Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante mkuu,Tumshukuru Mungu kwa kukupa furaha ya moyo wako, nakupongeza kwa uvumilivu ulionao wewe na familia yako. Mungu ni mwema sana na humjalia mja wake kwa wakati.
Ila Acha hayo mengine ya kupima sijui nini, mtoto ni wako. Acha kuiga wala kufuata hayo maneno. Endelea kufurahia upendo
Hongera sana chief na Kila laheri kwenye malezi.
Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.
Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.
Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.
Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.
Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.
Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.
Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.
Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.
Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.
Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.
Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.
Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.
Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.
Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.
Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.
Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.
Ameeeen!
Uzi ufungwe,,,unajitambua sanaAsante mkuu,
Wala siwezi kufanya hayo, aliyenipa ana maana zaidi kuliko hayo maneno ya wajinga.
Nimemuomba(mungu) amenipa alafu niwe na mashaka juu ya kunipa kwake? Si nitakuwa nakufuru mkuu
Acha waseme na waongee, furaha yangu imeziba masikio Kwa ujinga wao
Waache wajifurahishe
Mkuu wew ni wamaana sana.Najua namna gani ulivyo na furaha. Mungu aizidishe furaha yako mara dufu.
Ndugu yangu alisubiri miaka 8 bila ya mtoto. Can u imagine? Tena wote wakiwa na afya njema bila tatizo lolote. Kila kitu kipo sawa, ila mimba haikamati.
Kila upande ukaanza kuinyooshea kidole upande mwingine. Upande wa mume (sisi) tukaanza kusema ndugu yetu hana shida. Tufanye mpango *mke wa pili.
Upande wa mke unamuasa ndugu yao, agawe uroda kwa wanaume wengine. Wamfungulie jamaa njia 🤣🤣🤣. Duh!
.
Tafrani tupu. Maneno mengi sana. Lakini wenza wale waliamua kusubiri. Waliamua kuupa muda uamue.
Baada ya miaka nane ya msoto, hatimaye wakabarikiwa kupata mtoto wa kike, mrembo kweli kweli. Mchangamfu na mjanja sana. Huna haja ya kuulizia kama ni wa babaye, unahitimisha tu.
Bahati ilikuwa kwao. Walioana wangali vijana. Sasa wana watoto watano wenye furaha kubwa.
Usikilize maneno ya watu. Hawajui mateso uliyopitia. Furahia na umshukuru Mungu. Mrejeshee sifa na utukufu. Binadamu hawa wanaokutia wasiwasi ndiyo wale waliokuwa wanakusimanga wewe na mkeo. Kisa mmeshindwa hata kupata mtoto mmoja.
Leo wanaibuka na kukutia hofu, ili uendelee kuishi kwa wasiwasi. Binadamu hajawahi kueleweka.
Kila la kheri.
Nenda katubie hii dhambi ya kuzaa na mke wa mtuAnyway nimeshashuhudia wanawake wawili wakibebeshwa mimba na wanaume tofauti wasio na waume zao kwenye ndoa, mmojawapo kati ya hao ana mtoto wangu nilifanya kumsaidia baada ya kuniambia changamoto alizokuwa akipitia kwenye ndoa yake nikaona hili jukumu nilibebe tu.
Tumekubaliana na yule mwanamke akitaka mtoto wa pili arudi tena kwangu, ili mtoto wa pili awe na ufanano na huyu wa kwanza, sio akazae hovyo leo baba wa mbagala kesho wa ilala, haitakuwa vizuri.
By the way, mwanamke kuzaa nje ya ndoa hapa mjini ni kawaida sana, wengi hufanya hivyo iwe mume wake ana tatizo la uzazi au hana, tusidhani mababa walezi wote ni wale wenye matatizo ya uzazi, hata marijali pia tunaweza geuzwa mababa walezi, ni jambo la sekunde tu, wanawake ndio wanajua kila kitu, sisi ni vipofu tu.
Hii dunia tuiache kama ilivyo, pamoja na yote hapo juu mtoto wa kiume uliyempata anaweza kuwa ni wako 100%, ishi kwa amani na mkeo hasa kwa wakti huu akiwa kwenye uzazi.
Kila aliye Ni quote amesema mke wangu sio ndugu yangu. Kwa upande wangu bado naamini mke wangu ndio ndugu yangu.Mkuu na kuelewa vizuri ila ungesema ndugu zako wa dhati ni watoto wako, mke muondowe, utakua disappointed bure mpaka upate stroke, never ever trust a woman in your life time save your mother
hii dunia ukiutafuta sana ukwel utaupata ila unaweza ukuweke sehemu mbaya sana, afadhali usiujue ukwel kuliko kuujua maana unaweza shindwa kuishi nao na unaweza ukakutoa rohoUkweli mchungu unaoponya daima huwa unachoma Sana rohoni.
Ukweli mchungu unaoponya daima huwa unachoma Sana rohoni.
