Anyway nimeshashuhudia wanawake wawili wakibebeshwa mimba na wanaume tofauti wasio na waume zao kwenye ndoa, mmojawapo kati ya hao ana mtoto wangu nilifanya kumsaidia baada ya kuniambia changamoto alizokuwa akipitia kwenye ndoa yake nikaona hili jukumu nilibebe tu.
Tumekubaliana na yule mwanamke akitaka mtoto wa pili arudi tena kwangu, ili mtoto wa pili awe na ufanano na huyu wa kwanza, sio akazae hovyo leo baba wa mbagala kesho wa ilala, haitakuwa vizuri.
By the way, mwanamke kuzaa nje ya ndoa hapa mjini ni kawaida sana, wengi hufanya hivyo iwe mume wake ana tatizo la uzazi au hana, tusidhani mababa walezi wote ni wale wenye matatizo ya uzazi, hata marijali pia tunaweza geuzwa mababa walezi, ni jambo la sekunde tu, wanawake ndio wanajua kila kitu, sisi ni vipofu tu.
Hii dunia tuiache kama ilivyo, pamoja na yote hapo juu mtoto wa kiume uliyempata anaweza kuwa ni wako 100%, ishi kwa amani na mkeo hasa kwa wakti huu akiwa kwenye uzazi.