Bodhichitta
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 315
- 762
- Thread starter
- #161
Kiongozi mbona inaonekana kama una busara ila tu unajichetua!??Tafiti nyingi sana zinaonyesha kwamba kiini au chanzo cha Migogoro mingi sana pamoja na vyanzo vya ugomvi au Mauaji kwa wanandoa wengi sana hapa duniani ni wivu wa mapenzi, kukosa uaminifu katika ndoa (infidelity) au Wanaume kubambikiwa watoto ambao kimsingi sio watoto wao halisi wa kuwazaa (not biological Fathers). Visa vingi sana vya Mauaji ya wanandoa hususani kwa akina mama na watoto wao huwa vinahusiana na suala la hili la Wanaume kubambikiwa watoto, mambo yanapokuja kujulikana hadharani wakati tayari mwanaume ameshaingia gharama kubwa katika malezi ya watoto ambao baadaye inakuja kuthibitika kuwa siyo wake matokeo yake huwa ni mabaya Sana kupita kiasi.
Hivyo basi, njia pekee ya kuweza kuepukana na dhahama au mabalaa kama hayo ya Mauaji kwa wanandoa ni kuchukua tahadhari kubwa katika hatua za mapema, yaani kuwapima DNA watoto wanaozaliwa, Kama matokeo yatakuja tofauti kabisa na matarajii, basi mwanaume atakuwa na nafasi ya kuweza kujiepusha na gharama zisizomhusu za malezi ya watoto ambao siyo wake. Aidha, mtoto husika ataweza kupata malezi kutoka kwa baba yake halisi. Na mwisho kabisa, kupima DNA Mapema pia itasaidia Wanandoa kuwaepusha na janga kubwa la Migogoro ya hatari kati yao ambayo mara nyingi sana husababisha madhara makubwa sana yasiyorekebishika ktk siku za usoni, ikiwamo na mifarakano mikubwa na Vifo.
Kinga ni Bora kuliko Tiba, Kupanga ni Kuchagua!
The choice is yours.
Ushawahi siku Moja kumshauri baba yako afanye hivo kwako au Kwa ndugu zako??
Hivi unahisi hakuna namna nyingine ya wewe mwanaume kuhakiki hili jambo Kwa mazingira??
Mim binafsi Nina uhakika mkubwa saana juu ya hili.
Nilichukua tahadhari mapema na nilimwambia mwenyewe kuhusu hili kutokana na changamoto tuliyoipata
Uhakika nizaidi ya hiyo DNA