Safi sana,kama tahadhari ilichukuliwa na pia hiyo ya kupima DNA nayo pia ni nzuri,inaongeza uaminifu maradufu kwa wanandoa hasa pale inapojulikana kua mtoto ni wa baba huyo ambaye anadai mtoto ni wake.Katika kipindi cha kutafuta mtoto,baadhi ya wanandoa hupitia majaribu mengi,na moja ya majaribu ambayo hupitia ni kuwaza kujaribu NJE ili kujua kama tatizo lipo kwa nani,na hayo mawazo ya kujaribu nje,baadhi ya ndugu au marafiki,hutoa ushauri huo kwa wanandoa au mawazo yanamjia mhusika mwenyewe kujaribu nje,ili ahakiki.Katika hali hiyo,ikitokea kama ni mwanamke akapata ujauzito,hupata kigugumizi cha kuutoa,hivyo kuangalia namna njema,ya kuulinda na hatimaye kuleta kiumbe duniani,na hapo mwanamke ataendelea kumuweka mwanae katika hali ya usalama kwa kuendelea kumhakikishia mumewe kua MNAFANANA kweli na mawanao,na mapenzi huwa maradufu,ili kuweka sawa mambo.Sasa kwa kesi kama hii mhusika ambaye ni mwanaume,sidhani kama kuna shida ya kuongeza uhakika kwa kufanya vipimo kwenye kituo kinachoaminika cha kutolea huduma,ili kuwa na amani nyote wawili.Hii inaweza kua na tija kwa siku za mbeleni,hasa kuepusha mambo yasiyoweza kurekebishika mbeleni.Ikitokea siyo wako,bora kwenda kupandikiza mtoto hospitality kuliko kuishi na mtoto ambaye baba yake yupo mazingira ya kwako,na anakuona punguani au kakusaidi.Habari za kwanba mtoto siyo wako,huchelewa kukufikia,kwani watu wengi hukwepa kuonekana wabaya,kwa madhara yatakayoweza kutokea.Kiongozi mbona inaonekana kama una busara ila tu unajichetua!??
Ushawahi siku Moja kumshauri baba yako afanye hivo kwako au Kwa ndugu zako??
Hivi unahisi hakuna namna nyingine ya wewe mwanaume kuhakiki hili jambo Kwa mazingira??
Mim binafsi Nina uhakika mkubwa saana juu ya hili.
Nilichukua tahadhari mapema na nilimwambia mwenyewe kuhusu hili kutokana na changamoto tuliyoipata
Uhakika nizaidi ya hiyo DNA
Hahahahaa.Nikweli, Kuna swali lilikuwa linanifadhaisha saan vile ukikutana na mtu unamsalimia alafu anakuuliza watoto wanaendeleaje au unawatoto wangapi.
Saivi nitalitamani mkuu, maana Nina chakujibu
Daah! mke atakua alikua anaumia sana,safi sana kama hakujaribujaribu nje ili ahakiki kama ni mzima.Hahahahaa.
Mimi nilikaa miaka 2 miwili tu, majirani wakaanza maneno, eti wakawa wanamwambia wife mbona huzai. Wakawa wanajibiwa Mungu akipenda nitazaa kwa sasa bado hajatoa hiyo baraka.
Mwaka uliofuata wakawa wa kwanza kuja kutupongeza.
Amen mkawe wazazi wema! mtoto akue kwa hekima na kimo, kumpendeza Mungu pamoja na wanadamu.🦅 GirlTalk
Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.
Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.
Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.
Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.
Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.
Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.
Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.
Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.
Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.
Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.
Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.
Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.
Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.
Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.
Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.
Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.
Ameeeen!
Mzee mbona umeng'ang'ania saana DNA?Safi sana,kama tahadhari ilichukuliwa na pia hiyo ya kupima DNA nayo pia ni nzuri,inaongeza uaminifu maradufu kwa wanandoa hasa pale inapojulikana kua mtoto ni wa baba huyo ambaye anadai mtoto ni wake.Katika kipindi cha kutafuta mtoto,baadhi ya wanandoa hupitia majaribu mengi,na moja ya majaribu ambayo hupitia ni kuwaza kujaribu NJE ili kujua kama tatizo lipo kwa nani,na hayo mawazo ya kujaribu nje,baadhi ya ndugu au marafiki,hutoa ushauri huo kwa wanandoa au mawazo yanamjia mhusika mwenyewe kujaribu nje,ili ahakiki.Katika hali hiyo,ikitokea kama ni mwanamke akapata ujauzito,hupata kigugumizi cha kuutoa,hivyo kuangalia namna njema,ya kuulinda na hatimaye kuleta kiumbe duniani,na hapo mwanamke ataendelea kumuweka mwanae katika hali ya usalama kwa kuendelea kumhakikishia mumewe kua MNAFANANA kweli na mawanao,na mapenzi huwa maradufu,ili kuweka sawa mambo.Sasa kwa kesi kama hii mhusika ambaye ni mwanaume,sidhani kama kuna shida ya kuongeza uhakika kwa kufanya vipimo kwenye kituo kinachoaminika cha kutolea huduma,ili kuwa na amani nyote wawili.Hii inaweza kua na tija kwa siku za mbeleni,hasa kuepusha mambo yasiyoweza kurekebishika mbeleni.Ikitokea siyo wako,bora kwenda kupandikiza mtoto hospitality kuliko kuishi na mtoto ambaye baba yake yupo mazingira ya kwako,na anakuona punguani au kakusaidi.Habari za kwanba mtoto siyo wako,huchelewa kukufikia,kwani watu wengi hukwepa kuonekana wabaya,kwa madhara yatakayoweza kutokea.
Hongera in advance kwa kupata mtoto.
Hahahahaha.Daah! mke atakua alikua anaemia sana,safi sana kama hakujaribujaribu nje ili ahakiki kama ni mzima.
Hongera.
i second youNakushauri upime DNA ili kujihakikishia umiliki wa huyo mgeni mpya aliyewasili hapa duniani leo hii.
Kipimo Cha furaha uliyonayo leo hii itakuwa sawa sawa na kipimo Cha huzuni utakayopata wakati utakapokuja kugundua kwamba kumbe wewe ni baba mlezi tu wa huyo mgeni mpya aliyewasili.
Kwa leo sitaweza kukupongeza kwa ugeni wako huo hadi hapo baadaye nitakapopata majibu ya uhakika ya DNA Test kuhusu huyo mgeni wako.