Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7

Kiongozi mbona inaonekana kama una busara ila tu unajichetua!??

Ushawahi siku Moja kumshauri baba yako afanye hivo kwako au Kwa ndugu zako??

Hivi unahisi hakuna namna nyingine ya wewe mwanaume kuhakiki hili jambo Kwa mazingira??

Mim binafsi Nina uhakika mkubwa saana juu ya hili.

Nilichukua tahadhari mapema na nilimwambia mwenyewe kuhusu hili kutokana na changamoto tuliyoipata

Uhakika nizaidi ya hiyo DNA
 

Kwenye ndoa zenu kuna watoto wetu.
Huo uchokozi
 
Ramli chonganishi. Muache huyo bwana usimharibie siku yake
 
Hongera na kwa Kuzaliwa Kwake tu huko tarehe hiyo 27 kama ya GENTAMYCINE tegemea Mwanao kuwa na Nyota kali.
 
Mkuu nami naungana na wengine kukupa hongera
Nikijaribu kuvaa viatu vyako,furaha yako naiona. Hongera sana na Muombe Mungu akukuzie mwanao katika nyanja zote zaidi kimo akili na maarifa
 
Huu ni upuuzi mkubwa,,,kama ingekuwa hivyo je,huyu mwanamke angesubir miaka yote hiyo?

Wakati mimi ndani ya miaka hiyo nilikuwa na wawili

Tuache kuwakosesha furaha watu kwa mitazamo ya kipuuzi
 
mshukuru Mungu wa kweli, usimshukuru huyo mungu wa kiarabu. pia, subiri akue, sitaki kukukatisha tamaa. punguza munkari. sitaki kufafanua zaidi ya hapo ila mshukuru Mungu kwa ajili ya mkeo pia.
Huyu naye ni mpuuzi mmoja,,,kuna mungu wa kiarabu?
 
Tumshukuru Mungu kwa kukupa furaha ya moyo wako, nakupongeza kwa uvumilivu ulionao wewe na familia yako. Mungu ni mwema sana na humjalia mja wake kwa wakati.
Ila Acha hayo mengine ya kupima sijui nini, mtoto ni wako. Acha kuiga wala kufuata hayo maneno. Endelea kufurahia upendo
 
Wa kwako..??
 
Asante sana,,,uishi maisha marefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…