Nimepata Tsh. Milioni 1.3, naomba ushauri wa aina ya biashara ninayoweza kufanya

Mfano akaunti ya kampuni inaitaji signatures zenu nyote kama ni partiners na pesa yote inalipwa kwenye akaunti moja mnaibianaje?
 
Nimefanya biashara January to June,nikapata asilimia 75%,kuitunza mpaka January ijayo nimeila yote hapa nilipo nasubiri bakora za wasiojulikana sababu nimeyatimba na January Iko mbali,biashara za msimu ni kipengele
Wakulima wa korosho huko ni neema tu yaan kwa waliootea sasa hivi wanakula pension msimshangae yule mmakonde mgawa range rover 2 kwa mkupuo na kuzitupia kwenye mashimo matatu ya shangazi fulani
 
Hizo za nampa mtu utatupa pesa yako ndgu.

Bora biashara ile ambayo walau una muda nayo, vijana wanaunguza sana mitaji aisee.

Hiyo ya belo la nguo na kusepa nazo bush nimeipenda ila ukiifanya mwenyewe na iyo bonda ikusaidie chaka to chaka na kufata minada.
 
Binafsi ningekushauri ufanye hiyo biashara ya kwanza;

Saloon na kuingiza Movies na nyimbo

Kwanini biashara hii?
~Inahitaji Mtaji kidogo
~Una uhakika wa kuzalisha zaidi ya shilingi 300,000 Kwa Mwezi
~Inahitaji usimamizi kidogo, ukifanikiwa Kufunga CCTV camera utajua Kila shilingi inayoingia
~Ni biashara yenye risk ndogo
~Ni biashara inayotumia fedha kidogo za Uendeshaji(O&M).
 
Hii ya nguo nitaifanya mwenyewe kwa mikono yangu mkuu
 
Hivi utaratibu wa kufuata minada ukoje?
 
Hapo kazini kwako ndio mahali pazuri pa kuanzia , Anza kutoa mikopo midogo midogo kwa wafanyakazi wenzako isiyozidi 50k , weka mazingira mazuri kwa hr na watu wa accounts namna ya kupata rejesho. Factors nyingine kama majungu kazini watu wasiokopesheka nk ziweke kwenye mzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…