Nimempiga mke wangu milioni 2 kizembe sana

Nimempiga mke wangu milioni 2 kizembe sana

Mwanamke wa kiafrika yeye ameshajiwekea sheria kuwa lazima akikuomba hela mume umpatie kwa wakati huo huo kama huna we kakope ila umpe tu. Ila yeye yake asikupe sababu uliumbwa uteseke kwa ajili yake. Huu ujinga nimeukataa.

Sasa wakati mwengine mambo yakiwa magumu labda itokee huna chanzo tena cha kipato ama ajira imefikia ukomo ndio utajua hujui sasa. Imagine mnadaiwa kodi almanusura mfukuzwe ila unajua mke ana 8m ndani na kajikausha anasema hana hata shilingi 1OO.

Umejitahidi kwa namna zozote huoni jinsi mke yuko radhi mdhalilike ila kwa ubinafsi tu hela yake isitumike hata senti 5. Wakati umeendesha familia kwa zaidi ya miaka 15 bila kutegemea hata dala yake.

Huyu mtu akipigwa mi sioni tabu kabisa.
shida wanaume hatuwi wawazii mkuu mtu unajua kabisa hela ushatumia kwenye mambo ya kifamiliaa sijui kulipa kodi mara adaa lakini unashindwa kummwambia mwenzio nimekwamaa... mwanamke nae akikuomba hela unaona bora ukope umridhishe yeye kuliko kusema ukweli hela hunaa
 
Mbona ulivyompa hio idea alitoa hela? Au ukimuuliza huwa anasema hana hela? Kukubali kutoa hela yake kununua shamba ameonesha Hana issue.
Hilo shamba si litakuwa na title deed yake, kwani ni la familia sasa 😂😂😂
 
Mi nashangaa watu wanaongea habari za moral authority lkn wengi wao wana michepuko au wamewahi kuwa na michepuko. Hivi mnajua huo nao ni wizi? Ni sawa na umeiba penzi la mkeo na kupeleka kwengineko. Hivyo, mnavozungumza hapa muhakikishe mpo clean dhidi ya makandokando.

NB. Sitetei wizi. Jamaa aliatakiwa amchane mke wake kuwa kwanini anaficha pesa yeye anahangaika kukopa huku na kule kwa ajili ya ugonjwa wake mwenyewe. (Binafsi mimi mke wangu, hana hata chembe ya ubinafsi kwenye maswala ya pesa)
Kwa mkeo sio mbinafsi ni rahisi kumwambia una shida ya hela akakupatia tu ila kwa wale wa mizinga fm. Mke anaomba hela kama kahaba yani na hapo hapo anafanya kazi nzuri tu ya kumudu mahitaji yake.
 
Fact, ukweli na uwazi ndio wake zetu wanataka. Kama wewe mwenyewe unaficha ulichonacho, usitarajie mkeo awe muwazi kwako hata siku moja. Mimi binafsi huenda mke wangu ni muwazi kwangu kwasababu kila jambo tunalipanga pamoja na tunaenda pamoja katika kulitekeleza. Kila mali tunayonunua tunaandika majina yetu sote, zipo zingine namwandika yeye peke yake kwa ajili ya kumpa moyo kutokana na kujitoa kwake ndani ya familia. Mwanaume kuwa mkweli na muwazi ni nguzo muhimu katika kujenga familia ya mwili mmoja
Ni vyema nyie kama mnaishi kizungu. Ila kwa waliooa wanawake wenye ubinafsi wa kijinga itakuwa kazi. Mke anapambana kuwa superwoman ili akuvimbie ndani 😂😂😂
 
Hahahahahah jitu mkewe anaamka asubuhi na yeye wakienda wote vibaruani ila ikitokea dharura ikiwa jamaa amesafiri eti mke anatwanga simu. Baba fulani tuma hela kuna hili limetokea.

Aisee tujitahidi kuoa wanawake wanaotuelewa na kutupenda kwa dhati ya moyo. Mke hana hata chembe ya kujistukia eti yeye sindo mwanaume afanye yeye. Mtoto anatakiwa elf 5O ya school bus mzee hayuko au hitaji lolote la shule mama mtu anapiga simu kwa mzee akiwa kikaoni Arusha. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yet unasema una mke hapo. Bomba limepasuka kwa sababu ya presha ya Dawasco inahitajika replacement mke hadi apige simu na hela anazo na fundi yuko ikiwa mie niko porini?

