Bodhichitta
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 315
- 762
Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.
Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.
Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.
Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.
Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.
Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.
Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.
Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.
Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.
Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.
Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.
Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.
Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.
Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.
Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.
Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.
Ameeeen!