Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7

Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7


Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.

Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.

Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.

Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.

Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.

Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.

Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.

Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.

Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.

Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.

Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.

Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.

Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.

Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.

Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.

Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.

Ameeeen!​
Hongereni wote. Kila la kheri mdau..
 
Hongera.
Ushauri mwingine ni kama wa nguvu za giza.
Utapata pia watoto wengine. Kila jambo lina wakati wake
Mama mmoja na mme wake pale mbeya walingojea watoto kwa miaka mingi tena wakiwa na ukwasi mkubwa.

Walikuja kupata baada ya miaka saba ya ndoa. Sasa ni wakubwa na walikuwa wanazaa mapacha.

Achana na hao wapunga pepo, je wao wanaamini nini kuwa watoto wote ni wao?
 
Hongera sana Mkuu, nikusihi tu kwamba Furahia zaidi na zaidi kwa kupata mtoto huu ni wakati wako kuiona dunia ni sehemu yenye furaha na salama kwako kuishi.

Puuza hizi tahadhali unazopewa kwa sasa maana zitakufanya ushindwe kuwa na amani katika familia yako pasipo maana yoyote kwa sasa. Kama kuna lolote lenye utata lije baadae sio sasa.

Mungu awajaalie afya njema mama na kichanga chake. ENJOY
 
Anyway nimeshashuhudia wanawake wawili wakibebeshwa mimba na wanaume tofauti wasio na waume zao kwenye ndoa, mmojawapo kati ya hao ana mtoto wangu nilifanya kumsaidia baada ya kuniambia changamoto alizokuwa akipitia kwenye ndoa yake nikaona hili jukumu nilibebe tu.

Tumekubaliana na yule mwanamke akitaka mtoto wa pili arudi tena kwangu, ili mtoto wa pili awe na ufanano na huyu wa kwanza, sio akazae hovyo leo baba wa mbagala kesho wa ilala, haitakuwa vizuri.

By the way, mwanamke kuzaa nje ya ndoa hapa mjini ni kawaida sana, wengi hufanya hivyo iwe mume wake ana tatizo la uzazi au hana, tusidhani mababa walezi wote ni wale wenye matatizo ya uzazi, hata marijali pia tunaweza geuzwa mababa walezi, ni jambo la sekunde tu, wanawake ndio wanajua kila kitu, sisi ni vipofu tu.

Hii dunia tuiache kama ilivyo, pamoja na yote hapo juu mtoto wa kiume uliyempata anaweza kuwa ni wako 100%, ishi kwa amani na mkeo hasa kwa wakti huu akiwa kwenye uzazi.
Mimi kila mara nawazalisha wake za watu, Kiufupi mjini hapa asilimia 3.4% ya watoto wanazaliwa baba yao ni mimi
Cc : ephen_
 
Nakushauri upime DNA ili kujihakikishia umiliki wa huyo mgeni mpya aliyewasili hapa duniani leo hii.
Kipimo Cha furaha uliyonayo leo hii itakuwa sawa sawa na kipimo Cha huzuni utakayopata wakati utakapokuja kugundua kwamba kumbe wewe ni baba mlezi tu wa huyo mgeni mpya aliyewasili.

Kwa leo sitaweza kukupongeza kwa ugeni wako huo hadi hapo baadaye nitakapopata majibu ya uhakika ya DNA Test kuhusu huyo mgeni wako.
Ukisikia uchawi ndiyo huu sasa
 
Hongera.
Ushauri mwingine ni kama wa nguvu za giza.
Utapata pia watoto wengine. Kila jambo lina wakati wake
Mama mmoja na mme wake pale mbeya walingojea watoto kwa miaka mingi tena wakiwa na ukwasi mkubwa.

Walikuja kupata baada ya miaka saba ya ndoa. Sasa ni wakubwa na walikuwa wanazaa mapacha.

Achana na hao wapunga pepo, je wao wanaamini nini kuwa watoto wote ni wao?
au je wao ni watoto wa baba zao?
 
Kuna wasaga sumu humu 🤣🤣mtu kakaa miaka saba ...seven ocloko bila mtoto hivi unadhani ni mchezo.Maana kejeli za ndugu majirani zote uzifumbie macho si kazi rahisi maana utaitwa majina yote mabaya mara mkeo alikua malaya huyo alikaanga mayai na dawa za kuzia mimba,mkeo alitoa sana mimba na alikua anakutana na wanaume wenye uchi mkubwa sasa kizazi kimesogea ..ukija kwako sasa ohoo ww mwanaume suruali kitu kinatepweta huna lolote unamchafua mtoto wa watu tu ebwana kila tusi la kukufehesha utatukanwa.Kaka Mungu kakuona leo mpende sana mkeo na mtoto wako maana hao ndo familia yako.
 
Back
Top Bottom