Eti hela ya mke ni yake haitakiwi kuguswa, endeleeni kuwajaza ujinga. Kwangu mie mke ni asset lazma iwe na manufaa ya kijamii na hata kiuchumi. Sio kwa kumlazimisha au kumuibia ila ntahakikisha nae anachangia maendeleo yetu.
Espy Atoto ndio anatuita mafurushi tukiwa na mtazamo kama huu wako

Sema nini bora niwe furushi [emoji3] kiroho safi
 
Kama mwanamke unafanya kazi halafu hela zako hazichangii kwenye ustawi wa familia yako ni bora ukae nyumbani tu. Wengine tuko proud kabisa kuchangia maendeleo ya familia. Kila siku unaenda kazini kufanya nini sasa. Wanawake tuache ubinafsi . Mtu unashindwa kununua hata umeme au kulipia maji. Sisi tumezaliwa kijijini huko lakini baba na mama walishirikiana kutulea sisi mpaka tukasoma vizuri. Ingekuwa baba anabeba majukumu yote sijui kama tungefika hapa tulipo. Na waliisha pamoja mpaka kifo kikawatenganisha. Dada zangu wote pia nimeona walivyo bega kwa bega na waume zao na unaweza kuona jinsi maisha yao yalivyo mazuri.
Huu ndio usawa unaotakiwa mkuu, sio kudai 5O/5O ya kuachiwa usawa kwenye fursa za kimaisha halafu linapokuja swala la kuhusu uchumi baba anaachiwa akomae kuujenga mwenyewe huku mke nae anazalisha ila hachangii chochote zaidi ya kuongeza wategemezi (watoto) na kumtwisha jukumu baba pekeyake.

Matokeo yake kunakuwa na mstari flani kati ya mke na mume badala ya mshikamano. Huu ujinga hapana kabisa. Mke anaenda kazini akihitajika kuchangia anytime achangie. Sio kuficha ficha hela. Ubinafsi wa kijinga sana.
 
Umenena vyema sana. This is a matured mind. Umeweza linganisha vizuri sana mabadiliko ya nyakati. Watu wengi wanaleta mifano ya Saudi arabia ambako mwanamke hata kuendesha gari haruhusiwi. Huku kwetu mazingira hayo haya apply, jamii imetoa fursa sawa na zaidi sana mwanamke amepewa fursa zaidi hadi za upendeleo. Katika mazingira haya mke na mume wanapaswa kuwajibika kikamilifu kwa hali na mali zao ndani ya familia bila kuhitaji kukumbushwa.
Tena hali imekuwa mbaya sababu ya "women are highly encouraged" matokeo yake tuna raisi mwanamke kabisa leo hii!

Vijana wengi hawana kazi mtaani kama ilivyo kwa watoto wa kike. Sasa imefikia hatua mama ni teller wa bank bwana ni fundi madishi au dereva wa bolt boda boda. Sasa kwa hali kama hii unategemea mume ataweza lipia ada za "Christ the King" mwenyewe?

Lazma at sometime utaomba assist.
 
Kwa ufupi sana.

Kuna wakati wife alipata changamoto ya kiafya. Matibabu yalikuwa gharama kidogo kutokana na safari za hapa na pale. Kuna wakati akiba ikakata ikabidi nijikopeshe kupitia vyanzo vingine.

Siku moja nikachukua kadi na kuchungulia akaunti yake nikakuta ina milioni saba imetulia. Ikaniuma sana. Baada ya miezi mitatu nikachngulia tena nikakuta ile fedha bado imetulia.

Juzi kati tukapata shamba kwa milioni tatu. Nikampa idea ila nikampanga shamba linauzwa milioni 5. Akaikubali akanipa milioni 2 nimalize kazi.

Nikamaliza biashara na mkataba ukasoma 5m mwenye shamba akachukua 3m. Nikapiga 2m bila kelele.

My Take
Wake zetu mnaficha hela ili iweje? Kuweni mstari wa mbele kushughulika na changamoto za kifamilia

Umepigwa
 
Huu ndio usawa unaotakiwa mkuu, sio kudai 5O/5O ya kuachiwa usawa kwenye fursa za kimaisha halafu linapokuja swala la kuhusu uchumi baba anaachiwa akomae kuujenga mwenyewe huku mke nae anazalisha ila hachangii chochote zaidi ya kuongeza wategemezi (watoto) na kumtwisha jukumu baba pekeyake.

Matokeo yake kunakuwa na mstari flani kati ya mke na mume badala ya mshikamano. Huu ujinga hapana kabisa. Mke anaenda kazini akihitajika kuchangia anytime achangie. Sio kuficha ficha hela. Ubinafsi wa kijinga sana.
Na wznaume wakiendekeza eti hela za mwanamke ni zake huku anafanya kazi mtakufa kwa pressure kwa kuzidiwa na majukumu.
 
Back
Top Bottom