Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7

Asante mkuu,
Wala siwezi kufanya hayo, aliyenipa ana maana zaidi kuliko hayo maneno ya wajinga.

Nimemuomba(mungu) amenipa alafu niwe na mashaka juu ya kunipa kwake? Si nitakuwa nakufuru mkuu

Acha waseme na waongee, furaha yangu imeziba masikio Kwa ujinga wao

Waache wajifurahishe
 
Hongera sana chief na Kila laheri kwenye malezi.
 
Uzi ufungwe,,,unajitambua sana
 
Mkuu wew ni wamaana sana.

Mungu akuzidishie busara, nimeyashika maneno yako.
 
SIMP!! yaani unapelekeshwa mpaka unawasahau ndugu wa damu? Pamoja na changamoto zao, hupaswi kuwatenga hata siku moja. Huyo mkeo hata kesho anaweza kuondoka na hakuna kitu utamfanya
 
Nenda katubie hii dhambi ya kuzaa na mke wa mtu
 
Mkuu na kuelewa vizuri ila ungesema ndugu zako wa dhati ni watoto wako, mke muondowe, utakua disappointed bure mpaka upate stroke, never ever trust a woman in your life time save your mother
Kila aliye Ni quote amesema mke wangu sio ndugu yangu. Kwa upande wangu bado naamini mke wangu ndio ndugu yangu.
Ndugu zangu niliowatoa kwenye nyumba za makuti na kuwaweka kwenye nyumba zenye tiles ndio hao hao wanaonisaliti.
Me + my wife + my children. From now until further notice.
 
Safi sana,kama tahadhari ilichukuliwa na pia hiyo ya kupima DNA nayo pia ni nzuri,inaongeza uaminifu maradufu kwa wanandoa hasa pale inapojulikana kua mtoto ni wa baba huyo ambaye anadai mtoto ni wake.Katika kipindi cha kutafuta mtoto,baadhi ya wanandoa hupitia majaribu mengi,na moja ya majaribu ambayo hupitia ni kuwaza kujaribu NJE ili kujua kama tatizo lipo kwa nani,na hayo mawazo ya kujaribu nje,baadhi ya ndugu au marafiki,hutoa ushauri huo kwa wanandoa au mawazo yanamjia mhusika mwenyewe kujaribu nje,ili ahakiki.Katika hali hiyo,ikitokea kama ni mwanamke akapata ujauzito,hupata kigugumizi cha kuutoa,hivyo kuangalia namna njema,ya kuulinda na hatimaye kuleta kiumbe duniani,na hapo mwanamke ataendelea kumuweka mwanae katika hali ya usalama kwa kuendelea kumhakikishia mumewe kua MNAFANANA kweli na mawanao,na mapenzi huwa maradufu,ili kuweka sawa mambo.Sasa kwa kesi kama hii mhusika ambaye ni mwanaume,sidhani kama kuna shida ya kuongeza uhakika kwa kufanya vipimo kwenye kituo kinachoaminika cha kutolea huduma,ili kuwa na amani nyote wawili.Hii inaweza kua na tija kwa siku za mbeleni,hasa kuepusha mambo yasiyoweza kurekebishika mbeleni.Ikitokea siyo wako,bora kwenda kupandikiza mtoto hospitality kuliko kuishi na mtoto ambaye baba yake yupo mazingira ya kwako,na anakuona punguani au kakusaidi.Habari za kwanba mtoto siyo wako,huchelewa kukufikia,kwani watu wengi hukwepa kuonekana wabaya,kwa madhara yatakayoweza kutokea.
Hongera in advance kwa kupata mtoto.
 
Nikweli, Kuna swali lilikuwa linanifadhaisha saan vile ukikutana na mtu unamsalimia alafu anakuuliza watoto wanaendeleaje au unawatoto wangapi.

Saivi nitalitamani mkuu, maana Nina chakujibu
Hahahahaa.

Mimi nilikaa miaka 2 miwili tu, majirani wakaanza maneno, eti wakawa wanamwambia wife mbona huzai. Wakawa wanajibiwa Mungu akipenda nitazaa kwa sasa bado hajatoa hiyo baraka.

Mwaka uliofuata wakawa wa kwanza kuja kutupongeza.
 
Hahahahaa.

Mimi nilikaa miaka 2 miwili tu, majirani wakaanza maneno, eti wakawa wanamwambia wife mbona huzai. Wakawa wanajibiwa Mungu akipenda nitazaa kwa sasa bado hajatoa hiyo baraka.

Mwaka uliofuata wakawa wa kwanza kuja kutupongeza.
Daah! mke atakua alikua anaumia sana,safi sana kama hakujaribujaribu nje ili ahakiki kama ni mzima.
Hongera.
 
Amen mkawe wazazi wema! mtoto akue kwa hekima na kimo, kumpendeza Mungu pamoja na wanadamu.🦅 GirlTalk
 
Mzee mbona umeng'ang'ania saana DNA?

Nimekuambia uhakika ni zaidi ya DNA, we unasema kupima DNA.

Nahisi yameshawahi kukuta ila nikuambie tu kwamba so Kila mwanamke anaweza fanya kama alivyofanya huyo mke.

Sina mashaka na hili mkuu, labda liwe jambo kingine.

Wewe endelea kuwapima wakwako huyu wangu niachie
 
Hongera sana Mkûu
Hayo Mengine yapo chini yako.

NI Haki yako kuhakiki uhalali WA Mtoto au kutohakiki.

Na hiyo huja baàda ya Miaka 2-7 kama hutoona ufanano ndîo uanze kufikiri mambo ya DNA.

Lakini ushauri wàngu ni kuwa Mtoto akifikisha Miaka miwili ongeza Mwingine

Hao wanaosema pima DNA usiwapuuze wala usiwaone wanachuki na wéwe.
Wana hoja kûbwa hasa Kwa nyakati hizi.

Dunia haina huruma.

Ukweli haukimbiwi, alafu ukweli ukichelewa unaua,

Furahia Maisha yako lakini usiache kuchukua tahadhari.

Kuhusu hoja Mungu amekupa na Huwezi kupima kitu kinachotoka Kwa Mungu siô Hoja.
Vitu vya Mungu pia hupimwa na Mungu hana shida unapopima Baraka zake kutaka kujithibitishia NI kwèli zinatoka Kwàke?

Lakini hoja kûbwa ya kupima DNA zinakuwaga hizi:
1. Mtoto hafanani hata kitu Kimoja na wéwe
2. Mwanamke kutokuwa mwaminifu
3. Wanaume Wanaume wawili kugombea Mtoto mmoja.

Nabii Nuhu Wakati anazaliwa Baba yake Aitwaye Lamecki alimtilia Mashaka kuwa Nuhu siô Mtoto wake kutokana na mwonekano wa Nuhu.
Lameki akaongea na Babaake Aitwaye Methuselah, Kisha Methuselah akaenda Kwa Babaake Aitwaye Henoko. Huko akaambiwa huyo Mtoto yàani Nuhu licha ya kuwa ni watofauti lakini ametoka viunoni mwa Lameck hivyo Lamecki asiwe na hofu. Amtunze na Kumpenda Mtoto wake.

Siô Kosa kumtilia Mashaka Mtoto. Na unahaki ya Kutoa mashaka yako Kwa kujua ukweli kama hayo Mashaka Yapo kwèli
 
Daah! mke atakua alikua anaemia sana,safi sana kama hakujaribujaribu nje ili ahakiki kama ni mzima.
Hongera.
Hahahahaha.

Hayo ya kutaka nipunguze siku za kuishi, sitaki kuyafuatilia
 
i second you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…