Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7

Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.

Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.

Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.

Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.

Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.

Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.

Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.

Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.

Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.

Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.

Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.

Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.

Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.

Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.

Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.

Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.

Ameeeen!​
Wasikutie kinyongo wala kukukatisha tamaa watu wa humu, hongera sana na Inshallah Mwenyezi Mungu amjaalie awe mtoto wa kheri na upate wengine pia.
 
Na
Najua mkeo amepitia mengi Sana hasa kutoka kwa ndugu zako mwenyewe.
Mimi Sasa hivi ndugu yangu ni mke wangu na watoto nilio wazaa mwenyewe. Full stop.
Mtu unamuona ndugu wa damu kumbe unafiki umejaa moyoni mwake, ukimnunulia mkeo gari roho zinawauma kisa walitaka uwanunulie wao. Hata MTU kuja kwangu sitaki. Tutakutana kwenye misiba.

Bro mpe pole Shem kwa aliyopitia maana ameitwa kila jina baya. Hao wanafiki wakija kumuona waambie, amepumzika njooni siku nyingine.
Nikweli mkuu
 
Anyway nimeshashuhudia wanawake wawili wakibebeshwa mimba na wanaume tofauti wasio na waume zao kwenye ndoa, mmojawapo kati ya hao ana mtoto wangu nilifanya kumsaidia baada ya kuniambia changamoto alizokuwa akipitia kwenye ndoa yake nikaona hili jukumu nilibebe tu.

Tumekubaliana na yule mwanamke akitaka mtoto wa pili arudi tena kwangu, ili mtoto wa pili awe na ufanano na huyu wa kwanza, sio akazae hovyo leo baba wa mbagala kesho wa ilala, haitakuwa vizuri.

By the way, mwanamke kuzaa nje ya ndoa hapa mjini ni kawaida sana, wengi hufanya hivyo iwe mume wake ana tatizo la uzazi au hana, tusidhani mababa walezi wote ni wale wenye matatizo ya uzazi, hata marijali pia tunaweza geuzwa mababa walezi, ni jambo la sekunde tu, wanawake ndio wanajua kila kitu, sisi ni vipofu tu.

Hii dunia tuiache kama ilivyo, pamoja na yote hapo juu mtoto wa kiume uliyempata anaweza kuwa ni wako 100%, ishi kwa amani na mkeo hasa kwa wakti huu akiwa kwenye uzazi.
Hiyo paragraph ya mwisho ndo nimeielewa mkuu, hayo mengine ni ujinga mtupu.
 
Nakushauri upime DNA ili kujihakikishia umiliki wa huyo mgeni mpya aliyewasili hapa duniani leo hii.
Kipimo Cha furaha uliyonayo leo hii itakuwa sawa sawa na kipimo Cha huzuni utakayopata wakati utakapokuja kugundua kwamba kumbe wewe ni baba mlezi tu wa huyo mgeni mpya aliyewasili.

Kwa leo sitaweza kukupongeza kwa ugeni wako huo hadi hapo baadaye nitakapopata majibu ya uhakika ya DNA Test kuhusu huyo mgeni wako.
Dah!
 
Nilikua naitafuta hii comment.
 
mshukuru Mungu wa kweli, usimshukuru huyo mungu wa kiarabu. pia, subiri akue, sitaki kukukatisha tamaa. punguza munkari. sitaki kufafanua zaidi ya hapo ila mshukuru Mungu kwa ajili ya mkeo pia.
Mungu wa kweli ni yupi? Mbn unakuw mshamba mshamba mdgo angu karne ya 21 unamlazimisha mtu kuamini kitu unachoamini wewe, umelewa ??
 
Najua mkeo amepitia mengi Sana hasa kutoka kwa ndugu zako mwenyewe.
Mimi Sasa hivi ndugu yangu ni mke wangu na watoto nilio wazaa mwenyewe. Full stop.
Mtu unamuona ndugu wa damu kumbe unafiki umejaa moyoni mwake, ukimnunulia mkeo gari roho zinawauma kisa walitaka uwanunulie wao. Hata MTU kuja kwangu sitaki. Tutakutana kwenye misiba.

Bro mpe pole Shem kwa aliyopitia maana ameitwa kila jina baya. Hao wanafiki wakija kumuona waambie, amepumzika njooni siku nyingine.
Pole mkuu inaonekana ndugu wamekuumiza sana. Mkeo hawezi kamwe kuwa ndugu yako, yeye atabaki kuwa mke wako. Hivi viumbe vikifika miaka 45 vinaanza KUPIGANIA UHURU!
 
Uharo mtupu ulio andika hapa. Uchukie Hadi na wazazi kisa mkeo?

Wanaume kama wewe ukifa Leo sa2 asubuhi huyo mkeo ataolewa baada ya mazishi yako tu halafu Watoto wako watazagaa kama Watoto wa Bata.

Heri ungetukuza wazazi wako kwanza then mke. Ambae hata Sasa Hivi mkizinguana utaoa mwingine hata kesho
True yaan chukia nduguzo wote ila sio wazazi wako never usifanya ivo
 
Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.

Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.

Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.

Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.

Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.

Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.

Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.

Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.

Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.

Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.

Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.

Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.

Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.

Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.

Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.

Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.

Ameeeen!​
Hongeraaaa
 
Back
Top Bottom