bado unakula kwa babako ndio maana unasema hivi ..Ila ukioa ndio utajua ndoa Ni zaidi ya kuwa mwaminifu.
Mdogo wangu acha tu lazima tuwe na discipline/respect/principles kwa wake zetu, nothing can justify wizi kwa nìni usiombe pesa, kama hataki kukupa c ya kwakwe? Huo ndo wanaumme wewe ulitegemea nani akusaidie majukumu ya Kua Baba.
 
Akili mkichwa mtu wangu
 
Binafsi Huwa ninafanyaga baadhi ya arguments na Mzee wangu, ambaye namshukuru Mungu kwa kumweka hai mpaka sasa. Huwa ananiambiaga kama kijana wake, mwanaume ni lazima uwe na high bar kwenye maswala ya kimaadili na
Baba lazima uwe model ya familia mfano wa kuigwa kwa watoto na mke,.... sasa utakua je mdokozi af wizi wa ndani ya fimilia hiyo ni kama laanat
 
Hongera wanaokulaumu hayajawafika, hela za ke wengi NI ngumu kweli kutoka hata katika matumizi ya nyumbani, kuna jamaa anaacha kodi ya meza haitumiki kabisa na jioni anawahiwa kwa simu kwamba akirudi asisahau maandazi watakunywa chai usiku, hata mtoto akiumwa hatoi pesa lake NI mume atoe hana akakope ili mtoto atibiwe

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 

Labda ni mke wako tu ndiyo yupo hivyo!
 
Mdogo wangu acha tu lazima tuwe na discipline/respect/principles kwa wake zetu, nothing can justify wizi kwa nìni usiombe pesa, kama hataki kukupa c ya kwakwe? Huo ndo wanaumme wewe ulitegemea nani akusaidie majukumu ya Kua Baba.
Mke nadhani ndiye msaidizi namba moja wa mume wake,suala la eti una mke,umezidiwa majukumu,unamuomba msaada anakukatalia,kisa pesa ni ya kwake,huyo ni wanini sasa ndani kwangu?

Yaani niende nikadharaulike huko mtaani,nayeye anao uwezo wa kunisaidia halafu anakataa,hapana kwakweli,tena hawa wanawake ambao wakimpenda bodaboda au dereva bajaji,safari ya buku 8,dereva anapewa elfu 20?Hapana kwakweli,ndiyomaana hata wadada ambao ni waajiriwa,mi huwa naona wanaowashobokea kuwaoa,eti wanaweza kusaidiana kwenye majukumu,huwa nawashangaa,ni bora uoe mama wa nyumbani tu,alee watoto ipasavyo,na ujue mimi ndiyo kila kitu.
 
Hongera Dokta Sunzu....hio ni akili kubwa na umeishi nae kwa akili sana huyo mwanamke. Ni ujuha kwa mwanaume aka MCHUNGAJI WA FAMILIA kutokujua masuala nyeti ya mkeo kama pesa zake na mienendo yake kiujumla.

MCHUNGAJI (Mume) haulizwi MCHUNGWAJI (mke na watoto) , ila yeye ndiye anayewauliza. Mwanamke hatakiwi kujua pesa uliyonayo ila wewe mwanaume unatakiwa kujua pesa alizonazo mwanamke wako. Mwanaume ni mfano wa Serikali (kiongozi) na mwanamke ni mwananchi tu wa kawaida anayeongozwa. Serikali ni lazima iwe na kitengo cha intelejensia (upelelezi) kujua taarifa za wale inayowaongoza.

Kinyume na hapo hiyo inakuwa serikali dhaifu (mwanaume dhaifu/zezeta)
 
Sawa umesikika lakini kwanini uibe? Mke ni mtu muhimu katika familia akipoteza uaminifu wake utakua umepoteza dira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…